Ama baada ya
kumtukuza na kumshukuru Allah na pia kumtakia rehma na amani Mtume wetu.
Mwenyezi Mungu Ametuamrisha tuamini kwamba yeye yuko. Na Aya
zinazozungumzia suala hili ni nyingi sana pia ameumba viumbe
vinavyoonesha kwamba yeye yupo.Kwani kupatikana kwa viumbe ni kuonesha
kuna aliyeumba.
Enyi ndugu
katika imani ! Hakika katika kila kitu alivyoviumba Mwenyezi Mungu
(Subhaanahu wa Taala) ni dalili ya kuonesha kwamba yeye ni mmoja, na
ndiye anayestahiki kuabudiwa kwa haki kabisa na haifai kushirikishwa na
yoyote wala chochote.
Napenda nizitaje baadhi ya Aya ambazo zimetuamrisha kuzingatia katika ulimwengu.
قال تعالى : {أَوَلَمْ
يَنْظُرُوا فِي مَلَكُوتِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا خَلَقَ اللَّهُ
مِنْ شَيْءٍ وَأَنْ عَسَى أَنْ يَكُونَ قَدِ اقْتَرَبَ أَجَلُهُمْ
فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ} [الأعراف : 185].
Amesema Allah
(Subhaanahu wa Taala): {{ Je hawaangalii ufalme katika mbingu na ardhi
na alivyoumba Mwenyezi Mungu katika vitu, na huenda ikiwa umekaribia
muda wao wa kuondoka duniani kumalizika. Basi ni maneno gani baada ya
Qur’an watayamini}} [Al-Araaf : 185].
وقال : {أَفَلَمْ يَنْظُرُوا إِلَى السَّمَاءِ فَوْقَهُمْ كَيْفَ بَنَيْنَاهَا وَزَيَّنَّاهَا وَمَا لَهَا مِنْ فُرُوجٍ *الْأَرْضَ مَدَدْنَاهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنْبَتْنَا فِيهَا مِنْ كُلِّ زَوْجٍ بَهِيجٍ *تَبْصِرَةً وَذِكْرَى لِكُلِّ عَبْدٍ مُنِيبٍ } [ق : 6 – 8].
Amesema Allah
(Subhaanahu wa Taala): {{ Je hawaangalii mbingu juu yao vipi tuliijenga
na kuipamba na kuifanya kuwa haina nyufa. Na ardhi vipi tuliitandaza na
kuiweka vigingi (isitikisike) na tukaotesha katika ardhi hiyo kila mimea
mizuri hali ya kuwa ni kifumbua macho kwa kila mtu muelekevu}} [Qaaf : 6
- 8].
وقال : {أَفَلَا يَنْظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ * وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ * وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ * وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ } [الغاشية 17 – 20].
Amesema Allah
(Subhaanahu wa Taala): {{Je hamwangalii Ngamia vipi ameumbwa, na mbingu
vipi zimeinuliwa, na milima vipi imekitwa na ardhi vipi imetandikwa}]
[Al-Qaashiyah: 17- 20]. Hizi ni alama ambazo Mola anataka tuzingatie
kuumbwa kwake.
Napenda sasa
kutaja baadhi ya viumbe vingine vya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa
Taala). Navyo ni vinavyopatikana katika ardhi kama vile; Maji, Madini,
Majabali, Mimea aina tofauti tofauti, kwani Mwenyezi Mungu
ameidhalilisha ardhi hii kwa manufaa ya wanadamu na wanyama, wanadamu
wanailima kwenye ardhi na kupanda mimea ili kujipatia chakula chao,
wanatoa maji katika ardhi kwa matumizi yao na pia kuwanywesha wanyama
wao. Mwenyezi Mungu amesema
قال تعالى {وَفِي الْأَرْضِ آَيَاتٌ لِلْمُوقِنِينَ} [الذاريات:20].
Amesema Allah
(Subhaanahu wa Taala): {{ Na katika ardhi kuna alama nyingi kwa wenye
yakini}}. Tukiangalia mbinguni kuna nyota nyingi, jua, mwezi na sayari
nyinginezo. Vilevile mbinguni kuna viumbe vya Mwenyezi Mungu ambao ni
Malaika wanaotekeleza kazi alizowapa Mola aliyetukuka.
Na katika alama
nyingine za kumjua Mwenyezi Mungu ni usiku na mchana. Mchana ni
wakutafuta maisha na riziki na usiku ni kupumzika.
قال تعالى {وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاسًا *وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشًا } [النبأ:11:10] .
