MAFUNZO YA NDOA KUTOKA KWA FATMA BINT RASULU-LLAH.
Ilikuwa katika mwaka wa 2AH. Imam Ali (ra) alipomkabili Mtume SAAW kwa lengo la kumchumbia Bibi Fatma ( ra) na kumueleza :
‘Ewe Mtume wa Allah, umenilea mimi k...ama mwanao mwenyewe. Ulinijaza na zawadi zako, ukarimu wako na wema wako. Nimepewa nawe kila kitu katika maisha yangu. Sasa naomba wema mmoja zaidi kutoka kwako’.
Mtume SAAW alifahamu kwa kina lengo la Imam Ali ra. na akawa hana budi ila kumueleza mwanawe Bi Fatma: Kwamba Ali anaomba uchumba wake, na kumtaka jibu lake. Hata hivyo Fatma Zahra ra. akabakia kimya bila ya jibu lolote, na Mtume SAAW akatafsiri kimya chake ni kukubaliana na posa hiyo. Akarudi Mtume SAAW kumjuulisha Ali ra. kwamba ombi lake limekubaliwa. Na akamtaka aanze kufanya matayarisho ya harusi.
Miezi miwili baada ya ushindi wa Waislamu katika vita vya Badr, Imam Ali RA. na Bi Fatma
Zahra Binti wa Mtume SAAW walifunga ndoa. Maandalizi ya harusi yakafanywa, na Mtume SAAW akamkabidhi shughuli yote ya harusi kwa upande wa wanawake kusimamiwa na ‘nyanya’ yake Ummu Ayman.
Mwanzoni mwa mwezi wa Dhul-hijjah katika mwaka wa 2AH Mtume aliwaalika masahaba wa Muhajirina na Answar kuhudhuria katika shughuli ya harusi. Mtume SAAW mwenyewe akatowa hotuba ya ndoa, akawaozesha na akawatangaza rasmi Ali ra. na Bibi Fatma ra. kwamba tayari wameshakuwa mke na mume. Wageni waalikwa waliandaliwa na Mtume SAAW karamu ya nyama ya kondoo, mikate na kinywaji cha mchanganyiko wa tende na maziwa (juice). Waislamu wakala, wakanywa, wakafurahi na wakampongeza Mtume SAAW na maharusi katika tukio hili tukufu lililojaa baraka tele. Na Mtume SAAW akaomba baraka za Allah ziwe juu yao wote.
Siku chache baadae, ndani ya mwezi wa Dhul-hijjah, Bibi Fatma Zahra akaiga nyumba yao aliyokuwa akiishi na kupelekwa nyumbani kwa mumewe. Bibi Fatma akasaidiwa na Baba yake kupanda juu ya ngamia maalum kuelekea nyumbani kwake.
Katika siku hiyo, mji wote wa Madina ulijaaa furaha, nderemo, vifijo, hoi hoi na kuririma kwa ‘takbeer’. Salman al Farsi alishikilia hatamu za ngamia wa Bibi Harusi (ambae alikuwa ngamia jike wa Mtume SAAW) akaongoza msafara huku akisoma aya tukufu za quran, Mtume SAAW nae alitembea upande mmoja wa msafara, na upande wa pili alikuwepo Ami yake Hamza RA. (Bwana wa Mashahid).
Masahaba jumla na vijana wapanda farasi wa Bani Hashim walipanda farasi kama wasindikizaji wa bibi harusi. Panga zao zikiririma na kumeremeta na kunyanyuliwa juu kwa furaha isiyo na kifani. Nyuma yao wanawake wa Muhajirina na Answar wakiimba qasida nzuri nzuri katika maandamano yaliyozunguuka Msikiti wa Mtume (Masjid Nabawi) na yakafikia kilele chake chini ya nyumba ya maharusi. Baada ya kushuka bi harusi juu ya ngamia wake, Mtume SAAW akauchukua mkono wa bi Fatma ra. na akauweka juu ya mkono wa mumewe, akasimama juu ya kizingiti cha nyumba yao na kuwaombea dua:
‘Ewe Allah ninawaweka Ali na Fatma, waja wako wanyenyekevu, kwenye ulinzi Wako. Uwe Wewe ndio Mlinzi wao. Wabariki hawa. Kuwa radhi nao, na uwape neema Zako zisizo na mipaka, huruma, na fadhila Zako bora juu yao. Uifanye ndoa yao kuwa yenye matunda, na uwafanye wote imara katika upendo Wako, na ibada zako.’
