Hapa Tuna Kumbushana Kuhusu Uislam wetu,Tuna Habarishana Habari Mbali Mbali,Lakini Tukumbuke kwamba Uislam Hauto kwenda mbele kwa Maandamano au Kufanya Da3wa ya maneno tu,Bali Uislam utakwenda kwanjia alizo fundishwa Mtume(JIHAAD)Kuutangaza Uislam ni jukumu lakila muislam kwa hali na mali.كلكم راع وكلكم مسئول عن رعيّته/كنتم خير أمّة أخرجت للناس تئمرون بالمعروف وتنهون عن المنكر.
Followers
Thursday, December 19, 2013
Wednesday, December 11, 2013
Kumuoa Mkristo Atakayesilimu Siku YA Ndoa
SWALI:
Je inakubalika kumuoa Mkiristo atakaesilimu siku ya ndoa?
JIBU:
Sifa
zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote,
Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na
watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Hakuna
tatizo lolote endapo atasilimu kidhati, Imepokewa kutoka kwa Anas
amesema: Abu Twalha alipomuoa Ummu Sulaym, mahari yao ilikuwa ni
kusilimu, Ummu Sulaym alisilimu mwanzo kabla ya Abu Twalha,
alipomchumbia, akasema kwa hakika mimi nimeshasilimu, ikiwa utasilimu
utanioa, akasilimu na ikawa kusilimu ndiyo mahari yao" (An-Nasaaiy
6/114).
Lakini
Muislamu mwanamume awe makini na mwanamke mwenye kutaka kusilimu siku
ya ndoa, isijekuwa ni mwenye kumdanganya akawa anasubiri siku hiyo
wakati ameshatayrisha mambo ya harusi kisha amgeukie. Ikiwa hili ndilo
sharti aliloliweka huyo mwanamke basi nasiha yetu ni kuwa uwe makini na
ujaribu kuchunguza kwanza dhamira yake.
Na Allah Anajua zaidi
Mawasiliano Na Mchumba Baada Kuposa Na Kabla Ya Ndoa
SWALI:
INARUHUSIWA KUWASILIANA MARA KWA MARA NA MCHUMBA WAKO? KWA SIMU AMA BARUA AMA E-MAIL?
JIBU
Sifa
zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliyetukuka Mola
wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume
(Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya
Allahu 'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Qiyaamah.
Ama
kuhusu kuwasiliana baina ya mvulana aliyeposa na posa yake kukubaliwa
na msichana na walii wake basi hakuna tatizo lolote ikiwa mawasiliano
yao ni katika mipaka ya sheria. Hivyo, kumpigia simu hakuna ubaya ikiwa
ni katika kuyapanga yale mambo ya ndoa yao na matayarisho yake. Ama
ikiwa mawasiliano hayo yatakuwa nje ya misingi hiyo na kupelekea
kuzungumza kuhusu mahusiano na mapenzi na mengine yasiyofaa, basi ni
vizuri kujiepusha na mawasiliano hayo.
Mara
nyingi mawasiliano ya karibu kabla ya ndoa, yameleta uharibifu mkubwa
na madhara katika jamii na kusababisha posa nyingi kuharibika na hata
vatu kutumbukia katika zinaa.
Mbali
na mawasiliano hayo mvulana anaweza kwenda nyumbani kwa mchumba wake
bora tu wasikae faragha wao peke yao katika mazungumzo. Inabidi awe
pamoja nao maharimu wa msichana. Hii ni kwa sababu Mtume (Swalla Llaahu
'alayhi wa sallam) amesema: “Hakai faragha mwanamume na mwanamke ila wa tatu wao ni shetani. Na hakika shetani hutembea katika mwili wa mwanaadamu kama itembeavyo damu”.
Hii ni kuwa bado nyinyi hamjakuwa mume na mke, na mmoja kati yenu
anaweza kuvunja ndoa hiyo baada ya kuwa mmekubaliana hapo awali.
Mwanamume anaweza kusema basi hataki tena harusi au mwanamke kujibu kuwa
hakuna tena harusi.
Ile
desturi ya wachumba kuwa wanakwenda pamoja katika mabustani, sinema au
kusafiri kabla ya kuoana si desturi ya Kiislamu. Na athari yake mara
nyengine inakuwa mbaya kwani wanaweza kutumbukia katika maasi na kisha
mwanamume akasema hataki tena harusi na binti huyo. Baada ya hapo
wanaume wanakuwa wakimtweza binti kama yule na inakuwa ni vigumu kwake
kutakiwa na mume mwengine.
Na Allah Anajua zaidiUzazi Wa Kupanga Unafaa?
SWALI:
Jee Sheikh kuna njia yoyote ya uzazi wa mpangilio ya kiislam na kama ipo ni njia gani? Je, Sheikh kutumia condom kwa mke na mume ni vibaya?
JIBU:
Sifa
zote njema Anastahiki Allah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah
na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'Alayhi
Wa Aalihi Wasallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'Anhum) na
watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Hakika ni kuwa njia za mpango wa uzazi zipo katika ulimwengu huu nyingine zikiwa zinakubalika na Uislamu na nyengine hazifai kutumika. Njia ambayo haifai kutumika ni ile ya kufunga kizazi milele (permanent) isipokuwa kwa haja kubwa ambayo inakubalika kisheria kama shida ya mama katika kuzaa na mfano wake.
Njia ambayo inayokubalika ni ile ya kutumia azl (coitus interuptus -kumwaga nje maji ya uzazi). Jaabir ibn ‘Abdillahi (Radhiya Allaahu 'Anhu) amesema: “Tulikuwa tukifanya azl ilhali Qur’ani ilikuwa ikiteremshwa, habari hii ilimfikia Mtume (Swalla Allahu 'Alayhi Wa Aalihi Wasallam) naye hakutukataza” (Al-Bukhaariy na Muslim).
Wanachuoni wameafikiana
kuwa njia yoyote ya upangaji uzazi inakubalika isipokuwa ile ya kufunga
kabisa kizazi. Na mtu anatakiwa atumie njia ambayo ni salama kwa mwenye
kutumia kwa sababu zake za kibinafsi, lakini haifai kuwa ni sheria na
kanuni ya dola.
Wanachuoni wametumia Qiyaas ya kwamba kwa kuwa azl
ilikuwa inatumika kuzuia mbegu kufika kwenye uzao wa mama njia hizi
nyengine za upangaji uzazi zinaruhusiwa kwa muda kwa kuafikiana baina ya
mume na mke. Hivyo, kutumia condom inaruhusiwa. Kuhusu njia nyengine
inabidi wanandoa wapate ushauri kwa daktari Muislamu mtaalamu, mcha
Mungu ili ampatie njia muafaka na maumbile yake.
