.
Uzuri wa mwanamke katika nchi za Magharibi, na dunia kwa upana unafahamika kwa mtazamo maalumu, hufafanuliwa ati kuwa ni mwanamke mrefu, mwenye umbo mwanana, na sifa linganifu kwa uzuri wa sura, pua ya wastani, midomo ya kuvutia na nywele nyepesi zenye mremeto mara nyingi hupendelewa ziwe ndefu.
Kipimo hiki cha ‘mwanamke mzuri’ awali kimefafanuliwa na mataifa ya Magharibi ya kibepari ambapo mwanamke anayefikia kipimo hicho huhusishwa na ufanisi, kujiamini, kuwa na thamani na kuheshimiwa katika jamii. Germaine Greer, mwandishi na mtetezi wa haki za wanawake wa Magharibi anaelezea zaidi uhusiano kati ya uzuri na mafanikio katika kitabu chake kinachoitwa ‘The Whole Woman’ “Kila mwanamke anajua kwamba, licha ya kupata mafanikio mengine yote, atakuwa amefeli kama yeye si mzuri” Kwa bahati mbaya wanawake wa Kiislamu nao pia wamekumbwa na fikra na janga hili la kujitumbukiza katika fani ya urembo ili wajisikie wana thamani katika jamii.
Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kwamba mtazamo huu anaotaka mwanammke kushikamana nao si tu unawakilisha mwanamke huyo anavyotaka kujionesha kiwiliwili chake kwa ulimwengu, lakini pia unawakilisha haiba yake halisi, jinsi anavyoyaona maisha na jinsi anavyotaka kuishi katika maisha yake.
Mwanamke wa kiMagharibi hujivuna kwa kuwa yeye ni imara na huru mwenye kujitegemea, kushikilia imani kuwa yeye yupo huru huwakilisha anavyotaka na kuishi maisha anayotaka – kama yalivyo madai ya jamii huria za kidemokrasia. (secular liberal). Lakini ukweli uko mbali kabisa na mtazamo huu wa kijinga. Jamii ya Kimagharibi ya kibepari ambayo inajali zaidi maslahi kuliko misingi ya utu ndio iliyoweka kipimo cha mambo yanayofanya ‘uzuri’, na kwa sababu ya mtazamo huu huwafanya wao ni wenye kupagawa katika mambo ya mitindo na majarida ya urembo bila ya kusahau matumizi ya mabilioni kwa mambo ya urembo na nyengine kwenda kwa viwanda vya vipodozi.
Je kipimo cha urembo cha kiMagharibi kinaweza kupatikana?
Mafanikio ya masuala ya urembo na viwanda vya vipodozi vinategemea kwa kiasi kikubwa juu ya ukweli usiofichika kwamba urembo wa mwanamke mzuri kamwe haufikiwi , kwa kuwa viwanda vinafaidika kwa wanawake kutotosheka na maumbile yao na kuwalazimisha kugharamika kununua kila bidhaa ya urembo au kufanyiwa operesheni ya urembo ili kukabiliana na mbio za vigezo vya urembo unaokubalika.
Kwa hakika, haingii akilini kutarajia kuwa mwanamke wa jamii moja achilia mbali dunia nzima, apimwe kwa urefu fulani, uzito fulani, rangi fulani ya mwili na nywele, kwa sura fulani na umri fulani. Ukweli ni kwamba fikra hii haiendani na hali halisi ya maisha, bali kinachojitokeza zaidi katika hili ni sekta ya matangazo ya mara kwa mara ili kupima kwa vipimo bandia kama vile picha za warembo, na matumizi ya teknologia ya elektroniki ili kuchapua kipimo cha haiba ya mrembo bora.
Katika Uislamu hakuna dhana potofu ya kimagharibi juu ya urembo. Uislamu haujishughulishi kabisa kuweka viwango vya udanganyifu na visivyowezekana vya urembo, kisha kutarajia kuvifikia, badala yake umetuwekea ipi picha halisi tunahitaji kuwa nayo katika mazingira mbalimbali. Uzuri kwa mwanamke wa Kiislamu ni kufuata hukmu za kisharia, na ubaya ni kuziwacha hukmu hizo na kufuata matamanio ya nafsi zetu.
