Followers

Thursday, February 6, 2014

Haki Za Mume Na Mke


Mwanamume na mwanamke wanapofunga ndoa inawapasa wote watambue desturi, mwendo mwema na adabu katika maisha hayo ya mke na mume ili ndoa yao iwe katika mipaka ya sharia ya Dini yao. Zifuatazo ni haki za baina ya mume na mke kama ilivyo katika Qur-aan na Sunnah.
Allaah سبحانه وتعالى Anasema:
((وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ وَاللّهُ عَزِيزٌ حَكُيمٌ))
“Nao wanawake wanayo haki kwa Shari’ah kama ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Na Allaah ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.” [Al-Baqara 2: 228]
Aayah hii tukufu inatufundisha wazi kuwa mume na mke wote wana haki baina yao. Lakini aya imezidi kuonyesha kuwa mume haki zake zimezidi kwa daraja ambazo anatakiwa kuzipata kutoka kwa mke wake.
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم عند ما وقف في عرفة في حجة والوداع :(( يآ أيها الناس إن لنسائكم عليكم حقاً ولكم عليهن حق))أبو داود
Mtume صلى الله عليه وسلم alisema aliposimama ‘Arafah katika hutuba yake ya mwisho ya Hajj: “Ee nyie watu, hakika nyinyi mna haki juu ya wake zenu na wake zenu wana haki juu yenu.” [Abu Daawuud]
Baadhi ya haki hizo ziko sawa baina ya mume na mke na nyinginezo ziko tofauti baina yao.

HAKI ZA MUME NA MKE BAINA YAO
Zifuatazo ni haki ambazo zinawapasa wote wawili wazitimize baina yao:

1. Ukweli
Jambo hili linawabidi wote wawili walitimize baina yao, ili upatikane utulivu wa kuaminiana baina yao. Haiwapasi kudanganyana au kuhadaiyana katika mambo yao yote ya kimaisha ikiwa ni jambo kubwa au dogo likiwa la baina yao wawili au baina yao na watu wa nje.

2. Mapenzi na huruma baina yao
Mapenzi katika ndoa ni jambo muhimu kuweko kwani bila ya kuweko bila shaka ndoa itakuwa yenye upungufu na ikawa sio imara bali huenda ikavunjika kutokana na sababu ya upungufu huu wa mapenzi baina ya mume na mke. Kila mmoja awe na mapenzi ya dhati kwa mwenzake hata ipatikane raha ya nafsi na maridhio baina yao. Vile vile iwepo rahma baina yao kwa kuhurumiana katika mambo ya shida na dhiki hata iwe hadi kuwa mmoja wao anapofikiwa hali hii, basi mwenzie awe ndio kitulizo chake.
Allaah سبحانه وتعالى Amesema:
((وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَة ًإِنَّ فِي ذَلِكَ لَآ يَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ))
“Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.” [Ar-Ruum 30: 21]

3. Uaminifu
Kila mmoja wao awe muaminifu kwa mwenzake hata isiwekodhana mbaya au shaka baina yao. Mke na mume wanapotekeleza haki kama hii baina yao huwafikisha kupindukia uhusiano wao ukawa kuliko uhusiano wa ndugu.
Kila mmoja atambue kuwa yeye ni kioo na nafsi ya mwenzake, kwa hivyo vipi mtu asiweze kuwa muaminifu wa nafsi yake?