Tanbihi: Ieleweke kuwa njia nyingi za kutumia madawa na sindano zina madhara makubwa sana kwa binadamu, hivyo tuwe na tahadhari ya hali ya juu katika utumiaji wa vitu hivyo.
Kwa maelezo zaidi ingia katika kiungo kifuatacho :
Hukmu Ya Kusoma Vitabu Vya Mapenzi Na Tendo La Ndoa
SWALI:
JE KUSOMA VITABU VINAVYOZUNGUMZIA MASUALA YA MAPENZI NI SAHIHI? NA KAMA SI SAHIHI JE VYA KIDINI VINAVYOELEZEA MASUALA YA TENDO LA NDOA?
JIBU:
Sifa
zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliyetukuka Mola
wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume
(Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya
Allahu 'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Qiyaamah.
Ama
kusoma vitabu vinavyozungumzia masuala ya mapenzi havina tatizo ikiwa
vitakuwa vinakwenda sambamba na mafundisho ya Uislamu. Hivyo, vikiwa na
picha zenye kuonyesha mume na mke wakiwa uchi katika kufafanua au
kueleza vitakuwa havifai kabisa. Au katika maelezo yake ikiwa vitakwenda
kinyume na mafundisho ya Kiislamu pia vitakuwa havifai.
Ama vitabu vilivyoandikwa
na wanachuoni kwa kufuatana na maagizo ya Qur-aan na Sunnah hivyo
ndivyo vinavyohitajiwa kusomwa ili tupate muongozo sahihi wa wana ndoa
kufanya tendo la ndoa kwa njia zilizo sahihi. Ni muhimu kwa sababu
aghlabu wana ndoa wa Kiislamu huwa hawapati mafunzo hayo kiuwazi na
wengi wanaona aibu kuuliza, kisha wanaishia kujinyima haki zao katika
tendo la ndoa na huenda wakaingiwa na shauku ya kutafuta njia nyingine
za kupata mafunzo hayo ambazo sio halali kama kutazama sinema za ngono
n.k. Lakini watakapopata vitabu vyetu vya Kiislamu watapata mafunzo
sahihi na khaswa yanayotokana na mafunzo ya dini yetu.
Tutambue
kuwa dini yetu haifichi haki, na hakuna aibu kuelezea mambo ya ndani ya
ndoa yaliyo haki ili mafunzo hayo yawekwe wazi kwa Waislamu watambue
yanayowapasa kutenda kihalali hata waweze kujitosheleza na starehe za
kitendo cha ndoa, waweze kuimarisha ndoa zao na kujiepusha na vishawishi
vya haramu.
Kwa hakika vitabu hivi viko vingi katika lugha ya Kiarabu na kwa Kiswahili vimeanzwa kuandikwa kama kwa mfano Furaha ya Ndoa na Siri ya Unyumba na pia Zawadi kwa Wanandoa ambacho tayari kiko katika hii tovuti yenu kwenye kitengo cha vitabu, ingia hapa ukisome: ZAWADI KWA WANANDOA. Na chengine ambacho kimetafsiriwa ni Malezi ya Kijinsiya lakini bado kuchapishwa.
Na Allah Anajua zaidi
Hadithi Ya 01: Kila Kitendo Kwa Nia Yake
الحديث الأول
" إنما الأعمال بالنيات "
عن
أَمِيرِ المُؤمِنِينَ أَبي حَفْصٍ عُمَرَ بنِ الخطَّابِ رَضِيَ اللهُ
عَنْهُ قَالَ : سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ:
((إِنَّما الأَعْمَالُ بالنِّيَّاتِ وإنَّما لكُلِّ امْرِىءٍ ما نَوَى،
فَمَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ فَهِجْرَتُهُ إلى اللهِ
ورَسُولِهِ، ومَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ لِدُنْيا يُصِيبُها أو امْرأةٍ
يَنْكِحُها فَهِجْرَتُهُ إلى ما هَاجَرَ إليه)).
رَوَاهُ
إِمَامَا الْمُحَدِّثِينَ أَبُو عَبْدِ اللهِ مُحَمَّدُ بنُ إِسْمَاعِيل
بن إِبْرَاهِيم بن الْمُغِيرَة بن بَرْدِزبَه الْبُخَارِيُّ وَأَبُو
الْحُسَيْنِ مُسْلِمٌ بنُ الْحَجَّاج بن مُسْلِم الْقُشَيْرِيُّ
النَّيْسَابُورِيُّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا فِي "صَحِيحَيْهِمَا" اللذينِ
هُمَا أَصَحُّ الْكُتُبِ الْمُصَنَّفَةِ.
HADITHI YA 1
KILA KITENDO KWA NIA YAKE
Kutoka kwa Amiri wa Waumuni, Abu Hafs 'Umar Ibn Al Khattaab رضى الله عنه ambaye alisema : Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu صلى الله
عليه وسلم akisema:
Vitendo
vinategemea (vinalipwa kwa) nia na kila mtu atapata kwa mujibu wa kile
alichokusudia. Kwa hivyo yule aliyehama kwa ajili ya Allaah na Mtume
wake, uhamaji wake ni kwa ajili ya Allaah na Mtume wake, na yule ambae
uhamaji wake ulikuwa ni kwa ajili ya manufaa ya kidunia au kwa ajili ya
kumuoa mwanamke (Fulani) uhamaji wake ulikuwa kwa kile kilichomuhamisha.
Imesimuliwa
na Maimam wawili mabingwa wa hadithi Abu Abdalla Muhammad Ibn Ismail
Ibn Ibrahim Ibn Mughiyra Ibn Bardizbah Al Bukhari na Abu Al Husayn
Muslim Ibn Al-Hajjaj Ibn Muslim Al Qushayri An-Naysaburi, katika sahihi
zao mbili ambavyo ni vitabu vya kutegemewa. Maana Ya Hadiyth Dhwa'iyf
Maulamaa
wanasema kuwa: Hadiyth dhaifu ni ile isiyokuwa na sifa zinazokubalika.
Na wengine wakasema kuwa Hadiyth dhaifu ni ile isiyostahiki kuitwa
Sahihi wala Hasan (njema).
Zipo aina nyingi ya Hadiyth dhaifu zikiwemo:
Mursal:
Nazo ni zile zilizonyanyuliwa moja kwa moja kutoka kwa Taabi'iy mpaka kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم.
Taabi'iy ni Muislamu aliyeishi wakati wa Maswahaba رضي الله عنهم akawaona lakini hajamuona Mtume صلى الله عليه وآله وسلم.
