Followers

Thursday, May 9, 2013

UZAWA WA MTUME (SAAW) NI BISHARA YA USHINDI WA UMMA WETU



Amesema Mtume SAAW :
“Mimi ni dua ya baba yangu Ibrahim, ni bishara ya Issa, na mama yangu aliona ndotoni akitoka nuru (tumboni) kuyaangazia maqasri ya Sham”. (Imam Ahmad)
Kipenzi chetu Mtume SAAW ni dua ya Ibrahim As. kama Quran inavyotukumbusha:
رَبَّنَا وَابْعَثْ فِيهِمْ رَسُولاً مِنْهُمْ ا
“Ewe Mola wetu! Waletee Mtume anaetokana na wao” (2: 129)
Na pia ni bishara ya Issa As. alipowaeleza wana wa Israil kama ilivyotajwa ndani Quran.
وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِنْ بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ
”Na mimi ni Mwenye kuwabashiria Mtume baada yangu, jina lake ni Ahmad”. (61:6)
Amma kutoka nuru tumboni ni ndoto aliyoiona mama yake Mtume SAAW alipokuwa mja mzito akiwa na mimba ya Kipenzi chetu Mtume SAAW. Nayo ni bishara ya ushindi unaoendelea wa umma wake mpaka siku ya kiyama. Licha ya umma wake kusibiwa na kufikwa na mitihani na kutetereka hapa na pale kama hali tuliyonayo leo tangu kuangushwa Khilafah. Ikifafanua bishara hii ya ushindi Tafsiri ya Muhtaswar Ibn Kathir inanena haya:
‘ Na kuhusishwa Sham katika bishara hii ni kutokana na ukweli kwamba Sham itakuwa ndio Makao Makuu ya Uislamu katika zama za mwisho’ (akheri zaman).

Kama alivyosema Mtume SAAW :”Halitoacha kundi katika umma wangu kusimama juu ya haki, halitodhurika kwa atakaelipinga , wala halitodhoofika kwa kuwachwa mkono mpaka ije amri ya Mungu (ushindi) Nalo litatoka Shaam” (Bukhar na Muslim) (Mukhtaswar Ibn Kathir vol. 1 aya 129 Surat Baqara).
Na Sham ni maeneo ya Syria, Lebanon, Palestina, Jordan, na baadhi ya maeneo ya Iraq. Bishara hii ni moja katika nyingi juu ya ushindi wa umma huu, kama vile pia alivyosema Mtume SAAW: “Hakika Allah amenisogezea dunia yote nikaona kutoka mashariki mpaka magharibi .Na kwa hakika utawala wa umma wangu utafika sehemu zote nilizosogezewa. Na nimepewa khazina mbili, nyekundu na manjano. (Muslim)

Aidha, kuna bishara ya kurudi tena Khilafah, baada ya watawala waovu, inayosema: ‘kisha itarudi tena Khilafah kwa manhaj ya utume… au alipobashiri Mtume SAAW kuifungua/fathi Constatinople/Istambul iliyofunguliwa na Muhammad Fathi, na kufunguliwa kwa Rome ambayo bado haijafunguliwa, lakini ufunguzi wake hauna shaka insha-Allah.
Bishara hizi ni za ushindi kwa umma huu, lakini ni lazima tuweke ufahamu wa kina juu ya dhana na makusudio ya bishara. Kwa kuwa makafiri na masheikh wa vibaraka huleta ufahamu wa kimakosa kiasi cha kuwachanganya hata wenye ikhlasi.

Kwanza, endapo bishara imethibiti usahihi wake kutoka katika aya au hadithi za tawatur kuikanusha ni kuingia katika ukafiri . Kwa kuwa bishara huingia katika mambo ya kiimani /kiakida, nako ni kuamini mambo ya ghaib ambayo Muislamu huwajibika kuamini kama yalivyo, bila ya kutoa vigezo vya kiakili wala kutizama mawafikiano ya bishara hiyo na mazingira yaliyotuzunguuka.

Pili, kuamini bishara maana yake sio kujipweteka na kusubiri bishara hiyo ijiri, na kuacha kufanya kazi ya ulinganizi wa kurejesha dola, au kusema kama wanavyosema baadhi ya makundi kwamba hakuna haja ya kushughulika ‘Khilafah ni ahadi ya Allah Taala’. Hapana shaka ni ahadi ya Allah Taala hakuna anayelipinga hilo, lakini sheria imetufunga kufanya matendo maalum kuiendea bishara hiyo, na kufanya matendo hayo au kutofanya, hakuzuii bishara husika kujiri. Lakini lau hatukufanya matendo tuliyoamrishwa katika mzunguuko wetu wa kibinaadamu tutakuwa na dhambi, kwa kuwa sheria imetutaka tufanye matendo hayo.Hakuna mbora wa kufahamu bishara ya ushindi kama kipenzi chetu Mtume SAAW, lakini alihangaika kutafuta nusra kwa makabila mbalimbali ili asimamishe dola, alihajiri Makka kwa siri, alijificha, kukodi mjuzi wa njia, alipigana jihadi nyingi nk. Yote haya si kwa sababu alikuwa na shaka juu ya ushindi alioahidiwa, bali matendo haya huingia katika upande wa amri za Allah Taala ambazo aliwajibika atende na sio kujipweteka kusubiri ushindi. Au masahaba, nao walielewa vyema kuhusu bishara na hawakuwa na shaka juu ya bishara mbali mbali, lakini walifanya matendo waliyotakikana na sheria kuyatenda.