4. Tabia njema
Wawe na tabia njema na upole katika kauli na matendo ili iwepo heshima baina yao kama Alivyosema Allaah
((وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ))
“Na kaeni nao kwa wema” [An-Nisaa 4: 19]
Kauli hii ya Allaah سبحانه وتعالى imekamilishwa na kauli ya Mtumeصلى الله عليه وسلم
“Nakuusieni kuwafanyia wema wanawake.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

5. Kuhifadhiana siri na aibu
Haiwapasi wote kutoleana siri zao au kutoa aibu zao kwa watu wengine, bali kila mmoja ahifadhi heshima ya mwenziwe kwa watu wa nje.
Mtume صلى الله عليه وسلم kasema: “Watu watakaokuwa katika hali mbaya kabisa mbele ya Allaah سبحانه وتعالى siku ya Qiyaamah ni mwanamme anaekwenda kwa mke wake na mke kwa mume wake kisha akapita kutoa siri yake.” [Muslim]

Hizo kwa ujumla ni desturi na haki ambazo zinapaswa kutekelezwa sawa sawa baina ya mume na mke kwani walikwishachukua ahadi nzito ya Allaah:
((وَكَيْفَ تَأْخُذُونَهُ وَقَدْ أَفْضَى بَعْضُكُمْ إِلَى بَعْضٍ وَأَخَذْنَ مِنكُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا))
“Na mtachukuaje na ilhali mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti?” [An-Nisaa 4: 20]
Vile vile hivi itakuwa wametimiza kumtii Allaah سبحانه وتعالى katika kauli Yake:
((وَلاَ تَنسَوُاْ الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ إِنَّ اللّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ))
“Wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Allaah Anayaona mnayoyatenda.” [Baqarah 2: 237]
Zifuatazo ni haki ambazo zinampasa mmojawao azitimize kwa Mwenzake:

HAKI ZA MKE KUTOKA KWA MUME

1. Ni wajibu wa mume kumlisha mkewe anapokula yeye, kumvisha anapovaa yeye na kumtimizia mahitajo yake ya nyumbani.

2. Mume vile vile ni wajibu wake kumtia adabu mke anapohisi uasi wa mke wake kama Alivyoamrisha Allaahسبحانه وتعالى katika kauli ifuatayo:
 ((وَاللاَّتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلاَ تَبْغُواْ عَلَيْهِنَّ سَبِيلاً إِنَّ اللّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا))
“Na ambao mnachelea kutoka katika utiifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikutiini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Allaah ndiye aliye juu na Mkuu.” [An-Nisaa 4: 34]
Aayah hii inataka maelezo kidogo kwani baadhi wa wanaume wameifahamu sivyo Allaah سبحانه وتعالى Aliposema: “muwahame katika malazi na wapigeni.”
Ibn ‘Abbaas na wengineo wamesema kuwa Aayah imemaanisha kupiga mpigo usio mkali (yaani mpigo hafifu) Al-Hasan Al- Baswriy kasema kuwa ina maana mpigo usio wa nguvu.
Ma’ulamaa wameelezea maana hasa ya kauli hii kwamba inamaanisha:

a) Kwanza mume amnasihi mkewe bila ya kumshutumu au kumuonea au kumtia aibu kwa watu. Atakapomtii hapo basi yawe yamekwisha.

b) Atakapoendelea kutokumtii mume wake basi awe mbali nae kitandani, yaani asiwe analala nae kwa muda hivi wala asiseme nae mpakamke ahisi vibaya ajue kuwa kweli mumewe kakasirika nae, Pindi mke akikubali makosa yake basi yawe vile vile yamekwisha warudie hali yao kama kawaida.

c) Kisha tena ikiwa bado mke hana utiifu, hapa sasa mume anaweza kumpiga mkewe. Lakini sio kumpiga kwa nguvu kama walivyofahamu waume wengine bali kama alivyotuelezea Mtume صلى الله عليه وسلم katika hadithi ifuatayo:
في صحيح مسلم عن جابر عن النبي صلى الله عليه وسلم : أنه قال في حجة الوداع: واتقوا الله في النساء فإنهن عندكم عوان ولكم عليهن ألا يوطئنفرشكم أحدا تكرهونه فإن فعلن ذلك فاضربوهن ضربا غير مبرح ولهن عليكم رزقهن وكسوتهن بالمعروف.
Imepokelewa na Muslim kutoka kwa Jaabir kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم kasema katika Hijja ya kuaga: “Mcheni Allaah kwa wanawake kwani wao ni wasaidizi wenu. Mnayo haki juu yao kuwa wasimuruhusu mtu msiyempenda kukanyaga zulia lenu. (kuingia katika nyumba yao) Lakini wakifanya hivyo, mnaruhusiwa kuwatia adabu ndogo. Wao wana haki kwenu kwamba muwatimizie matumizi yao na nguo kwa njia ya kuridhisha.”