Kwa mfano Tabi'iy aseme:
“Mtume wa Mwenyezi Mungu صلى الله عليه وآله وسلم amesema…”
Wakati yeye hajawahi kuonana na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم.
Maulamaa wamekhitalifiana juu ya kuzitumia Hadiyth za aina hii katika makundi manne:
1. Imaam Abu Haniyfah na Imaam Maalik na baadhi ya wanavyuoni wanasema kuwa Hadiyth hizi zinafaa kutumika.
2. Imaam An-Nawawiy akieleza juu ya Jamhuur kubwa ya Maulamaa na pia akimnukuu Imaam Ash-Shaafi'iy anasema kuwa Hadiyth za aina hii zinaweza kutumika kama ni hoja lakini si hoja ya moja kwa moja (ya kutegemewa).
3. Imaam Muslim anasema: “Hadiyth Mursal kwetu sisi na kwa wengi kati ya wanavyuoni si hoja hata kidogo.”
4. Wengine wakasema kuwa inaweza kuwa hoja pale tu ikiwa imepokelewa kutoka kwa Tabi'iy mkubwa, kisha Hadiyth hiyo iwe imefanyiwa kazi na Swahaba yeyote au na wanavyuoni wengi.
Munqatwi'i:
Hizi ni zile Hadiyth zilizokatika Isnadi zake, yote sawa kukatika huko kuwe mwanzo au mwisho wa majina ya wapokezi
Al-Mudallas:
Nazo
ni zile Hadiyth ambazo muelezaji aeleze kuwa amehadithiwa na mtu
aliyeishi katika zama moja kisha ikathibiti kuwa hawajapata kuonana. Au
ahadithie kama kwamba amehadithiwa na mtu huyo wakati ukweli ni kuwa hakuhadithiwa na mtu huyo, kwa mfano aseme:
“Amenihadithia fulani.” Au: “Nilimsikia fulani.” Wakati ingekuwa sahihi kama angesema:
“Amesema fulani.” Au: “Kutoka kwa fulani.”
Maulamaa wanasema kuwa Mudallis (muelezaji wa Hadiyth hizi) hazikubaliwi riwaya zake hata kama aliwahi mara moja tu katika maisha yake kusema uongo katika Hadiyth.
Wengine akiwemo Imaam Ash-Shaafi'iy wakasema kuwa: “Ni zile Hadiyth alizodallis tu hazikubaliki, lakini zile alizozielezea kwa njia sahihi zinakubalika.”
Mudhwtwarib:
Nazo ni zile Hadiyth nyingi zinazogongana. Hadiyth aina hii zimedhoofishwa kwa sababu ya kugongana kwake na kutokuwa thaabit.
Munkar:
Nazo ni zile zilizohadithiwa na ‘Dhaifu’ (mtu asiyeaminika) kisha zikakhitilafiana na Hadiyth zilizohadithiwa na Thiqah (mtu mwenye kuaminika).
Al-Mudhwa'af:
Nazo ni zile Hadiyth zilizodhoofishwa na baadhi ya Maulamaa kutokana na udhaifu wa wapokezi wake, wakati baadhi nyingine ya Maulamaa wakasema kuwa ni sahihi.
Al-Matruuk:
Nazo
ni zile zilizohadithiwa na mtu anayetuhumiwa kwa uongo katika Hadiyth
au hata katika mazungumzo yake. Au anayetuhumiwa kuwa ni Faasiq wa
maneno au vitendo. Matruuk pia ni yule mwenye kusahau sana au mwenye kukosea sana.
Wakati Gani Hadiyth Dhaifu Inakuwa Na Nguvu?
Hadiyth
dhaifu inapata nguvu pale tu ikiwa rawi wake (mwenye kuhadithia)
anatuhumiwa kuwa ameanza kusahau sahau. Ni Sharti awe Thiqah hatuhumiwi
kwa Uongo wala kwa Ufaasiq wala kwa kusahau sana. Kisha Hadiyth alozungumza juu yake ziwe zimepokelewa kwa njia nyingi sana, na hapo inapanda darja na kuwa ‘Hadiyth Hasan.’
Na
hii ni kwa sababu imepokelewa kwa njia zinazokubalika tena kwa njia ya
rawi asiyetuhumiwa kwa uongo au kwa sababu ovu za kumdhoofisha.
Kuzifanyia Kazi Hadiyth Dhaifu:
Maulamaa wamekhitalifiana katika hukumu za kuzifanyia kazi Hadiyth za aina hii katika makundi matatu:
1. Wapo
wanaosema kuwa Hadiyth hizi hazifai kuzifanyia kazi kabisa, yote sawa
iwe katika kuamrisha mambo ya Fadhila au katika Hukmu. Na hii ni kauli
ya Yahya bin Ma'iyn na Abu Bakr bin Al-'Arabiy na pia Al-Bukhaariy na Muslim.
2. Wengine wakasema kuwa Hadiyth hizi zinaweza kufanyiwa kazi.
3. Na
wengine wakasema kuwa Hadiyth hizi zinaweza kufanyiwa kazi katika mambo
ya Fadhila na katika kuwaidh watu tu. Na kwamba zisitumike katika kutoa
hukmu au katika ibada, tena ziwe zimekamilisha baadhi ya masharti kama
vile asituhumiwe mmojawapo wa wapokezi wake kwa uongo au ufasiki n.k. Na
pia udhaifu wa Hadiyth usiwe mkubwa sana, na pia mtu anapoelezea Hadiyth ya aina hii awajulishe watu kuwa ina udhaifu ndani yake.
Anasema Dr. Muhammad Al-‘Ajjaaj Al Khatwiyb katika kitabu chake ‘Al-Mukhtaswar Al-Wajiyz fiy 'Uluum al-Hadiyth:
“Mimi
naunga mkono rai ya mwanzo inayosema kuwa Hadiyth dhaifu zisifanyiwe
kazi kabisa. Zipo Hadiyth za kutosha zilizo sahihi katika mambo ya
fadhail na mawaidha kiasi ambapo haina haja ya kuingiza Hadiyth zenye
shaka zinazoweza kuwa ni maneno ya uongo aliyozuliwa Mtume wa Mwenyezi
Mungu صلى الله عليه وآله وسلم.”
Pia Fadhail na Tabia njema ni katika mambo muhimu sana katika dini kwa hivyo haina haja kuzitumia Hadiyth dhaifu kwa ajili yake.”
Rai ya Dr. Muhammad Al-‘Ajjaaj ni bora zaidi kwa sababu mtu atawezaje kuiamini Hadiyth iliyosimuliwa
na Mudallis, mtu mwenye kubadilisha majina ya Mashaykh au ya miji
akijua kuwa anawadanganya wasikilizaji wake, au muongo ‘Kadhaab’
anayependa kuwadanganya watu katika mambo ya kidunia ambaye hatoshindwa
kuwadanganya katika mambo ya dini.
