Followers

Thursday, May 9, 2013

SERIKALI IMETOA TAMKO YA KUPIGA MARUFUKU MIHADHARA YA KIDIIN

MIHADHARA YA KIDIIN KUPIGWA MARUFUKUwww.fahadahm.blogspot.com
HATIMAYE Serikali imeanza kubaini sehemu ya kiini cha vurugu na vitendo viovu vinavyofanywa kwa kisingizio cha udini nchini na kutangaza hadharani kuwa mihadhara ya kidini inachangia.

Mihadhara kama mihadhara ambayo inalenga kueneza Neno la Mungu haina matatizo, lakini inapotumiwa kuhubiri mabaya ya dini nyingine, hapo ndipo inapopoteza umuhimu.

Lakini kwa kuwa sasa Serikali imeuona mchango wa mihadhara hiyo katika vurugu za kidini, ni dhahiri kwamba hatua zinapaswa kuchukuliwa, ikiwa ni pamoja na kutoa uamuzi mgumu ili kunusuru amani ya nchi.

Awali, waumini wa dini za kiislamu na kikristo, walidhani kuwa kuanzishwa kwa mihadhara hiyo kulilenga kuhubiri dini na kuwapa mafunzo mema waumini kama ifanyikavyo ndani ya majengo ya ibada.

Imani hiyo ndiyo ilifanya hata Serikali kudhani kweli hayo ndiyo yanayofanyika, lakini kumbe baadhi ya wahubiri ambao ni viongozi wa dini, walianza kutetereka na kutumia vibaya majukwaa ya mahubiri hayo.

Waliibuka waumini wa dini hizo mbili kubwa nchini, wakaanza kuchambua Biblia na Korani kinyume na makusudio, lengo likiwa ni kuonesha kuwa vitabu hivyo vitukufu si lolote bali vinadanganya waumini.

Polepole mahubiri hayo yaliachiwa kukithiri na kujenga chuki katika nyoyo na vichwa vya waumini na hatimaye dini moja kuonekana haifai na nyingine inafaa.

Bila shaka upotofu na upotoshaji huo ndio uliofanya sasa waibuke wanadini wanaovutana kuhusu nani achinje na nani asichinje, wakisahau kuwa huko nyuma jambo hilo lilifanyika bila ubishani wala ugomvi!

Mihadhara potofu ya kuponda dini nyingine, ndiyo iliyowafikisha Watanzania walipo hivi sasa ambapo mtu wa dini moja anamwangalia wa nyingine kwa jicho la chuki na husuda.

Mihadhara hii ambayo imekuwa ikifanyika katika maeneo ya wazi na kutumia vipaza sauti vyenye sauti kubwa mchana na usiku, imekuwa ikivuta hisia za wengi na wengine kushawishika kufanya hata mabaya yanayohubiriwa.

Chuki ya kidini hushika zaidi katika akili za binadamu na kuzama katika nyoyo zao na hivyo kuwa vigumu sana kumgeuza kirahisi aliyeamini na ndiyo sababu wengine huwa tayari kujitoa mhanga ‘kufia dini’.

Ikumbukwe, kwamba viongozi wa dini huaminika zaidi ya hata viongozi wa familia, kaya, siasa na hata serikali; wanalolisema wao linaaminika kwa sababu ndiyo njia ya kuuona ufalme wa Mbinguni.

Kutokana na ukweli huo, ndiyo sababu tumesikia vita vya wenyewe kwa wenyewe visivyomalizika katika nchi ambako chuki za kidini zimetamalaki.

Watanzania tunaelekea huko, tukioneana haya sasa na kuacha hali hii ijichimbie miongoni mwa jamii, matokeo yake yatakuwa mabaya na hakutakuwa na wa kulaumiwa ila sisi wenyewe.

Tufike mahali sasa tuone kuwa kuendelea na hali hiyo ni hatari kwa mustakabali wa nchi, kwani tutafikia mahali ambako tutapigana kidini vita ambavyo mwisho wake hakika ni mgumu.

Serikali sasa isimame kidete na kutoa kauli nzito, kwamba kuanzia sasa mihadhara ya kidini imepigwa marufuku na kama ni mafunzo ya dini na mahubiri yafanyike ndani ya makanisa na misikiti na majengo mengine ya ibada

No comments:

Post a Comment

10 Ways of Protection from Shaytan:

Imam Ibn ul Qayyim

Seeking refuge with Allah from Shaytan. Allah the Most High said, “And if there comes to you from Satan an evil suggestion, then seek refuge in Allah. Indeed, He is the Hearing, the Knowing.” [41:36]

Recitation of the two soorahs al-Falaq and an-Nas, as they have wondrous effect in seeking refuge with Allah from evil, weakening Shaytan and protection from him. This is why the Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said: “No person seeks refuge with anything like the Mu`awwidhatayn (soorahs al-Falaq and an-Nas)”. [an-Nasaa’i, 5337]

Recitation of Ayat al-Kursi (2:255).

Recitation of soorah al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “The house in which al-Baqarah is recited is not approached by Shaytan.” [Muslim]

The final part of al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “Whoever recites the two last verses of al-Baqarah at night they will suffice him.” [Muslim]

Recitation of the beginning of soorah Mu’min (Ghafir), until His saying, “wa ilayhi-l-maseer” (to Him is the destination). (i.e. “Ha. Meem. The revelation of the Book is from Allah, the Exalted in Might, the Knowing, the forgiver of sin, acceptor of repentance, severe in punishment, owner of abundance. There is no deity except Him; to Him is the destination.” [40:1-2])

Saying “la ilaha ill Allah wahdahu la sharika lah, lahul mulku wa lahul hamdu wa huwa `ala kulli shay’in qadir” (there is nothing worthy of worship except Allah, He has no partner, His is the Dominion and Praise, and He is able to do all things) a hundred times.

The most beneficial form of protection from Shaytan: abundance of remembrance of Allah, the Exalted.

احمد محب الدين الأخبار جديد/احب الله ورسوله

حبّ الرسول صلّى الله عليه وسلّم

قال عليه والصلاة والسلام <<من أحبّ سنّتي فقد أحبّني ومن أحبني كان معي في الجنة>>وقال تعالى<<قل إن كنتم تحبّون الله فاتبعوني يحبب كم الله و يغفر ذنوبكم>>

Popular Posts