3. Ni wajib wake mume kumpa mafundisho ya dini mke wake anayoyahitaji kama mke bado hakuwa na elimu ya dini yake. Ikiwa yeye mwenyewe mume hawezi basi amruhusu mkewe kuhudhuria madarasa ili apate elimu ya dini yake kwani ni muhimu kwake kuijua kutahirisha nafsi yake na kuweza kujirekebisha yale mabaya yanayokatazwa ili ajieupushe yeye na aila yake yote na moto kama alivyosema Allaah سبحانه وتعالى:
 ((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا))
“Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto.” [At Tahriym 66: 6]

4. Ni wajibu wake mume kumrekebisha mkewe anapokosea kufuata sharia za dini yake kama kuhakikisha mavazi ya stara na kuitimiza hijaab, vile vile asimwachie kuchanganyika na wanaume isipokuwa wale waliokuwa kaharimishwa nao.

5. Ni wajibu wake kumhifadhi kwa kila njia. Mume awe ndio mlinzi wake na mwenye majukumu kwake katika mambo yake yote kama Alivyosema Allaah سبحانه وتعالى
((الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاء))
“Wanaume ni wasimamizi wa wanawake” [An-Nisaa 4: 34]
Mtume صلى الله عليه وسلم kasema: “Mwanamme ni mchunga (msimamizi) wa nyumbani kwake na ataulizwa kuhusu uchungaji (usimamizi) wake.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

6. Ikiwa mume ana mke zaidi ya mmoja, inampasa afanye uadilifu baina ya hao wake katika matumizi yao ya chakula, nguo, maskani na kadhalika. Allaah سبحانه وتعالى kakataza kutokuadilisha kwa kusema:

 ((فَإِنْ خِف ْتُمْ أَلاَّ تَعْدِلُواْ فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ذَلِكَ أَدْنَى أَلاَّ تَعُولُواْ))
“Na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi (oeni) mmoja tu, au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea kutokufanya jeuri.” [An-Nisaa 4: 3]
Juu ya hivyo Mtume صلى الله عليه وسلم aliusia kuwa wanawake watendewe mema kama alivyosema
“Mbora wenu ni yule Aliye mbora kwa familia yake na mimi ni mbora kabisa kwa familia yangu.” [At-Twabaraaniy]

HAKI ZA MUME KUTOKA KWA MKE

1. Mke ajue umuhimu wa kumtii mume wake kuwa ni jambo muhimu na kutokumtii ni jambo la hatari kwani hadithi inasema:
((لَوْ كُنْتُ آمِراً أَحَداً أَنْ يَسْجُدَ لأِحَدٍ لأَمَرْتُ الْمَرْأَةَ أَنْ تَسْجُدَ لِزَوْجِهَا مِنْ عِظَمِ حَقَّهِ عَلَيْهاَ))
Mtume صلى الله عليه وسلم kasema: “Kama ningeliweza kumuamrisha mtu amsujudie binaadamu mwenzake, ningeliamrisha mwanamke amsujudie mume wake kwa jinsi haki ya mume ilivyo tukufu kwa mke wake.” [Tuhfat Al-Ahwadhi 4.323 kutoka Tafsiyr ya Ibn Kathiyr]