Na vipi mtu ataweza kuifanyia kazi Hadiyth Mudhtwarib inayogongana na Hadiyth Swahiyh au Hadiyth Matruuk iliyodhoofishwa kwa ajili ya tabia ovu za msimulizi kwa ajili ya uongo na ufasiki n.k.
Na Allah Anajua zaidi
Friday, December 6, 2013
Dunia Imejaa Ghururi
Dunia Imejaa Ghururi
Naaswir Haamid
Hakika
dunia imejaa ghururi, basi yasikudanganyeni maisha ya dunia wala
asikudanganyeni yule mdanganyi mkubwa (Ibilisi) katika (mambo ya)
Mwenyezi Mungu. Dunia itupeni mbali kama vile Mwenyezi Mungu Alivyotutaka na itafuteni akhera yenu, kwani Mwenyezi Mungu Ameipigia mfano dunia[1].
"Na wapigie mfano wa maisha ya dunia ni kama
maji tunayoyateremsha kutoka mawinguni; kisha huchanganyika nayo mimea
ya ardhi kisha ikawa majani makavu yaliyokatikakatika ambayo upepo
huyarusha huku na huko. Na Mwenyezi Mungu Ana uweza juu ya kila kitu.
"Mali
na watoto ni pambo la maisha ya dunia. Na vitendo vizuri vibakiavyo
ndivyo bora mbele ya Mola wako kwa malipo na tumaini bora (kuliko hayo mali na watoto)". Al Kahf - 45 – 46
Nakuusieni
waja wa Allaah kumuogopa Allaah, kwani Taqwa ni jambo bora la
kunasihiana baina ya waja wa Allaah, na ndiyo amali Anayoridhika nayo
Mwenyezi Mungu kutoka kwa waja wake.
Mumeamrishwa
kumcha Mungu na kwa ajili ya wema mumeumbwa, kwa hivyo ogopeni yale
Allaah Aliyokutahadharisheni nayo, kwa sababu Amekutahadharisheni na
adhabu kali kabisa.
Muogopeni
Mwenyezi Mungu kuogopa kwa kweli na tendeni matendo yenu bila ya
kujionesha kwa watu wala kutaka sifa au umaarufu, kwani mwenye kufanya
amali yoyote ile kwa ajili ya kujipendekeza kwa mwengine asiyekuwa
Allaah, basi Mwenyezi Mungu Humsukumiza nazo amali zake kwa huyo
aliyemfanyia amali hiyo.
Ogopeni
adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu Hajakuumbeni kwa upuuzi, na wala
Hakuacha chochote kiende ovyo. Keshataja athari zenu na Keshajua siri
zenu na kuzihesabu amali zenu na kuziandika ajali zenu. Kwa hivyo dunia
isikubabaisheni kwani inawaghururisha watu wake, na ameghurika yule
atakayebabaishwa nayo.
Kwa Nini Wanaume Wamepewa Cheo/Fadhila/Mamlaka Zaidi Kuliko Wanawake? Wanawake
Kwa Nini Wanaume Wamepewa Cheo/Fadhila/Mamlaka Zaidi Kuliko Wanawake?
Wanawake
SWALI:
Assalamu alayum warahmatu llahi taala wabarakatu. Naomba kuuliza maSWALI: ambayo yananiumiza kichwa changu na kila ninaemuuliza naona sijafaidika bado na majibu ninayoyapata. Kwa nini mwanamme ana cheo kikubwa kuliko mwanamke katika uislam wakati mwanamke ana kazi kubwa kuliko mwanamme? Mwanamke anazaa, anashughulikia nyumba na watoto, anamshughulikia mume kama mtoto mchanga, mwanamke ni mtu mwenye kazi masaa ishirini na nne hapumziki, mwanamme kazi anayoifanya ni kutafuta kijio. Lakini tunaambiwa kwamba kama kuna kusujudu baada ya M Mungu tungeambiwa tusujudie waume zetu, na mirathi wao wamepewa mingi kuliko wanawake, lazima ukitoka uage wao si lazima, wao wamepewa uwezo wa kuoa mke mwengine, wamepewa uwezo wa kutoa talaka, na mambo mengi ambayo mwanamke hakupewa, swali langu liko hapo.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mwanamme kupewa cheo zaidi kuliko mwanamke.
Hakika hili ni suala ambalo linaonekana hivyo na watu hasa kwa ajili ya kasumba ambazo zinatiwa na wasiokuwa Waislamu wasiouelewa Uislamu na haki inayompatia kila mmoja.
Awali ya yote inatakiwa tufahamu kuwa aliyempatia haki kila mmoja wetu ni Allaah Mtukufu ambaye Anamjua kila mmoja wetu na kila analostahiki. Hakika ukichambua haki zilizoko kwa kila mmoja wetu utakuta kuwa mwanamke amepatiwa haki zaidi na Uislamu kuliko mwanamme. Tutajaribu katika jibu letu kuangazia yote yaliyoulizwa na ndugu yetu.
Kabla ya kuendelea na kuangazia haki na wajibu wa mwanamke na fadhila zake, tuangalie mwanamke alivyokuwa akifanywa kabla ya kukamilishwa Uislamu kwa kuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa mfano:
1. Katika Bara Arabu mwanamke alikuwa hana hadhi, akiuliwa pindi anapozaliwa (an-Nahl [16]: 58 – 59), kurithiwa na hata watoto wake wa kambo pindi alipokuwa mumewe, kunyimwa urithi kabisa na mengineo mengi.
2. Mwanamke katika ustaarabu wa Kigiriki alikuwa ni chombo cha kuondolea matamanio ya kiwiliwili cha mwanamme; hivyo alikuwa akiuzwa kama machungwa sokoni. Socrates alisema: “Mwanamke ni chanzo cha machafuko yote duniani, yeye ni kama mti wa dafali ambao sura ya nje ni ya kuvutia mno lakini iwapo ndege ataula basi ni wazi atakufa”
.
3. Ama mwanamke katika Ukristo hana thamani kabisa. Kulingana na Biblia, mwanamke hana utukufu kwa sababu ameumbwa kwa ajili ya mwanamme (1 Wakorintho 11: 7 – 10). Vile vile yeye ni najisi (Ayubu 14: 1 – 4), ndiye asili ya dhambi (Mwanzo 3: 12) na kadhalika.
4. Mwanamke katika Ubaniyani alikuwa akichomwa hadi kufa na mumewe iwapo mume atakufa kabla yake na kutokuwa na uhuru kabisa wa aina yoyote.
