- Aina
nyingine ya shirki ni kumpenda mtu au kitu zaidi kuliko Mwenyezi Mungu
tena katika hali ya kumtukuza au kukitukuza kitu kile na
kukidhalilikia.Na pindi mapenzi haya yafanyiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu
basi ni shirki.
قال تعالى : {وَمِنَ
النَّاسِ مَنْ يَتَّخِذُ مِنْ دُونِ اللَّهِ أَنْدَادًا يُحِبُّونَهُمْ
كَحُبِّ اللَّهِ وَالَّذِينَ آَمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِلَّهِ } [البقرة : 165].
Amesema Mwenyezi
Mungu (Subhaanahu wa Taala): "Na katika watu wanawafanya wasiokuwa
Mwenyezi Mungu kuwa wanavyompenda Mwenyezi Mungu na hakika walioamini
wanampenda zaidi Mwenyezi Mungu}} [Al-Baqara : 165].
Jueni ndugu
katika imani kwamba ukubwa wa dhambi la shirki kwani Mwenyezi Mungu
hamsamehe anayemshiriksha endapo atafariki na dhambi hizo bila kumtaka
yeye msamaha kwa kuwa Mola (Subhaanahu wa Taala) haridhii isipokuwa
Tawhidi na pia haisamehe shirki. Kwa hivyo, adhabu ya mshirikina ni
kubwa na atapata udhalilifu hapa duniani kabla ya kuadhibiwa kesho
akhera.
قال تعالى : { إِنَّهُ مَنْ يُشْرِكْ بِاللَّهِ
فَقَدْ حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ وَمَا
لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنْصَارٍ} [المائدة:72].
Amesema
Mola (Subhaanahu wa Taala): {{Hakika mwenye kumshirikisha Mwenyezi
Mungu amemuharamisha pepo na makazi yake ni motoni na hawatapata
madhalimu wenye kuwasaidia}} [Al-Maaidah : 72].
Napenda tujiuze maswali yafuatayo;
1- Ni nani katika sisi hataki usalama duniani na kesho akhera?
2- Ni nani kati yetu hataki kuingia peponi bila ya hesabu?
3- Ni nani kati
yetu hataki kupata uhai mzuri duniani na kuokoka siku ambayo haitofaa
mtu mali yake wala watoto isipokuwa atayenda kwa Mwenyezi Mungu kwa moyo
uliyosalimika na madhambi?
Jawabu la
maswali tuliyoyauliza kuitekeleza Tawhidi katika maisha yake yote. Kubwa
linalotakiwa ni mtu kujifundisha mambo yanayofungamana na Tawhidi
vizuri kuyatilia umuhimu mkubwa katika maisha yake kwa kusoma vitabu vya
Tawhidi na kusikiliza darasa za wanavyuoni walioshikamana na Tawhidi na
sunna, kwani kufanya hivyo ni nuru katika nyoyo. Na vile vile kuvisoma
vitabu vya Tawhidi ili kujua Tawhidi ni nini Tawhidi,sababu za
shirki,hukmu za shirki na dalili za hukumu za shirki hizo, kuyajuwa hayo
ni mwangaza ili mtu asibaki katika giza la shirki, na Tawhidi pia
hutengeneza moyo wa mtu na jamii kwa jumla.
Enyi ndugu
katika imani! Msihadaike na dunia na kuipuuza Tawhidi iliyokusanya kila
kitu na kila mafanikio duniani na kesho akhera na kwa ajili ya Tawhidi
wametumlizwa Mitume wote na kuumbwa pepo na moto. Nawausia ndugu zangu
Waislamu mulipe suala hili la Tawhidi kipaumbele katika maisha yetu, na
muikabili Tawhidi kwa nia njema na nia ya kweli. Na haifai kulipuuza kwa
hali yoyote kwani atayelipuuza suala hili yuko katika hatari kubwa
duniani na vile vile kesho akhera.
Mwisho
Twamshukuru
Mungu tumegusia nukta muhimu kwa kubainisha umuhimu wa Tawhidi na kwamba
Tawhidi ni sababu kubwa ya kuokoka mwanadamu siku ya kiama kupata
msamaha pia tukabainisha kwamba Tawhidi ni sababu ya kuondoshewa balaa
na fitna na mwisho tumebainisha umuhimu wa kujifundisha Tawhidi na
shirki kwa aina zake.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Azitengeneze nia zetu katika vitendo vya kila siku na azitengeneze ibada zetu za kwa jumla, pia Aitengeneze Dini yetu na dunia yetu kwani yeye ni muweza wa kila kitu.
No comments:
Post a Comment
10 Ways of Protection from Shaytan:
Imam Ibn ul Qayyim
Seeking refuge with Allah from Shaytan. Allah the Most High said, “And if there comes to you from Satan an evil suggestion, then seek refuge in Allah. Indeed, He is the Hearing, the Knowing.” [41:36]
Recitation of the two soorahs al-Falaq and an-Nas, as they have wondrous effect in seeking refuge with Allah from evil, weakening Shaytan and protection from him. This is why the Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said: “No person seeks refuge with anything like the Mu`awwidhatayn (soorahs al-Falaq and an-Nas)”. [an-Nasaa’i, 5337]
Recitation of Ayat al-Kursi (2:255).
Recitation of soorah al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “The house in which al-Baqarah is recited is not approached by Shaytan.” [Muslim]
The final part of al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “Whoever recites the two last verses of al-Baqarah at night they will suffice him.” [Muslim]
Recitation of the beginning of soorah Mu’min (Ghafir), until His saying, “wa ilayhi-l-maseer” (to Him is the destination). (i.e. “Ha. Meem. The revelation of the Book is from Allah, the Exalted in Might, the Knowing, the forgiver of sin, acceptor of repentance, severe in punishment, owner of abundance. There is no deity except Him; to Him is the destination.” [40:1-2])
Saying “la ilaha ill Allah wahdahu la sharika lah, lahul mulku wa lahul hamdu wa huwa `ala kulli shay’in qadir” (there is nothing worthy of worship except Allah, He has no partner, His is the Dominion and Praise, and He is able to do all things) a hundred times.
The most beneficial form of protection from Shaytan: abundance of remembrance of Allah, the Exalted.