2. Mke inampasa kumtimizia haja ya mumewe wakati wowote anapomhitajia kujimai naye, kwani kuna hatari kwa kutokumtii mumewe katika jambo hili kama ifuatavyo:
((إذا دَعَا الرَّجُلُ امْرَأتَهُ إِلىَ فِرَاشِهِ فَأَبَتْ عَلَيْه لَعَنَتْهَا الْمَلائِكَةُ حَتَّى تُصْبِحَ))
“Mume atakapomwita mkewe kitandani na akikataa mke, basi malaika watakuwa wanamlaani huyo mke mpaka asubuhi” [Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy]

3. Kumhudumia mumewe kwa upole (yaani bila ya kujikalifisha zaidi ya uwezo wake)

4. Haimpasi mke kutoa sadaka kitu chochote bila idhini ya mumewe. Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم
((قال صلي الله عليه وسلم ” لا تنفق المرأة من بيتها شيئا إلا بإذن زوجها قالوا يا رسول الله ولا الطعام قال ذلك من أفضل أموالن))ا صحيح ابن ماجه – (حديث حسن الألباني)
Asitoe sadaka mwanamke kitu chochote kutoka nyumbani ila kwa idhini ya mumewe. Wakasema ewe Mjumbe wa Allaah hata chakula? Kasema hicho ni mali bora yetu. [Hadiyth imepokelewa na Ibn Maajah na Shaykh Al-Albaaniy kasema ni ‘Hasan’.]
Ama mwanamke anayo haki kutoa sadaka katika kipato chake mwenyewe kisicho cha mumewe.
Katika Hadiyth nyingine sahihi inatujulisha kuwa mwanamke anaweza kutoa sadaka ikiwa anatambua kuwa hatoghadhibikiwa na mumewe.
((عن همام قال سمعت أبا هريرة رضي اللهم عنهم عن النبي صلى اللهم عليه وسلم قال إذا أنفقت المرأة من كسب زوجها عن غير أمره فله نصف أجره)) - البخاري
Kutoka kwa Hamaam kasema: Nimemsikia Abu Hurayrah kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم kasema: Mwanamke akitoa sadaka kutoka katika kipato cha mumewe bila ya amri yake basi na yeye atapata thawabu nusu yake.” [Al-Bukhaariy]

5. Haimpasi mwanamke kutoka nyumbani kwake bila ya idhini ya mumewe (hata kwenda kwa wazazi wake)

6. Haimpasi mwanamke kumfanyia ujeuri, ufedhuli au usafihi mumewe
(عن عبد الرحمن ابن عوف قال قال رسول الله صلى اللهم عليه وسلم إذا صلت المرأة خمسها وصامت شهرها وحفظت فرجها وأطاعت زوجها قيل لها ادخلي الجنة من أي أبواب الجنة شئت) صحيح الترغيب
“Kutoka kwa Abdur-Rahman Ibn ‘Awf kasema: Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم: Atakaposwali mwanamke Swalah zake tano, akafunga mwezi wake (wa Ramadhaan), akahifadhi sehemu zake za siri (asifanye uzinifu), akamtii mume wake, ataambiwa ingia peponi kupitia mlango wowote autakao.”[Swahiyh at-Targhiyb]

Bila ya shaka baada ya kutimiza haki hizi, ndoa itakuwa yenye kudumu bila ya kuwa na matatizo makubwa ya kuiharibu au kuivunja.


Please don't scroll down without Typing

 "Ameen", your Ameen is powerful.!!
Oh! Allah grant me a spouse who:
will be the garment for my soul.
who will satisfy half of my deen.

who will be righteous and on Allah's path.
who will remind me to pray.
who earns money and things from halaal sources.
who always refer to Qur'an and Hadith.
who uses Sunnah as his/her moral guide.
who is always thankful and appreciate Allah for the man/woman at his/her side.
who always be conscious of his/her anger.
who often fasts and prays.
who is sensitive and charitable.
who will honour and protect me.
who can guide me in this temporary life.
who loves me when I am with him/her, but still has me in his/her heart and on his/her mind when I am not with him/her. i make this dua on behalf of me and u all may ALLAH swt accept it from me O our Sustainer! Grant that our spouses and our offspring be a joy to our eyes, [56] and cause us to be foremost among those who are conscious of Thee!”
Share and say AAmeeen ya ALLAH