5. Mwanamke wa Kirumi alikuwa ni pambo kwa mwanamme na kwa kuwafurahisha wafalme alikuwa anaimbishwa akiwa uchi. Na tabia hii ya kishenzi imebakia hadi leo.
6. Mwanamke wa Kichina alikuwa hana haki yoyote katika jamii, na mumewe alikuwa ana haki ya kuuza mwili wa mkewe kwa wanaume wengine. Naye alirithiwa kama mali na jamaa za mumewe pindi anapoaga dunia.
7. Ama mwanamke wa kisasa katika tamaduni mbali mbali amekuwa ni chombo cha kuridhisha wanaume kwa njia moja au nyingine. Hakuna bidhaa yoyote inayouzwa bila kuonyesha mwanamke kwenye matangazo.
Tukija katika Uislamu Allaah Aliyetukuka Amempatia kila mmoja kati ya mwanamme na mwanamke majukumu, haki na wajibu wake kulingana na maumbile yake. Hata hivyo, mwanamme amepatiwa daraja ya juu kuliko mwanamke. Anasema Aliyetukuka:
“Wanaume ni walinzi wa wanawake; kwa sababu Allaah Amewafadhilisha baadhi yao kuliko wengine, na kwa sababu ya mali zao wanazozitoa” (an-Nisaa’ [4]: 34).
Ama majukumu yao yanakuwa ni wenye kusaidiana ili kuleta mabadilko mazuri katika jamii. Utapata kwa suala lingine mwanamke yuko juu ya mwanamme na kwa jambo jingine ni mwanamme mwenye jukumu kubwa zaidi.
Uislamu umetangaza kabisa kuwa asili ya mwanamke na mwanamme ni moja:
“Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi (asili) moja. Na Akamuumba mkewe kutoka katika nafsi ile ile. Na Akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi” (an-Nisaa’ [4]: 1).
Na Mtume (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:
“Hakika wanawake ni ndugu wa wanaume” (Abu Daawuud na at-Tirmidhiy).
Ama katika Uislamu hakuna kosa la asili ambalo analaumiwa mwanamke bali wote wanalaumiwa kwa kushawishiwa na Shaytwaan:
“Lakini Shaytwaan aliwatelezesha wote wawili na akawatoa katika hali waliyokuwa nayo” (al-Baqarah [2]: 36).
Na pia:
“Wakasema: Mola wetu! Tumedhulumu nafsi zetu, na kama Hutatusamehe, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye hasara” (al-A‘raaf [7]: 23).
Hivyo, wote walikosa na wakasamehewa, kwa hiyo kutokuwa na makosa baada ya hapo.
Mwanamme na mwanamke wapo sawa katika malipo lau mmoja wao atatenda mema. Anasema Aliyetukuka:
“Na mwenye kutenda mema akiwa mwanamme au mwanamke naye ni Muumini, basi hao wataingia Peponi wakiruzukiwa bila hesabu” (al-Ghaafir [40]: 40).
Na pia,
“Hakika Mimi sipotezi juhudi ya mfanya juhudi miongoni mwenu akiwa mwanamme au mwanamke” (aal-‘Imraan [3]: 195).
Pia waweza kutazama kuhusu haya katika Suratun Nahl: 97 na pia Suratul Ahzaab: 35.
Na mwenye kufanya uhalifu ima wa kuiba au kuzini, akiwa mwanamke au mwanamme atapata adhabu hiyo hiyo. Tazama adhabu ya wizi katika Suratul al-Maa’idah: 38 na uzinzi katika Suratun Nuur: 2.
Pia Uislamu umempatia kila mmoja wao usawa wa kiuchumi na kumiliki mali, kufanya biashara baina ya jinsia hizo mbili. Allaah Aliyetukuka Anasema:
“Na wala msitamani vile ambavyo Allaah Amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wanayo sehemu (haki kamili) ya walivyo vichuma na wanawake pia wanayo sehemu (haki kamili) ya vile walivyo vichuma” (an-Nasaa’ [4]: 32).
Na kwa ajili hii tunaona vipi wanawake katika enzi tofauti waliweza kuusaidia Uislamu na Waislamu kwa pesa zao, mfano mmoja ni Mama wa Waumini Khadijah (Radhiya Allaahu ‘anha).
Mwanamke naye ana haki sawa katika kurithi kile ambacho kimeachwa na jamaa wa karibu. Kwa hilo, Allaah Aliyetukuka Anasema: “Wanaume wana sehemu katika mali wanayoacha wazazi na jamaa wakaribu. Na wanawake pia wana sehemu katika yale waliyoacha wazazi na jamaa wa karibu” (an-Nisaa’ [4]: 7).
Hata hivyo, Uislamu umempatia mwanamme sehemu mbili kwa moja anayopata mwanamke. Huenda hilo likaonekana ni dhuluma kwa mwanamke, lakini tukiona hekima kwa mgao huo tunaweza kugundua kuwa pengine mwanamme amepata sehemu ndogo zaidi kwa mgao huo. Kwa muhtasari mwanamme amepatiwa sehemu kubwa zaidi katika urithi kuliko mwanamke katika shari’ah ya Kiislamu. Na hiyo ni kwa sababu zifuatazo:
1. Mwanamme amelazimishwa kutoa mahitaji kwa mkewe, wanawe, jamaa zake wa karibu, tofauti na mwanamke ambaye hakukalifishwa kishari’ah kutoa mahitaji yoyote. Kwa hiyo, mali anayopata mwanamme inatumika kwa watu wengi ilhali ya mkewe itakuwa ni yake anaweza kuweka akiba, wala hatolazimika kutoa senti moja katika mali aliyorithi kwa ajili ya watu wengine.
2. Mwanamme anawajibika kutoa mahari kumpa mwanamke wakati akioa ilhali mwanamke yeye hatoi mahari bali ndiye anayepatiwa mahari tena anayotaka yeye.
3. Wajibu wa kuwaelimisha watoto, kuwatibu wenye kumtegemea na kuwatunza ni wa mume. Kwa hivyo, urithi wake wote utatumika kwa mambo kama hayo, ilhali urithi wa mwanamke ni wake naye hana wajibu kama huo.