Tatu, bishara tulizopewa lazima zitulize nyoyo za Waislamu na sio kutapatapa na kujiingiza katika aibu, fedheha na mitego ya makafiri, kana kwamba hatuna mfumo kamili wa maisha wenye manhaj/njia yake yenye kujitosheleza. Kiasi cha baadhi kudiriki hata kudandia ukafiri kama kuunga mkono vyama vya kikafiri vya kidemokrasia na mchakato wa katiba zao za kikafiri za kiilmania/kisekula na za kitwaghuti. Mtume SAAW hata katika hali ngumu ya kuteswa watu wake na kunyanyaswa hakujiingiza kuunga mkono tawala za kikafiri wala taratibu/nidhamu zao. Na kwa hakika yeye alipewa kubwa zaidi, na sio kutoa maoni katika katiba ambayo wenye nidhamu yao wakitaka watayachukua maoni hayo na wasipotaka watayatupilia mbali! Bali Mtume SAAW alitaka kupewa ufalme kamwe, na alikataa kata kata. Au pia alipoona masharti ya baadhi ya makabila yaliyotaka kumpa nusra ya kusimamisha dola yanapingana na Uislamu kama vile kabila Amr bin S’asah walipotaka kumpa utawala lakini akiondoka uwe katika mikono ya kabila hilo. Mtume SAAW alikataa kata kata. Au pale kabila la Bani Shayban walipompa masharti ya kuwa wampe Mtume SAAW hatamu za madaraka lakini kwa sharti asipigane vita na Mafursi, kwa kuwa kabila hilo lina mkataba na Mafursi juu ya jambo hilo. Mtume SAAW alilikataa. Aliyakataa masharti haya yote na akasimama na msimamo thabiti wa Kiislamu wala hakuleta kisingizio cha maslahi ya Waislamu. Licha ya kujua kwa yakini kwamba watu wake wanateswa, wana tabu na mashaka kiasi cha kuhitaji nusra ili wapate faraja.

Ajabu ! Ambayo baadhi ya Waislamu hawaizingatii ni kwamba makafiri hawaongozwi na wahyi, wala hawana bishara yoyote upande wao, bali wanaongozwa na matamanio yao na mipango ya akili zao finyu. Lakini wao wanajiamini katika kusukuma ajenda zao za kipotofu na huzileta kwa Waislamu moja kwa moja (radically) bila ya kusita sita. Basi iweje sisi Waislamu ambao Allah Taala yuko upande wetu , bishara za kipenzi chetu SAAW ziko upande wetu na tunafuata dini ya haki, kwanini tuwe na wasiwasi juu ya ushindi wetu?

Ni wajibu Waislamu katika kipindi hiki cha Mfunguo sita tunachokumbuka uzawa wa kipenzi chetu Mtume SAAW kurejea juu ya mstari wetu kama alivyotuonesha yeye kivitendo, na tusikubali kuburuzwa katika kutetea ukafiri kwa visingizio vya ‘maslahi ya Waislamu’. Visingizio vya uwongo vinavyotumika kuwahadaa Waislamu kubeba ajenda za kikafiri.

No comments:

Post a Comment

10 Ways of Protection from Shaytan:

Imam Ibn ul Qayyim

Seeking refuge with Allah from Shaytan. Allah the Most High said, “And if there comes to you from Satan an evil suggestion, then seek refuge in Allah. Indeed, He is the Hearing, the Knowing.” [41:36]

Recitation of the two soorahs al-Falaq and an-Nas, as they have wondrous effect in seeking refuge with Allah from evil, weakening Shaytan and protection from him. This is why the Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said: “No person seeks refuge with anything like the Mu`awwidhatayn (soorahs al-Falaq and an-Nas)”. [an-Nasaa’i, 5337]

Recitation of Ayat al-Kursi (2:255).

Recitation of soorah al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “The house in which al-Baqarah is recited is not approached by Shaytan.” [Muslim]

The final part of al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “Whoever recites the two last verses of al-Baqarah at night they will suffice him.” [Muslim]

Recitation of the beginning of soorah Mu’min (Ghafir), until His saying, “wa ilayhi-l-maseer” (to Him is the destination). (i.e. “Ha. Meem. The revelation of the Book is from Allah, the Exalted in Might, the Knowing, the forgiver of sin, acceptor of repentance, severe in punishment, owner of abundance. There is no deity except Him; to Him is the destination.” [40:1-2])

Saying “la ilaha ill Allah wahdahu la sharika lah, lahul mulku wa lahul hamdu wa huwa `ala kulli shay’in qadir” (there is nothing worthy of worship except Allah, He has no partner, His is the Dominion and Praise, and He is able to do all things) a hundred times.

The most beneficial form of protection from Shaytan: abundance of remembrance of Allah, the Exalted.

احمد محب الدين الأخبار جديد/احب الله ورسوله

حبّ الرسول صلّى الله عليه وسلّم

قال عليه والصلاة والسلام <<من أحبّ سنّتي فقد أحبّني ومن أحبني كان معي في الجنة>>وقال تعالى<<قل إن كنتم تحبّون الله فاتبعوني يحبب كم الله و يغفر ذنوبكم>>

Popular Posts