TIZAMA PICHA

TIZAMA PICHA: Mtoto mdogo Gerezani, Wako wapi watetezi wa haki za Binaadam!?
Uadui wa Serikali ya kibaraka ya Kenya dhidi ya waislamu umefikia kiwango cha juu kabisa ambapo mataifa yanayojitetea kwa kuchunga haki za kibinaadamu hujifagharisha kuzichunga haki hizo kwa ubaguzi mkubwa sana.
Miaka ya nyuma Marekani ambayo ndio taifa iliyokuwa ikiaminika lenye mashirika mengi ya kutetea haki za wanyonge na waliodhulumiwa lakini tangu kwanza kwa vita dhidi ya "Ugaidi (Uislamu) hiyo limekuja kuonekana wazi kuwa ni Propaganda za kuwadanganya na siasa za nje ya taifa hilo ya kuwahadaa mataifa inayowatumia kwa ubepari.
Itakumbukwa na kamwe tarehe haitoweza kusahaulika mamia ya damu za watoto iliyoimwaga Marekani ilipofanya uvamizi katika Ardhi ya Waislamu wa Afghanistaan na Iraq na kuwaua watoto wasio na hatia kwa kisingizio cha kupambana na Ugaidi/Uislamu.
Jinai za mataifa hayo dhidi ya waislamu ni mengi na laiti kama tutaanza kuangazia litakuja kuwa ni mlolongo mrefu wa makala isiyo na kikomo kinachoelezea miiili ya watoto wa Kislamu waliodhulumiwa kwanzia Mashariki ya kati,Asia,hadi kufikia pembe ya Afrika ambayo Kenya imejihusisha kwa namna mmoja au nyingine kuwaua watoto wa kislamu wa Somalia kwa kutumia ndege za Kijeshi kusini mwa Ardhi ya Waislamu wa Somalia.
Lengo hapo ni kuyabainisha wenye haki si waislamu au watoto wa Kislamu au hata wanawake bali walio haki zaidi kwa mataifa ya Kikafiri ni Watoto wao na watu wao wana haki zaidi kuliko wa kwetu waislamu wanaoishi mataifa yao,na wakikuona wewe una sura ya Kislamu basi kwao ni Adui mkubwa hata akiwa mtoto aliyopo msikitini.
Siku ya Jumapili ambapo wanajeshi wa Kenya kwa kushrikiana na Polisi wa nchi hiyo waliingia katika Msikiti mmoja uliopo mitaa ya Majengo Maarufu Masjid Mussa,na kwanza kufanya unyama na kuwapa vipigo visyo weza kusahaulika kwa walioupata na wasioupata maumivu hayo.
Ni kawaida ya waislamu wakienda Msikitini huwabebea na kuwachukua watoto wao kwa lengo la kuwafundisha maadili iliyo mema kwa watoto wao,Polisi baada ya kumwua Baba wa mwenye mtoto walimkamata mtoto na kumsweka Gerezani bila huruma ambapo Baadhi ya wanasiasa,wataalamu wa kislamu imewachukiza kitendo cha kufungwa mtoto mdogo hata miaka miwili bado kufikisha.
Kitendo cha Polisi na wanajeshi imedhihirika wazi kwa wasio ujua malengo na Mipango yao kuwa lengo kuu ni Uislamu na kuwaua waislamu na sheria za kuwaua waislaam ilishawahi kupitishwa na walioupitisha baadhi yao wamo wabunge wanaojiita wao ni Waislamu ambapo leo hii wanaijutia. Tafadhali Share.
Tafadhali Usisahau Kushare Click Share Hapa Chini.
PICHANI: Waislamu waliodhulumiwa wakiwa Gerezani na Mtoto-
anaedaiwa kufungwa kwa kuhatarisha Usalama wa Taifa nchini Kenya. لاحول ولاقوّة إلابلاالله
اللهم انصر المسلمون والمسلمات