Labda tuchukue mfano wa mzazi aliyekufa akaacha mvulana na msichana na akiwa amebakisha 30,000. Kwa mgao wa Kiislamu ikiwa hakuna mrithi mwengine, mvulana atapata 20,000 na msichana 10,000. Na endapo wote wawili wamefikisha umri wa kuoa na kuolewa, na kila mmoja atalipa au kulipwa elfu kumi (10,000). Kwa minajili hiyo, mvulana atatoa 10,000 na kubakisha 10,000, ilhali msichana akipata 10,000 atakuwa na pesa taslimu 20,000. Hizi pesa za msichana ni zake na anaweza kuzitumia kwa njia yoyote atakayo ilhali mvulana pesa alizobaki nazo itabidi azitumie kumtazama mkewe na watoto atakaporuzukiwa. Msichana hata akizaa jukumu la kumtazama yeye pamoja na mtoto/ watoto ni la mumewe. Na lau ikitokea sinto fahamu (su-u tafaahum) baina ya mume na mkewe, na kutokea talaka msichana huyo atarudi kwa kaka yake na ni jukumu la kaka kumtazama katika hali zote zile.
Pia Uislamu umeweka nidhamu kuwa wazazi wanatakiwa wawalee watoto wote bila ya kuwabagua kati yao kulingana na jinsia zao. Allaah Aliyetukuka Anatuambia:
“Enyi Mlioamini! Jiokoeni nafsi na jamaa zenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe” (at-Tahriym [66]: 6).
Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye watoto wa kike watatu au dada watatu au watoto wa kike wawili au dada wawili akawalea vyema na akamcha Allaah kwa ajili yao basi atapata Pepo” (at-Tirmidhiy).
Na hivyo, hapa tunapata msisitizo wa umuhimu wa kuwalea watoto wa kike kwa wema na njia nzuri.
Uislamu umempatia haki mwanamke kwa kumuelimisha sawa na mwanamme na umesisitiza sana kupewa elimu wanawake tangu awali ya risala yake kupitia kwa Mtume wa mwisho (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Allaah Aliyetukuka Ametujulisha kwamba wenye kumuogopa yeye kikweli ni watu wenye elimu bila kubagua jinsia,
“Na kwa hakika wanaomuogopa Allaah katika viumbe Vyake ni wenye elimu” (al-Faatwir [35]: 28).
Pia jinsia zote mbili zina jukumu la kuamrisha mema na kukataza maovu. Hiyo ni kama Alivyosema Aliyetukuka:
“Na Waumini wanaume na Waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao. Huamrisha yaliyo mema na kuyakataza maovu” (at-Tawbah [9]: 71).
Inatakiwa tufahamu kuwa kila mmoja – kati ya mwanamme na mwanamke ni mchungaji na ana jukumu kila mmoja katika Nyanja yake katika maisha. Mume na mke wanatakiwa wasaidiane katika kutengeneza jamii kwa njia iliyo nzuri zaidi.
Yapo majukumu mengine ambayo yanampasa mwanamme peke yake, miongoni mwayo ni kuitazama nyumba yake na pia kuipigania Dini ya Allaah Aliyetukuka. Mwanamke hapaswi kuitazama nyumba ila tu anapotaka kumsaidia mumewe na hiyo itakuwa ni ihsani kwa upande wake. Ama Jihadi wanawake, hawana uwajibu wa kutekeleza hilo. Na kwa ajili ya kutazama nyumba zao, wakati mmoja wanawake walimtuma msemaji wao, Asmaa’ bint Yaziyd as-Sakan (Radhiya Allaahu ‘anha) alikuwa kwa Mtume (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa yupo pamoja na Maswahaba zake, ambaye alisema: “Ewe Mtume wa Allaah! Umetumwa kwa wanawake na wanaume, nasi tumekuamini. Hata hivyo, wanaume wanapata fadhila zote kwani wao wanahudhuria Swalah pamoja nawe, wanapata kujifunza kwako na wanapigana katika njia ya Allaah ilhali sisi twawatazama watoto wao wakiwa hapo. Je, nasi tutapata nini?” Akasema: “Kukaa kwenu nyumbani mnashirikiana nao katika thawabu”.
Uislamu umetambua kazi kubwa ya mwanamke, hasa katika kubeba mimba, kuzaa na kumlea mtoto na kwa ajili hiyo, Allaah Aliyetukuka Anasema:
“Na Tumemuusia mwanaadamu wazazi wake – mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumnyonyesha na kumuachisha kunyonyesha katika miaka miwili – ya kwamba Unishukuru Mimi na wazazi wako” (Luqmaan [31]: 14).
Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa: “Ni nani aliye na haki wa usuhuba wangu?” Akasema: “Mama”. Kisha nani? Akasema: Mama. Kisha nani? Akasema: Mama. Kisha nani? Akasema: Baba” (al-Bukhaariy na Muslim).
Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametoa dhamana kwa mwanamke ambaye ataswali Swalah zake tano, kufunga mwezi wa Ramadhaan na kumtii mumewe kuwa ataingia Peponi kwa mlango wowote atakao.
Ama kuhusu talaka ameachiwa mume kwa sababu yeye ni mvumilivu zaidi na anaweza kuzuia hasira zake kwa wakati ambao alikuwa afanye jambo ambalo litaleta hasara katika jamii. Mara nyingi mwanamke hisia zake zinakwenda na yale mabadiliko ambayo anakabiliana nayo katika maisha yake na mwilini mwake mabadiliko ambayo mwanamme hana kwa kiasi cha mwanamke. Mwanamke ni mwepesi wa kuchukua hatua za haraka kisha kujuta baadaye mbali kabisa na mwanamme. Bila shaka, mwanamke pia amepatiwa aina mbili za talaka – Khul’ (kujitoa na kujivua katika ndoa) na pia kupitia kwa Qaadhi ikiwa mume ana makosa.
Ukitazama katika haya tuliyoyaeleza utakuta kuwa mwanamke amepatiwa fadhila kubwa na Uislamu kwa yale majukumu wafanyao na kazi zao nzuri.
Tunatumai majibu haya yataondosha shaka shaka ulizokuwa nazo na ambazo zinachangiwa sana na makafiri na wale Waislamu haswa wanawake wanaodai kupigania haki za wanawake wanaotumiwa na makafiri.
Na Allaah Anajua zaidi

MASWALI NA MAJIBU KWA MUJIBU WA QUR'AN NA SUNNA
Hijaab Ya Sheria Inahusu Kufunika Uso Na Miguu?
Wanawake
SWALI:
Naomba nifahamishwe hijabu ipasavyokuwa, je uchi wa wa mwanamke does it include miguu?since summer is nearing most of us are shoping for open shoes, is it allowed, I know other madh-habs say we should infact cover our whole faces but I don’t think the qur'an specifies that in particular?.