Kushikamana na aina hii ya muelekeo ni kitu ambacho kimo ndani ya uwezo wa kila mtu, na unatukomboa kutoka katika shinikizo kuwa ‘ndani ya mbio za urembo’ na kubadilisha ngozi zetu, upana wa umbo letu nk. Mambo ambayo udhati wake hayakubaliani na hali halisi na hayawezekani kamwe.
Mwanamke wa Kiislamu ana msingi madhubuti wa kujihukumu yeye mwenyewe na wengine. Msingi ambao haubadiliki kulingana na kufuata kila mkondo unaoibuka. Yeye anachojali ni juu ya utii kwa Mwenyezi Mungu سبحانه وتعالى na ana uhakika kuwa hiki ndicho kipimo sahihi cha mafanikio.
إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ
“Hakika mbora wenu kwa Mwenyezi Mungu ni yule mcha Mungu (muumini) zaidi mwenye
Taqwa” [Al-Hujrat 13]
Kwa hiyo, suala kubwa tunalopaswa kuwa nalo si upi urembo wa ‘ndani’ na upi urembo wa ‘nje’ , lakini cha msingi ni kujifunga kuwa Muislamu kikamilifu (shakhsiya ya Kiislamu), ambaye anafikiria juu ya mambo yote ndani ya mipaka ya Uislamu.
Aidha, tunapaswa kutambua kwamba kuna udanganyifu wa mabilioni ya pesa unaoendelea. Hakuna mwanaadamu wa kweli anayeonekana kama picha zilizo ndani ya majarida ya warembo, ambazo daima hughushiwa na za udanganyifu. Maadili tunayopaswa kushikamana nayo lazima yawe ni kutoka ndani ya Uislamu peke yake, kwa kuwa huu ndio mtazamo sahihi kwa kila kitu. Hebu tuweni wanawake Waislamu wanaofikiri ambao hujali vitu sahihi na sio kuburuzwa na yale wanayovaa wana mitindo na warembo maarufu. Ambapo vipodozi kutufanya sisi kuonekana weupe, na upumbavu wa chakula gani cha kujaribu kesho ili kufinyanga miili yetu. Mwisho wa maneno mfumo unaotawala dunia wa kibepari, haujali zaidi ya utajirisho wa mapesa. Na hiyo ndio sababu ya msingi inayowafanya kuweka vipimo hivi. Ambavyo ni wajibu kuvipinga kwa nguvu zote na kuleta mabadiliko.

No comments:
Post a Comment
10 Ways of Protection from Shaytan:
Imam Ibn ul Qayyim
Seeking refuge with Allah from Shaytan. Allah the Most High said, “And if there comes to you from Satan an evil suggestion, then seek refuge in Allah. Indeed, He is the Hearing, the Knowing.” [41:36]
Recitation of the two soorahs al-Falaq and an-Nas, as they have wondrous effect in seeking refuge with Allah from evil, weakening Shaytan and protection from him. This is why the Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said: “No person seeks refuge with anything like the Mu`awwidhatayn (soorahs al-Falaq and an-Nas)”. [an-Nasaa’i, 5337]
Recitation of Ayat al-Kursi (2:255).
Recitation of soorah al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “The house in which al-Baqarah is recited is not approached by Shaytan.” [Muslim]
The final part of al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “Whoever recites the two last verses of al-Baqarah at night they will suffice him.” [Muslim]
Recitation of the beginning of soorah Mu’min (Ghafir), until His saying, “wa ilayhi-l-maseer” (to Him is the destination). (i.e. “Ha. Meem. The revelation of the Book is from Allah, the Exalted in Might, the Knowing, the forgiver of sin, acceptor of repentance, severe in punishment, owner of abundance. There is no deity except Him; to Him is the destination.” [40:1-2])
Saying “la ilaha ill Allah wahdahu la sharika lah, lahul mulku wa lahul hamdu wa huwa `ala kulli shay’in qadir” (there is nothing worthy of worship except Allah, He has no partner, His is the Dominion and Praise, and He is able to do all things) a hundred times.
The most beneficial form of protection from Shaytan: abundance of remembrance of Allah, the Exalted.