Valentine Day (Siku Ya Wapendanao) Na Hukumu Ya Kuisherehekea


BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu was Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa ‘Aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa Ba’ad,
Allaah سبحانه وتعالى Ametuchagulia dini ya Kiislamu ambayo ndio dini ya haki na Hatokubali dini yoyote nyingine kama Anavyosema:
((وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الإِسْلاَمِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ))
((Na anayetafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasirika)) [Al-'Imraan:85]
Na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ametuambia kuwa kutakua na makundi katika ummah wake ambao watawafuata maadui wa Allaah سبحانه وتعالى katika desturi na mila zao kama ifuatavyo:
((ستتبعون سنن من كان قبلكم شبراً بشبر وذراعاً بذراع حتى لو دخلوا جحر ضب لدخلتموه)) قالوا: أتراهم اليهود والنصارى؟ قال: ((فمن إذن؟)) البخاري ومسلم
 ((Mtafuata nyendo za wale waliokuja kabla yenu hatua kwa hatua mpaka itafika hadi wakiingia katika shimo la kenge, na nyinyi mtaingia pia)) Wakasema (Maswahaba): Ewe Mtume! Je, unamaanisha Mayahudi na Manaswara? Akasema: ((Hivyo nani basi mwengine?)) Al-Bukhariy na Muslim
Maneno hayo aliyoyasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hakika yamesadikika kwani tunaona jinsi gani Waislamu siku hizi wanavyoigiza mila, desturi na tabia za makafiri na kuzisherehekea kama mfano siku hii inayoitwa ‘Valentine day’ (Siku ya Wapendanao).
Na baya zaidi na la kusikitisha sana ni kwamba sherehe hizi zinaenezwa katika njia mbali mbali za mawasiliano kama kutumiana kadi, barua pepe (e-mail), salamu katika simu za mkono. Hakika fitna hii humfanya Muislamu aharibu ‘Aqiydah (Iymaan) yake kwa kudhani kuwa anafanya jambo la kawaida na hali ni jambo lisilo katika sheria ya dini yetu bali ni shirki kubwa na upotofu wa kufuata wanayoamini makafiri.


Historia Ya Sherehe Ya Siku Ya Valentine
Sherehe hii ya wapendanao ni sherehe ya wapagani wa Kirumi wakati dini yao ya upagani ilikuwa ni dini iliyotapakaa kwa Warumi karne zaidi ya kumi na saba zilizopita. Na fikra zao ilikuwa ni kuelezea hisia ya ‘mapenzi ya kiroho’
Kulikuwa na visasili (uongo) zilizohusishwa na sherehe hii ya upagani ya Warumi ambao umeendelea kutoka warithi wa Kikiristo. Miongoni mwa uongo huo ni kuamini kwao Warumi kuwa Romulus, aliyevumbua Rome, alinyonyeshwa siku moja na mbwa mwitu mwanamke, hivyo akampa nguvu na hikma.
Warumi walikuwa wakisherehekea tukio hili katikati ya Februari kila mwaka kwa kufanya sherehe kubwa. Na mojawapo ya tambiko katika sherehe hii ni kuchinja mbwa au mbuzi. Vijana wawili wenye nguvu hujipaka damu ya mbwa au ya mbuzi katika miili yao, kisha huiosha damu hiyo kwa maziwa. Baada ya hapo, watu hufanya gwaride wakiwa vijana hawa wawilii wako mbele wakiongoza gwaride iliyokuwa ikitembea barabarani. Vijana hao wawili walikuwa wakichukua vipande vya ngozi ambavyo waliwapigia watu wanaowavuka. Wanawake wa kirumi walikuwa wakipokea mapigo hayo wakiamini kuwa yatawahifadhi na kutibu utasa.