Amesema Allah
(Subhaanahu wa Taala): {{ Na tumeufanya usiku ni nguo na tukaufanya
mchana ni wa kutafuta maisha}}. Na katika alama hizi mbili za usiku na
mchana amewafanyia watu mchana kwenda katika ardhi ya Allah na kutafuta
fadhila zake na katika kutafuta fadhila hizo atazidi kubainikiwa
mwanaadamu na kuzifahamu alama nyingine za Mwenyezi Mungu. Na katika
usiku ni wakati wa kujipumzisha baada ya uchovu wa mchana katika hali ya
kutafuta riziki na kutafuta maisha.
Tukigusia zaidi
alama za Allah ni wanyama wengi wakubwa kwa wadogo na katika wadogo kuna
wadogo zaidi, kuna wengine ametufanyia kuwatumia katika kazi zetu za
kila siku, kama kubeba mizigo na kutupeleka sehemu nyingine Na dalili
ya alama za Mwenyezi Mungu ni kuumbwa kwetu kwani kuna mazingatio
makubwa sana.
قال تعالى {وَفِي أَنْفُسِكُمْ أَفَلَا تُبْصِرُونَ} [الذاريات:21].
Mola (Subhaanahu
wa Taala) Amesema:{ Na je katika nafsi zenu basi hamuoni}. Aya hii
inatueleza kuwa katika maumbile yetu wanadamu kuna mazingatio makubwa
kumjua Mwenyezi Mungu. Lengo kuu la kumtambua ni kuzingatia katika
viumbe vyako ni kumjua yeye ili kumthamini, kwani tukimthamini
tutamuabudu haki ya kumuabudu na hilo ndio lengo kuu la kuumbwa majini
na binadamu.
قال تعالى : {وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ} [الذاريات: 56].
Mola (Subhaanahu
wa Taala) Amesema: {{Na sikuumba na majini na binaadamu isipokuwa
waniabudu}}. Napenda kusema kwamba Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)
ndiye aliyeumba ulimwengu wote na viumbe vyote bila usaidizi wa mtu
yoyote na yeye ndiye anayeupeleka ulimwengu huu. Kwa hivyo, Yeye ndiye
anayestahiki ibada kwa sababu hakuna yoyote aliyemsaidia katika uumbaji.
Ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa kuumba na anaupeleka ulimwengu
aliomba anavyotaka na wala haulizwi kwa analofanya bali viumbe ndio
watakaoulizwa katika vitendo vyao.
Ndugu katika
imani! Jueni ya kwamba viumbe vyote ambavyo vinapatikana ulimwenguni
havijileti vyenyewe bali Mwenyezi Mungu aliyetukuka ndiye aliyeviumba
viumbe hivyo.
قال تعالى : {أَمْ خُلِقُوا مِنْ غَيْرِ شَيْءٍ أَمْ هُمُ الْخَالِقُونَ * أَمْ خَلَقُوا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بَل لَا يُوقِنُونَ } [الطور: 36:35].
Mwenyezi Mungu
(Subhaanahu wa Taala) Amesema kwenye Kitabu Chake: {{ Au mumeumbwa kwa
kisichokuwa kitu au nyinyi ndio waumbaji. Au nyinyi ndio mlioumba
mbingu na ardhi bali wao hawana yakini}}. Kulingana na Aya hizi
zinaonesha kwamba ulimwengu haukujiumba wenyewe na haukuwa kiumbe
ambacho hakikumbwa wenyewe na kitu bali lazima tena kuna aliyeumba
ulimwengu huu na akasimama kwa jambo lake (huo ulimwengu) naye si
mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) hakuna Muumba
asiyekuwa Yeye wala Mola asiyekuwa Yeye.
Enyi waumini!
Lau mtaambiwa kuna jumba kubwa la ghorofa lililokamilika, halina kasoro
yoyote, ya kwamba limejijenga lenyewe mtaamini? Bila shaka hili ni
jambo lisilowezekana kabisa. Na lau inasemekana kuwa jumba kubwa la
ghorofa limepatikana ghafla mtaamini? sina shaka kwamba mtasema
haiwezekani. Kwa hivyo, huu ulimwengu ulio mpana uliokwenda juu na
chini. Haiwezekani kabisa kujileta wenyewe na haiwezekani kabisa
kujitokeza ghafla bali ni lazima kuna aliyeuleta ulimwengu huu ambaye
ni Mjuzi Muweza naye ni Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala).
Tujue ya kwamba
hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) katika
kutudhalilishia ardhi na vilivyomo humo. Kwa hivyo, ni lazima kwa kila
Muislamu kushukuru neema kubwa za Mwenyezi Mungu Alizotuneemesha Allah
Mola wa viumbe vyote. Akipenda Mwenyezi Mungu tutabainisha suala la
kuzishukuru neema za Mwenyezi Mungu katika khutba ya pili.