Pamoja na mafunzo mengi yaliyomo katika tukio hili kubwa. Hata hivyo, funzo moja kubwa na muhimu linadhihirika wazi wazi. Namna Mtume SAAW alivyoondosha fikra chafu ya uaswabia na ubaguzi kivitendo kwa kuwashirikisha mstari wa mbele kikamilifu masahaba wasiokuwa waarabu katika tukio hili. Hilo hudhihirika katika hali mbili. Kwanza, alimpa jukumu nyanya yake Ummu Ayman kusimamia shughuli ya harusi kwa upande wa wanawake. Huyu ni mwanamke mwenye asili ya kihabeshi (Ethiopia) awali aliyekuwa mtumwa wa baba yake Mtume SAAW, na baadae Mtume akampa uhuru wake. Ikumbukwe kwamba Ummu Ayman kwa kauli ya Mtume SAAW ni mwanamke wa peponi, na ndie mwanamke aliyekuja kuolewa na Zaid bin Harith ra. na kumzaa shujaa katika mashujaa wakubwa wa kiislamu. Jemadari Usamah bin Zaid ra. Sahaba ambae pia Mtume SAAW alimpa jukumu la ujemadari wa jeshi la kiislamu bila ya kuzingatia kabila wala nasabu yake, na akawaacha wenye makabila makubwa ya kiqureish na waarabu jumla katika kubeba jukumu hili.
Katika hali ya pili, Mtume SAAW alimchagua Salman Al Farsi kuongoza msafara wa bi harusi bila ya kumzingatia kwamba yeye si muarabu. Bali alimpa hadhi hiyo kwa moyo mkunjufu bila ya kuonyesha hisia yoyote ya kibaguzi. Salman ra. awali kabla ya kusilimu aliwahi kuuzwa kuwa mtumwa wa yahudi katika viunga vya Madina, na akakombolewa baada ya kusilimu kwake. Uislamu ukampandisha daraja ya juu hadi siku moja ‘Muhajirina’ na ‘Answar’ walipozozana juu ya haiba yake, wengine wakisema Salman ni ‘Answar’ na baadhi wakisema ni katika ‘Muhajirina’. Mtume akaondosha mzozo wao huo kwa kusema: ‘Salman ni katika Ahul-bayt yangu’.
Leo umma wa kiislamu baada ya kuanguka Khilafah na kufitinishwa na makafiri umesibiwa kwa kiasi kikubwa na uchafu, uovu na maradhi ya dhambi kubwa ya uaswabia na ubaguzi, kuanzia wa kimaeneo, kikabila, rangi, nchi nk. Dhambi ambayo Mtume SAAW aliikemea wazi kwa ukali kwamba ni ‘uvundo’ na tujiepushe nao. Na badala yake Uislamu unatuamrisha kwamba kipimo pekee cha kumzingatia mtu ni Uislamu na ucha Mungu wake.Tukumbuke kauli yake Mtume SAAW aliposema:
‘Kwa hakika watu wote tangu zama za Adam mpaka leo wako sawa kama meno ya kitana, na hakuna ubora juu ya Muarabu kwa asiyekuwa Muarabu, wala ubora wa Mwekundu kwa Mweusi, ila kwa ucha Mungu.’(Mustadarak- ul-Wasa’il)

No comments:
Post a Comment
10 Ways of Protection from Shaytan:
Imam Ibn ul Qayyim
Seeking refuge with Allah from Shaytan. Allah the Most High said, “And if there comes to you from Satan an evil suggestion, then seek refuge in Allah. Indeed, He is the Hearing, the Knowing.” [41:36]
Recitation of the two soorahs al-Falaq and an-Nas, as they have wondrous effect in seeking refuge with Allah from evil, weakening Shaytan and protection from him. This is why the Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said: “No person seeks refuge with anything like the Mu`awwidhatayn (soorahs al-Falaq and an-Nas)”. [an-Nasaa’i, 5337]
Recitation of Ayat al-Kursi (2:255).
Recitation of soorah al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “The house in which al-Baqarah is recited is not approached by Shaytan.” [Muslim]
The final part of al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “Whoever recites the two last verses of al-Baqarah at night they will suffice him.” [Muslim]
Recitation of the beginning of soorah Mu’min (Ghafir), until His saying, “wa ilayhi-l-maseer” (to Him is the destination). (i.e. “Ha. Meem. The revelation of the Book is from Allah, the Exalted in Might, the Knowing, the forgiver of sin, acceptor of repentance, severe in punishment, owner of abundance. There is no deity except Him; to Him is the destination.” [40:1-2])
Saying “la ilaha ill Allah wahdahu la sharika lah, lahul mulku wa lahul hamdu wa huwa `ala kulli shay’in qadir” (there is nothing worthy of worship except Allah, He has no partner, His is the Dominion and Praise, and He is able to do all things) a hundred times.
The most beneficial form of protection from Shaytan: abundance of remembrance of Allah, the Exalted.