Kuungamana Baina Mtakatifu Valentine (Saint Valentine) Na Sherehe Hii
Mtakatifu Valentine (Saint Valentine) ni jina waliopewa mashujaa wawili wakongwe waliokufa ambao ni wana wa kanisa la kikiristo. Inasemekena kwamba walikuwa ni wawili au mmoja tu. Huyo mmoja alikufa Rome kutokana na mateso ya kiongozi wa Kigothi aliyeitwa Claudius. Kanisa la Saint Valentine lilijengwa kwa ajili ya kudumisha kumbukumbu yake.
Warumi walipoingia ukristo, wakaendelea kusherehekea sikukuu ya wapendanao (valentine day) lakini wakabadilisha kutoka fikra ya upagani ya ‘mapenzi ya kiroho’ (spiritual love) na kuleta fikra nyingine iliyojulikana kama ni ‘mapenzi ya mashujaa’ yaliyowakilishwa na Saint Valentine ambaye aliuliwa kwa ajili ya kutetea mapenzi na amani. Vile vile ikajulikana ni sikukuu ya wapenzi, na Saint Valentine alifanywa kuwa ni mlezi wa mapenzi ya mtakatifu.
Miongoni mwa imani yao inayoambatana na sherehe hii ni kwamba majina ya wasichana waliofika umri wa kuolewa yaliandikwa katika vikaratasi vidogo vilivyokunjwa mviringo kisha vikawekwa katika chombo juu ya meza. Kisha wavulana waliotaka kuoa waliitwa na kila mmoja huchagua karatasi moja ikiwa na jina la msichana. Kisha hujiambatanisha naye huyo msichana aliyempata kutokana na kura hiyo aliyochagua kwa muda wa mwaka ili wajuane vizuri kisha tena hufunga ndoa, au kama hawakuelewana hurudia tena kufanya kura inapofika siku hiyo mwaka unaofatia.
Vile vile imesemekana kwamba chanzo cha sikukuu hii, ni kwamba warumi walipokuwa wakristo baada ya ukristo kutapakaa, Mfalme wa Kirumi Claudius II alitoa hukumu katika karne ya tatu kwamba askari wasioe kwa sababu kuoa kwao kutawashughulisha na vita walivyokuwa wakipigana. Hukumu hiyo ilipingwa na Saint Valentine ambaye alianzisha kuozesha maaskari kwa siri. Alipokuja kujua mfalme, alimfunga jela na akamhukumu kuuliwa. Huko jela akapendana na mtoto wa mkuu wa jela, lakini ikawa ni siri kwani kutokana na sheria ya ukristo, mapadri na makasisi wameharamishwa kuoa au kupenda.

Hata hivyo alipewa heshima yake na wakristo kwa sababu ya kushikilia na kujikita imara katika ukristo wakati mfalme alipotaka kumsamehe kwa sharti aache ukristo na kuabudu miungu ya Kirumi ili awe msiri wake na awe mkwe wake. Lakini Saint Valentine alikataa ahadi hiyo na akapendelea ukristo, kwa hiyo akauliwa siku ya tarehe 14 Februari 270 CE. Ndio ikaitwa siku hii kwa jina la huyo mtakatifu (Valentine).
Papa (Pope) naye akaifanya siku hiyo ya kufa Saint Valentine tarehe 14 Februari 270 CE kuwa ni sikukuu ya mapenzi. Na ni nani alikuwa Papa huyo? Ni Askofu mkuu wa kanisa la ‘universal church’, ambaye ni mrithi wa mtakatifu Peter.
Ndugu Waislamu tazameni vipi huyo askofu anavyohusika katika kuadhimisha sikukuu hii ambayo ni uzushi katika dini yao ya Kikiristo. Hii itukumbushe kauli ya Allaah سبحانه وتعالى
((اتَّخَذُواْ أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللّهِ))
((Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu)) [At-Tawbah: 31]


Matendo Yanayotakiwa Kujiepusha Nayo Ambayo Yanayofanyika Katika Sikukuu Hii
 Kuonyeshana bashasha na furaha kama ilivyo katika sikukuu zao nyingine.