Enyi waumini!
mcheni Allah (Subhaanahu wa Taala) na kumshukuru kwa uongofu aliotupa na
aliyotufundisha yale ambayo tulikuwa hatujui katika mambo yaliyo na
maslahi katika Dini yetu na kutujuza mambo yasiyofikiwa na akili zetu na
ambayo haifungamani na na maslahi yetu hali ya kuwahurumia nyinyi na
hamkupewa ilimu isipokuwa kidogo.
Mwenyezi Mungu
Aliyetuelimisha vipi alianza kuumba huu ulimwenguni, na ilimu hii
huwezi kuipata mpaka kupitia Mtume rehma na amani zimfikie. Na yoyote
atakayetaja chochote kuhusu jinsi ya kuumbwa mbingu na ardhi, hakika
ni wajibu tulinganishe na mafunzo walio kuja nayo Mitume ikiafikiana na
vile walivyotufundisha Mitume, basi itakubaliwa, na ikienda kinyume
na maelezo ya Mitume haikubaliwi na ikiwa Mitume hawakubainisha basi
sisi itabidi tulinyamazie suala hilo wala haifai kabisa kutia ufundi
wetu mpaka itubainikie kuwa ni haki au ni batili.
Tunamshukuru
Mola aliyetukuka. Rehma na amani zimfikie Mtume wetu Muhammad. Ama baada
ya kupeleka shukrani kwa Mwenyezi Mungu na kumtakia rehma na amani
Mtume Muhammad. Tumegusia katika khutba ya kwanza yanayohusiana na
dalili za kumjua Allah katika viumbe vyake, vile vile kubainisha ukubwa
wa Mwenyezi Mungu na kustahiki kwake kuabudiwa peke yake, huku
tukiangazia kudhalilishwa viumbe mbali mbali kwa maslahi ya wanadamu.
Vilevile kulinganiwa watu kutumia viumbe hivi katika kujikurubisha kwa
Mwenyezi Mungu na kumuabudu yeye peke yake. Katika khutba hii ya pili
napenda kubainisha shukrani za wanadamu kwa Mwenyezi Mungu kwa neema
tofauti tofauti.
Enyi ndugu
katika uislamu! Shukrani ni kumsifu aliyekupa neema. Na shukrani kwa mtu
inakusanya nguzo tatu muhimu, kiasi kwamba haiitwi shukrani kwa
Mwenyezi Mungu mpaka zikamilike, nazo ni:
(1) Mtu kuitambua neema katika moyo wake.
(2) Kuizungumza neema ile kwa ulimi wake.
(3) Kuitumia
neema ile katika kumtii Mwenyezi Mungu. Kwa ufupi kabisa tunaweza kusema
kuwa shukurani inafungamana na moyo, ulimi na viungo vya mwanadamu
vilivyobakia. Kazi ya moyo ni kuitambua neema ile ya kwamba inatoka kwa
Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) na kumpenda Mwenyezi Mungu.
Na kazi ya ulimi
ni kuitaja neema ile na kumsifu Mwenyezi Mungu kwa neema hiyo na viungo
vilivyosalia kazi yake ni kuvitumia katika kufanya maamrisho ya
Mwenyezi Mungu. Tusisahau ya kwamba kuna faida anayoipata mwenye
kumshukuru Mola na faida hiyo ni radhi zake Allah (Subhaanahu wa Taala).
قال تعالى {وَاللَّهُ
أَخْرَجَكُمْ مِنْ بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ لَا تَعْلَمُونَ شَيْئًا
وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ لَعَلَّكُمْ
تَشْكُرُونَ} [النحل:78]
Amesema Allah
(Subhaanahu wa Taala): {{ Mwenyezi Mungu Amewatoa katika matumbo ya
mama zenu hali ya kuwa hamjui chochote akawajaalia masikio, macho na
moyo ili mumshukuru yeye}}.
Mtume wetu
Muhammad ni mfano mzuri katika kumshukuru Mola (Subhaanahu wa Taala) kwa
neema nyingi alizomneemesha yeye na viumbe vyote. Alikuwa
Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akiswali mpaka ikivimba miguu
yake akaulizwa: Wewe pia wafanya hivi na umeshasamehewa dhambi zako
zilizotangulia na zitakazaokuja?. Akasema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi
wasallam): Je, basi siwi mja mwenye kushukuru]. Na imethibiti kwamba Mu’adh bin Jabal alifundishwa na Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie kukutaja na kukushukuru wewe na kufanya vizuri ibada yako].