JIBU:
Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kuhusu kufunika Miguu:
Naam miguu ya mwanamke inalazimu kufunikwa. Imepokewa kutoka kwa Ummu Salamah amesema: nilimuuliza Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati lilipozungumzwa suala la kipimo cha nguo ya chini ya mwanamume (ambayo inatakiwa isivuke mafundo ya miguu), ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na ipi hukumu ya kipimo cha nguo ya mwanamke? Akasema: "Ataiteremsha (kiasi cha) shubiri) akasema Ummu Salamah kwa maana hiyo si itaonekana (miguu yake)? Akasema: (Na aiteremshe) kiasi cha dhiraa moja wala asizidishe zaidi ya hapo" (Abuu Dawuud: 4117 na Maalik katika Muwatwa: 2017).
Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyah (Rahimahu Allaah) amesema katika Majmuul-Fataawa 22/110:
“…….inavyoonyesha kuwa rai ya Imaam Ahmad ni dhahiri kabisa kuwa kila kiungo cha mwanamke ni ‘awrah’ (uchi) hata pia kucha zake. Na hii pia ni rai ya Imaam Maalik”
Dalili ni kutoka katika Aayah ifuatayo:
((وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ))
((Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo waliyoyaficha)) [An-Nuur: 23:31]
Imaam Ahmad amesema: “…. Mapambo ambayo yaliyodhihirika ni nguo ….. kila kiungo cha mwanamke ni ‘awrah’ hata kucha zake. Imesimuliwa katika Hadiyth “Mwanamke ni ‘Awrah”. Hii ni umbo lote la mwanamke. Na sio makruuh (haichukizi) kufunika mikono yake wakati wa kuswali, kwa hiyo pia ni sehemu ya ‘awrah kama ilivyo miguu. Hivyo Qiyaas (Analogy) imekusudiwa kwamba uso pia ni ‘awrah’ japokuwa haukutakiwa kufunikwa wakati wa Swalah na sio kama mikono…” [Sharh al-‘Umdah 4/267-268]
Dalili anayoichukulia Imaam Ahmad ni hii:
Imesimuliwa na ‘Abdullaah kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye amesema: ((Mwanamke ni ‘awrah’ na anapotoka nje basi matumaini ya shaytwaan huwa juu)) [At-Tirmidhiy, 1173 na Shaykh Al-Albaaniy kasema Swahiyh katika At-Tirmidhiy 935.]
Kuhusu kufunika uso:
Maulamaa wamekhtilafiana kuhusu mas-ala haya. Maelezo kamili utayapata katika Jibu la Swali kwenye kiungo kifuatacho ambalo limeshaulizwa Alhidaaya:
JE, INAFAA MUME KUMLAZIMISHA MKE KUVAA NIQAAB?
Mwanamke wa Kiislamu analazimika kuyafahamu masharti ya hijabu yanavyopasa kuwa, nayo ni haya yafuatayo:
1. Inatakiwa hijabu ikisitiri kiwiliwili chote cha mwanamke, (pamoja na khilafu iliyopo kati ya wanachuoni kuhusu suala la uwajibu wa kuufunika uso na kutoufunika);
2. Jilbaab la mwanamke lisiwe na mapambo.
3. Kitambaa cha jilbaab kinatakiwa kiwe kizito (kisioneshe vazi la ndani);
4. Jilbaab linatakiwe liwe pana (isibane);
5. Jilbab halitakiwi kutiwa manukato;
6. Jilbaab halitakiwi lifanane na mavazi ya kiume;
7. Jilbaab halitakiwi lifanane na mavazi ya makafiri;
8. Jilbaab halitakiwi liwe ni katika mavazi ya fakhari.

mashahiri mazuri
Muumba Mwenye viapo kila aina,
Anatuhakikishia kuwa ipo Siku itasimama,
Wakati ukiwadia wa kuisagasaga milima,
Mwezi na nyota zitakapokunjana,
Ole wao siku hiyo hao wanaokana.
Aliyetolewa tumboni atamkimbia wake mama,
Aliyebeba mashaka tisa miezi atamuacha mwana,
Rafiki na wapenzi walio karibu watafarikiana,
Ndugu kwa ndugu watakaribia kupigana,
Ole wao siku hiyo hao wanaokana.
Sauti ya Mwingi wa Rehema Itakaponguruma,
Makafiri na wanafiki nyoyo zao hazitatuwama,
Waliokadhibisha kwao haipo katu salama,
Vilio vyao havitawaweka sehemu njema,
Ole wao siku hiyo hao wanaokana.
Umri uliopotezwa hautarudi nyuma,
Kwa nguvu watajaribu meno kuyabana,
Wakijuta kujishughulisha zaidi na ngoma,
Mipira na starehe zisizokuwa na maana,
Ole wao siku hiyo hao wanaokana.
Wale waliokadhibisha Zake nyingi neema,
Wakafanya usengenyaji kuwa amali ya kuchuma,
Wakati ukawapita Akhera hawakuitizama,
Wataburuzwa ndani ya moto hutwama,
Ole wao siku hiyo hao wanaokana.
Waliokadhibisha neema watashuhudia Qiyaama,
Wataingizwa katika moto ulio mrefu na mpana,
Usio kuwa na kizuri chakula wala huruma,
Adhabu zitapanda daraja kwa kufuatana,
Ole wao siku hiyo hao wanaokana.
Watiifu kwa Mola waliotumia vyema zama,
Wataingizwa Peponi nyoyo zipate salama,
Amani na utulivu utokao kwa Karima,
Utawapatia faraja na furaha daima,
Ole wao siku hiyo hao wanaokana.
Waliomcha Mungu watalipwa mema,
Watakula na kustarehe wapendavyo namna,
Watakuwa na maisha yasiyo koma,
Ni malipo yatokayo kwa mwingi wa Rehema,
Ole wao siku hiyo hao wanaokana.
Ewe Muislamu haujafika wakati bayana?
Wa kujiweka mbali na sifa za anayekana?
Ukatenda mazuri na yaliyo mema?
Je unataka kulipwa mfano wa huyo anayekana?
Hadithi Ya 17: Mola Kaandika Uzuri (wema) Katika Kila Kitu
Hadithi Ya 17: Mola Kaandika Uzuri (wema) Katika Kila Kitu
الحديث السابع عشر
"إن الله كتب الإحسان على كل شيء"
عن أبي يَعْلَى شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ رضي اللهُ عنه، عن رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال: ((إنَّ اللهَ كَتَبَ الإِحْسانَ على كلِّ شَيءٍ، فإذا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا الْقِتْلَةَ، وَإذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذِّبْحَةَ، ولْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ ولْيُرِحْ ذَبيحَتَهُ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA 17
MOLA KAANDIKA UZURI (WEMA) KATIKA KILA KITU
Kutoka kwa Abu Ya’ala Shaddad Ibn Aws رضي الله عنه ambaye amesema: Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Mola kaamrisha wema katika kila kitu. Kwa hiyo unapoua (mnyama), ua vizuri na unapochinja chinja vizuri. Basi kila mmoja wenu anoe kisu chake barabara (anapotaka kuchinja) na amuondoshee machungu (asimtese) yule mnyama anayemchinja.
