Followers

Thursday, May 9, 2013

SIMU HIZIII...TUSIPOZITUMIA VIZURI TUTAKUJA JUTAAA......

www.fahadahm.blogspot.com
Tuwe Macho na 'Ofa Za Maangamizi'



Wakati Ibilisi alipochukua ahadi kwamba atawapotosha wanaadamu, hakuwa na masikhara kwa kauli hii na aliazimia kwa kutekeleza hilo. Ndani ya karne hii inayoitwa ya sayansi na teknolojia, amerahisishiwa mambo kabisa katika kuwapotosha wanaadamu hadi unaweza kusema kwamba hakuna hata mmoja aliye nje ya wasajiliwa wa daftari la Ibilisi!

Wala hakuna kipya ambacho kimerahisisha wanaadamu kupotea ulimwengu wa leo kama zilivyo simu. Tumeshaelezana mengi katika makala zilizopita, lakini kwa haya maovu yanayoendelea kufanywa yabidi tukumbushane tena kwa namna jamii ya Waislamu inavyozidi kupotoka. 'Asaa huwenda tukatanabahi ukweli wa upande wa pili wa shilingi.

Kwa kiwango kikubwa matumizi ya simu yamepenya kwa kila rika: vijana na wazee, wake kwa waume, wagonjwa na wazima, matajiri na masikini, wote takribani ni wenye kutumia huduma hii. Tunapozungumzia kuhusu simu, tusirudi zama za mababu na mabibi zetu tukadhani ni zile za kukamata kwa mikono miwili, mmoja ukiwa ukishika cha kuzungumzia na mwengine cha kusikilizia. Hakika tunazungumzia hizi simu za mkononi maarufu kwa jina la mobile.

Kumekuwa na ushindani mkubwa katika mashirika ya simu hadi kusikia ya kwamba kuna huduma zinazokaribiana kuwa bure. Wenyewe wanatangaza ya kwamba kutakuwa na ofa usiku kucha kuzungumza bure. Lakini kabla ya kwenda mbali, tujiulize "kweli hii ni bure?" Simu unaihudumia kwa kuigharamia, bila ya kuigharamia huwezi kutumia ofa hizo. Halkadhalika ofa nyingi ni lazima ujisajili japo kwa kiwango cha chini ili uweze kutumia ofa hizo. Hapo ndio tunaamini ule msemo wa kimombo – There is no free lunch. Unapoalikwa chakula cha mchana, basi hiyo kuitikia dua'h ndicho ulichoitiwa. Dunia hii haina bure kabisa.

Cha kusikitisha zaidi ni wale vijana wa jinsia tofauti wanapokaa wakizungumza ndani ya simu hizi usiku mzima! Sio hivyo tu, bali Waumini wakiwa kwenye visimamo vya usiku wao hata habari hawana. Tabia hii ilishtadi zaidi maeneo yetu katika mwezi mtukufu wa Ramadhaan. Kweli hili lina khayr na sisi Waislamu?

Kama utafuatilia kwa makini mazungumzo hayo ya simu za bure, basi utakuta kwamba asilimia kubwa ni ya usengenyaji, uongo, uzushi, udaku na baya zaidi ndio mlango wa zinaa. Masaa matano Muislamu mzima kagandia simu, kinachofanywa hapo si chengine isipokuwa ni kuzikata dakika za uhai bure bure. Yareti angepitia aya za Qur-aan na kuzijua maana yake ili kuzifanyia kazi angepata fadhila kubwa. Wenye akili tu ndio wanaelewa umuhimu wa kuchunga muda.

Hii tabia ya kujiingiza kichwa na miguu katika ofa inatudhihirishia kwamba wanaadamu wote wapo kwenye khasara. Isipokuwa tu kwa Waumini, ambao wanachunga muda wao katika kutenda mema kupitia simu hizo kwa kuusiana juu ya kushikamana na subira pamoja na katika kutenda haki. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema ndani ya Kitabu Kitukufu:
{{Naapa kwa zama (zako ewe Nabii Muhammad).}}

{{Kuwa binaadamu yuko katika hasara.}}

{{Isipokuwa wale walioamini na wakafanya vitendo vizuri, na wakausiana (kufuata) haki na wakausiana (kushikamana) na subira (kustahamiliana).}}

[Suratul-'Asr: 1 – 3]

Kama Muislamu ajijua ni dhaifu wa nafsi yake, basi ajizuilie kujiunga katika ofa hizo. Kwani itakuwa ndio sababu ya kuangamia kwake na jamii inayomzunguka.
Waislamu tuchunge muda wetu hapa duniani kwa kufuata yale yenye kuleta natiyjah (matokeo) ya khayr na salama. Tuwe ni wenye kuchunguza na kuwa waangalifu kabla ya kufanya maamuzi ya kutumia huduma hizi. Haya mambo sio bure wala hayajaanzishwa kuzipatia nchi utajiri wa mali tu, bali lengo kuu ni kudumaza harakati za Waislamu makundi kwa makundi.

Tunamuomba Allaah Mwingi wa Rahmah na Mwenye kurehemu Atujaalie tawfiyq ya kutenda mema, kuusiana haki na subira. Aamiyn!

No comments:

Post a Comment

10 Ways of Protection from Shaytan:

Imam Ibn ul Qayyim

Seeking refuge with Allah from Shaytan. Allah the Most High said, “And if there comes to you from Satan an evil suggestion, then seek refuge in Allah. Indeed, He is the Hearing, the Knowing.” [41:36]

Recitation of the two soorahs al-Falaq and an-Nas, as they have wondrous effect in seeking refuge with Allah from evil, weakening Shaytan and protection from him. This is why the Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said: “No person seeks refuge with anything like the Mu`awwidhatayn (soorahs al-Falaq and an-Nas)”. [an-Nasaa’i, 5337]

Recitation of Ayat al-Kursi (2:255).

Recitation of soorah al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “The house in which al-Baqarah is recited is not approached by Shaytan.” [Muslim]

The final part of al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “Whoever recites the two last verses of al-Baqarah at night they will suffice him.” [Muslim]

Recitation of the beginning of soorah Mu’min (Ghafir), until His saying, “wa ilayhi-l-maseer” (to Him is the destination). (i.e. “Ha. Meem. The revelation of the Book is from Allah, the Exalted in Might, the Knowing, the forgiver of sin, acceptor of repentance, severe in punishment, owner of abundance. There is no deity except Him; to Him is the destination.” [40:1-2])

Saying “la ilaha ill Allah wahdahu la sharika lah, lahul mulku wa lahul hamdu wa huwa `ala kulli shay’in qadir” (there is nothing worthy of worship except Allah, He has no partner, His is the Dominion and Praise, and He is able to do all things) a hundred times.

The most beneficial form of protection from Shaytan: abundance of remembrance of Allah, the Exalted.

احمد محب الدين الأخبار جديد/احب الله ورسوله

حبّ الرسول صلّى الله عليه وسلّم

قال عليه والصلاة والسلام <<من أحبّ سنّتي فقد أحبّني ومن أحبني كان معي في الجنة>>وقال تعالى<<قل إن كنتم تحبّون الله فاتبعوني يحبب كم الله و يغفر ذنوبكم>>

Popular Posts