Tunajua vyema
kila wakati tukumbuke kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutudhalilishia
neema nyingi na fadhila zake ili tupate kumuabudu yeye peke yake hana
mshirika. Bado anasisitiza katika suala hili la kushukuru neema za Allah
kwa kutaja neema za Allah kwa wingi. Anasema Hasan Al Baswariy: ‘
Tajeni neema hizi kwa kwa wingi kwani kufanya hivyo ndio kuzishukuru’.
Kwa hakika Mola Amemuamrisha Mtume wake na pia sisi kuzizungumza na
kuzitaja neema tulizopewa aliposema (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى : {وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ} [الضحى : 11]
{{ Na ama neema za Mola wako zizungumze}} [Adhuhaa: 11]
Mwisho wa khutba
hii, nawausia na kujiusia nafsi yangu kutumia neema za Mwenyezi Mungu
vilivyo, kwani utumiaji wa neema vilivyo ni katika kushukuru neema
hiyo. Kutumia macho inavyotakiwa ni kuishukuru neema hiyo kwani wako
watu hawana neema hiyo ya macho,kutumia ulimi vizuri ni kushukuru neema
hiyo ya ulimi. Neema ya mikono na miguu kuzishukuru neema hizi ni
kuzitumia katika mambo ya kheri. Maneno haya tuliyoyataja yanatufundisha
ya kwamba kila neema ina namna yake ya kuishukuru.Tukimalizia neema ya
chakula.
يقول الله تعالى : {يَا
أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ
وَاشْكُرُوا لِلَّهِ إِنْ كُنْتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ} [البقرة : 172]
Mola (Subhaanahu
wa Taala) Amesema: {{ Enyi mulioamini kuleni katika vizuri
mulivyoruzukiwa na mumshukuru Allah ambaye mnamuabudu na kumtii}}
[Al-Baqara : 172]. Pia Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Anasema:
وقال : {فَكُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّهُ حَلَالًا طَيِّبًا وَاشْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّهِ إِنْ كُنْتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ}
[النحل : 114]
{{ Kuleni katika
alivyowaruzuku Allah vilivyo halali vizuri na mushukuru neema za
Mwenyezi Mungu ikiwa kweli mnamuabudu}} [Al-Nahal : 144].
Mwisho
Tunamshukuru
Mola Aliyetuwezesha kuyazungumza yanayohusiana na baadhi ya alama za
kumjua Mungu kupitia viumbe vyake. Pia nimegusia kuhusu ukubwa wa Mungu
na kwamba yeye Ndiye anayestahiki kuabudiwa. Vilevile ni kuweza
kuchambua suala la watu kumshukuru Mungu aliyetudhalilishia viumbe
vyake, na nimewakumbusha katika kutumia neema za Mungu alizotupa kwa
kumuabudu yeye.
Mwisho
kabisa tunamuomba Mwenyezi Mungu Atujaaliye miongoni mwa wenye
kuzishukuru neema zake, na kupata radhi zake, na atujaaliye ni wenye
kumcha na kumuabudu yeye mpaka mwisho wa uhai wetu na tuingie katika
pepo yake. Na rehma na amani zimfikie Mtume Muhammad.
No comments:
Post a Comment
10 Ways of Protection from Shaytan:
Imam Ibn ul Qayyim
Seeking refuge with Allah from Shaytan. Allah the Most High said, “And if there comes to you from Satan an evil suggestion, then seek refuge in Allah. Indeed, He is the Hearing, the Knowing.” [41:36]
Recitation of the two soorahs al-Falaq and an-Nas, as they have wondrous effect in seeking refuge with Allah from evil, weakening Shaytan and protection from him. This is why the Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said: “No person seeks refuge with anything like the Mu`awwidhatayn (soorahs al-Falaq and an-Nas)”. [an-Nasaa’i, 5337]
Recitation of Ayat al-Kursi (2:255).
Recitation of soorah al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “The house in which al-Baqarah is recited is not approached by Shaytan.” [Muslim]
The final part of al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “Whoever recites the two last verses of al-Baqarah at night they will suffice him.” [Muslim]
Recitation of the beginning of soorah Mu’min (Ghafir), until His saying, “wa ilayhi-l-maseer” (to Him is the destination). (i.e. “Ha. Meem. The revelation of the Book is from Allah, the Exalted in Might, the Knowing, the forgiver of sin, acceptor of repentance, severe in punishment, owner of abundance. There is no deity except Him; to Him is the destination.” [40:1-2])
Saying “la ilaha ill Allah wahdahu la sharika lah, lahul mulku wa lahul hamdu wa huwa `ala kulli shay’in qadir” (there is nothing worthy of worship except Allah, He has no partner, His is the Dominion and Praise, and He is able to do all things) a hundred times.
The most beneficial form of protection from Shaytan: abundance of remembrance of Allah, the Exalted.