Suala Nambari 10 Linaloeleweka Vibaya
Uislamu unazalisha jamii iliyo vivu, isiyoelimika kwasababu:
- vitu vyote vinatokana na Mungu, na hivyo ni sawa kuamini hakuna hiari ya mwanaadamu-‘fatalism’
- teknolojia na sayansi ya sasa haikubaliwi
Hoja zilizotolewa kwa suala hili linaloeleweka vibaya ni za uongo, na hilo
suala wenyewe hakika limekanushwa moja kwa moja na Qur-aan na Sunnah.
Wakati ni kweli kwamba Muumba ni chanzo cha kila kitu juu yetu, lakini
sio kweli kwamba hili linaweza kutumika kuwa ni udhuru wa binaadamu
kujificha kama aya zifuatazo kutoka Qur-aan zinavyoeleza (tafsiri):
{{Na wale washirikina wanasema: “Kama
angalipenda Mwenyezi Mugnu tusingaliabudu chochote badala Yake, sisi
(tusingefanya hivyo) wala baba zetu, wala tusingaliharamisha chochote
bila Yeye (kututakia haya).” Basi kama hivi walifanya wale waliokuwa
kabla yao. Basi kuna juu ya Mitume isipokuwa kufikisha (ujumbe) wazi wazi (tu basi)?}} [16:35]
{{Na
husema: “Angalipenda Mwingi wa rehema tusingewaabudu hao (masanamu,
Ametuandikia Mwenyewe haya Mwenyezi Mungu, basi Anayapenda).” Hawana
ilimu kwa haya (wanayoyasema); hawasemi ila maneno ya kuvurumiza tu.}} [43:20]
Allaah
Ametufundisha kupitia kwa Qur-aan na Sunnah kwamba sote tuna kiwango
fulani cha uhuru. Uhuru huu ni lazima ufanyiwe kazi sawa sawa kwa mujibu
wa Qur-aan na Sunnah ili kumridhisha Muumba. Hii ni hamasa iliyo kubwa
kwa Waislamu wote kuwasukuma kuwa ni wenye ujuzi ulio bora, wanaweza
kuwa Waislamu walio imara kabisa. Kama jamii ya Waisalmu leo hawawezi
kusuluhisha matatizo yao,
basi sio kwasababu ya uelewa wao wa Uislamu, isipokuwa ni kwasababu ya
ujinga wao wa njia hii ya maisha. Umuhimu wa kutafuta elimu na kufanya
kazi yanaelezwa wazi ndani ya Sunnah.
Kutokana na Sunnah, hususan ndani ya somo la Sunnah linaloitwa Sunnah ya Abuu-Daawuud, tunaona:
Amesimulia
Anas bin Maalik: Mtu wa Answaar alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuomba, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) alimuuliza: Jee una chochote ndani ya nyumba yako?
Akajibu: Ndio, kipande cha nguo, sehemu ambayo tunavaa na sehemu ambayo
tunatandika (katika sakafu), na bakuli la mbao ambalo tunakunywia maji.
Alisema: Vilete kwangu. Baadaye alivileta vitu hivi kwake na yeye (Mtume) alivichukua kwenye mkono wake na kuuliza: Ni nani atakayevinunua hivi? Mtu mmoja akasema: Mimi nitavinunua kwa dirham moja, Alisema mara mbili au mara tatu: Nani atajitolea zaidi ya dirham moja?
Mtu mmoja akasema: Mimi nitanunua kwa dirham mbili. Alimpatia vitu hivi
na kuchukua dirham mbili, na kumpatia Answaari, alisema: Nunua chakula kwa moja yake na wafikishie ukoo wako, na nunua shoka na lilete kwangu.
Baadaye alilileta kwake. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) aliliunganisha mpini pamoja nalo kwa mikono yake na
kusema: Nenda, tafuta kuni na uziuze, na nisikuone kwa wiki mbili. Mtu yule alikwenda zake na kutafuta kuni na kuuza.
Alipopata dirham kumi, alikuja kwake na kumnunulia guo na baadhi yake
kwa chakula. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) akasema: Hili ni bora kwako (kuliko) lile, kuomba kutakuja kama
ni alama kwenye uso wako Siku ya Hukumu. Kuomba ni ruhusa kwa watu
watatu tu: yule ambaye anakufa kwa njaa, yule ambaye ana deni lililokuwa
baya mno, au yule ambaye anahusika na kulipa fidia na anapata tabu
kulipa.
Pia kutokana na Sunnah, hususan ndani ya somo la Sunnah linaloitwa Suna ya Ibn Majah, tunaona kwamba Mtume wa Allaah amesema:
Kutafuta elimu ni wajibu kwa kila Muislamu.
Ujuzi
wa Qur-aan na Sunnah ndio aina za elimu zilizo bora kabisa, na elimu
inayonufaisha binaadamu pia ni nzuri. Qur-aan na Sunnah hazizuii usomaji
wa dunia hii na ukweli Muumba Anatuhimiza kuuchunguza ulimwengu
tunaoishi kwa mujibu wa aya ifuatayo kutoka kwenye Qur-aan (tafsiri):
{{Katika
kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana, ziko hoja (za
kuonyesha kuwapo Mwenyezi Mungu Mmoja), kwa wenye akili. Ambao
humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa na wakilala. Na
huzingatia umbo la mbingu na ardhi (pia. ‘Namna gani Mwenyezi Mungu
alivyoumba.’ Wakasema) “Mola wetu! Hukuviumba hivi bure. Utukufu ni
Wako. Basi Tuepushe na adhabu ya Moto.}} [3:190-191]
na kilicho kibaya ndani yake kinatokana na sisi.
No comments:
Post a Comment
10 Ways of Protection from Shaytan:
Imam Ibn ul Qayyim
Seeking refuge with Allah from Shaytan. Allah the Most High said, “And if there comes to you from Satan an evil suggestion, then seek refuge in Allah. Indeed, He is the Hearing, the Knowing.” [41:36]
Recitation of the two soorahs al-Falaq and an-Nas, as they have wondrous effect in seeking refuge with Allah from evil, weakening Shaytan and protection from him. This is why the Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said: “No person seeks refuge with anything like the Mu`awwidhatayn (soorahs al-Falaq and an-Nas)”. [an-Nasaa’i, 5337]
Recitation of Ayat al-Kursi (2:255).
Recitation of soorah al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “The house in which al-Baqarah is recited is not approached by Shaytan.” [Muslim]
The final part of al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “Whoever recites the two last verses of al-Baqarah at night they will suffice him.” [Muslim]
Recitation of the beginning of soorah Mu’min (Ghafir), until His saying, “wa ilayhi-l-maseer” (to Him is the destination). (i.e. “Ha. Meem. The revelation of the Book is from Allah, the Exalted in Might, the Knowing, the forgiver of sin, acceptor of repentance, severe in punishment, owner of abundance. There is no deity except Him; to Him is the destination.” [40:1-2])
Saying “la ilaha ill Allah wahdahu la sharika lah, lahul mulku wa lahul hamdu wa huwa `ala kulli shay’in qadir” (there is nothing worthy of worship except Allah, He has no partner, His is the Dominion and Praise, and He is able to do all things) a hundred times.
The most beneficial form of protection from Shaytan: abundance of remembrance of Allah, the Exalted.