Imesimuliwa na Muslim

Thursday, December 5, 2013
022 - Hadiyth Ya 22: Kuhifadhi Undugu Wa Kiislamu, Haki, Heshima, Kutokufanyiana Uadui, Chuki Na Kudharauliana
عَنْ
أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّه (صلى الله
عليه و آله وسلم) ((لاَ تَحَاسَدُوا وَلاَ تَنَاجَشُوا وَلاَ تَبَاغَضُوا
وَلاَ تَدَابَرُوا ولاَ يَبِعْ بَعْضُكُمْ عَلَى بَيْعِ بَعْضٍ, وَكُونُوا
عِبَادَ اللَّهِ إِخْوَانًا. الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ لاَ يَظْلِمُهُ
وَلاَ يَخْذُلُهُ وَلاَ يكذبه ولاَ يَحْقِرُهُ. التَّقْوَى هَاهُنَا))
وَيُشِيرُ إِلَى صَدْرِهِ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ ((بِحَسْبِ امْرِئٍ مِنْ
الشَّرِّ أَنْ يَحْقِرَ أَخَاهُ الْمُسْلِمَ. كُلُّ الْمُسْلِمِ عَلَى
الْمُسْلِمِ حَرَامٌ دَمُهُ وَمَالُهُ وَعِرْضُهُ)) رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Msihusudiane,
wala msipandishiane bei [katika biashara pasina kuwa na haja ya
kununua], wala msibughudhiane, wala msikatane, wala msiingie katika
biashara waliyokwishaingia wenzenu, nyote kuweni ni waja wa Allaah ndugu
moja. Muislamu ni ndugu wa Muislamu, hamdhulumu, wala haachi
kumsaidia, wala hamdanganyi, wala hamdharau. Taqwa ipo hapa)) akaashiria kifuani mwake mara tatu. ((Yatosha kuwa shari mtu kumdharau nduguye Muislamu. Kila Muislamu juu ya Muislamu mwenziwe ni haramu damu yake, mali yake, na heshima yake)).[1]
Mafunzo Na Hidaaya:
- Uislamu unasisitiza kuchunga haki na heshima baina ya watu, na unatahadharisha kudharauliana. [Rejea Hadiyth namba 88, 89, 96 126].
يَا
أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَىٰ أَن
يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِّن نِّسَاءٍ عَسَىٰ أَن
يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ ۖ وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ ۖ بِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ ۚ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿١١﴾
Enyi
mlioamini! Watu (wanaume) wasiwadharau watu (wengineo, kwani) huenda
(waliodharauliwa) wakawa bora kuliko wao. Na wala wanawake
(wasiwadharau) wanawake (wengineo), huenda (waliodharauliwa) wakawa bora
kuliko wao. Na wala msikashifeni, na wala msiitane majina ya utani
(mabaya). Uovu ulioje wa jina la ufasiki baada ya iymaan. Na yeyote
asiyetubu, basi hao ndio madhalimu[2]
- Uislamu unakataza kuudhiana [Al-Ahzaab 33: 58] na kutendeana uadui bali kushirikiana kwa wema [Al-Maaidah 5: 2].
- Waislamu wote ni ndugu [Al-Hujuraat: 49: 10].
- Uhasidi, bughudha na chuki, ni miongoni mwa maradhi ya moyo yanayomhatarisha Muislamu siku ya Qiyaamah kufika mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) akiwa na moyo usiosalimika [Ash-Shu’araa 26: 88-89].
- Uislamu unasisitiza kuungana si kutengana au kukatana undugu [Muhammad 47: 22-23].
- Kuuana ni miongoni mwa madhambi makubwa, nayo yanahusiana na haki ya mtu [An-Nisaa: 92-93].
- Taqwa ipo moyoni, na inadhihirishwa kwa vitendo vyake, kukhofu kutenda uovu na kutenda mema.
- Muislamu anafaa achunge sana asije kuingia katika haramu kwa kuvunja heshima ya nduguye, kumwaga damu yake au kula mali yake.
- Hii ni Hadiyth ‘adhimu yenye kutufunza mahusiano mema na maingiliano mazuri baina ya Waislamu wao kwa wao na wanaadamu wote duniani.
Subscribe to:
Posts (Atom)
احمد محب الدين الأخبار جديد/احب الله ورسوله
حبّ الرسول صلّى الله عليه وسلّم
قال عليه والصلاة والسلام <<من أحبّ سنّتي فقد أحبّني ومن أحبني كان معي في الجنة>>وقال تعالى<<قل إن كنتم تحبّون الله فاتبعوني يحبب كم الله و يغفر ذنوبكم>>
Popular Posts
-
Hijaab Ya Sheria Inahusu Kufunika Uso Na Miguu? Wanawake SWALI: Naomba nifahamishwe hijabu ipasavyokuwa, je uchi wa wa mwanamke does ...
-
Mwanamume na mwanamke wanapofunga ndoa inawapasa wote watambue desturi, mwendo mwema na adabu katika maisha hayo ya mke na mume ili ndoa ya...
-
cave of as habul kahf/pango la as habul kahfi ndani yake Cave of Ashabe-Kahf (interior) The main view above shows a section of the int...
-
TIZAMA PICHA: Mtoto mdogo Gerezani, Wako wapi watetezi wa haki za Binaadam!? Uadui wa Serikali ya kibaraka ya Kenya dhidi ya waislamu ume...
-
WWW.FAHADAHM.BLOGSPOT.COM kuburi la bilal ibn rabaah(r,a) Hili ndio kaburi la sahaba ambae alikua ni mtu wa karibu mno na mtume (s,a,w)...
-
PADRI AFUMANIWA NA MKE WA MTU! STORY NA PICHA KAMILI HIZI HAPA - BongoClan™
-
KISAA CHA BILAL....MUADHINI WA MWANZO KATIKA UISLAMU. Bilaal Bin Rabaah (Radhiya Allaahu 'Anhu) ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu...
-
WACHUMBA KUZOEANA TABIA KABLA YA NDOA.. Hii ni ada na desturi ambayo inaishi na kuchukua nafasi katika baadhi ya familia katika jamii zetu....
-
www.fahadahm.blogspot.com This tomb is believed to be that of Shoayb (a.s.). He is regarded as being the father-in-law of Musa (a.s.) and...
-
"Ameen", your Ameen is powerful.!! Oh! Allah grant me a spouse who: will be the garment for my soul. who will satisfy half of my...