 Kupeana mawaridi mekundu (Red Roses) ambayo ni alama ya kuelezea mapenzi, ‘mapenzi ya kiroho’ ya wapagani au ‘mapenzi’ ya Wakristo. Hivyo inajulikana kuwa ni ‘Sikukuu Ya Wapendanao’.

 Kupelekeana kadi. Na kadi nyingine zina picha za ‘mungu wa mapenzi wa kirumi’ ambaye ana mbawa mbili, akiwa amekamata upinde na mshale. Huyu ndio mungu wa mapenzi wa wapagani warumi. Shirk iliyoje hii ndugu Waislamu?

 Kubadilishana maneno ya mapenzi na matamanio katika kadi wanazopelekeana, yakiwa katika mfumo wa kimashairi, tenzi na sentensi fupi fupi. Kadi nyingine zina picha za kimzaha na maneno ya kuchekesha, na mara nyingi zina maneno ya kusema ‘Kuwa Valentine wangu’. Hii inaashiria maana ya kikiristo ya sikukuu hii baada ya kuwa asili yake ni kutokana na fikra za upagani.

 Katika nchi nyingi za kimagharibi, hufanyika sherehe siku hiyo ambayo kunakuweko kuchanganyika wanaume na wanawake, kuimba, na kucheza dansi. Na wengi wanapelekeana zawadi kama mawaridi, maboksi ya chokoleti kwa wake zao, marafiki na wanaowapenda.
Kutokana na maelezo yote hayo ya chanzo cha sikukuu hii, tunaona kwamba siku hiyo haina uhusiano wowote katika Uislamu, bali yana uhusiano na washirikina mapagani, hata wakristo katika dini yao nao pia ni uzushi, sasa itakuwaje sisi Waislamu tuwaigize kusherehekea?
Basi ndugu Waislamu tutambue kuwa jambo hili ni ovu mno, haimpasi Muislamu kuharibu ‘Aqiydah (iymaan) yake kwani kuna hatari kubwa kushiriki katika sherehe hii nayo ni kuingia katika kumshirikisha Allaah سبحانه وتعالى, na kama tunavyojua kuwa Allaah سبحانه وتعالى Hamsamehe mtu anayefanya shirki pindi akifariki bila ya kutubu kama ilivyo katika aya ifuatayo:
 ((إِنَّ اللّهَ لاَ يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَلِكَ لِمَن يَشَاء وَمَن يُشْرِكْ بِاللّهِ فَقَدِ افْتَرَى إِثْمًا عَظِيمًا))
((Hakika Mwenyezi Mungu Hasamehe kushirikishwa, na Husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa)) [An-Nisaa: 48]
Hivyo ni kuharamishwa na Pepo na kupata makazi ya moto, tunajikinga na Allaah kwa hayo.
((إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللّهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللّهُ عَلَيهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَار))
((Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu Atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na waliodhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru)) [Al-Maaidah: 72]
Tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى Atuepushe na kila aina ya shirk na Atuonyeshe yaliyo ya haki tuyafuate, na yaliyo ya batili tujiepushe nayo na Atuajaalie ni miongoni mwa wale wanaosikiliza kauli (nyingi) wakafuata zile zilizo njema. Aamiyn

AARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Makafiri hao waingia na viato muskitini

Kumb: 03/1435 02 Rabiul-Thani 1435 Hijri 03-02-2014
Uvamizi Wa Polisi Msikiti Musa Ni Ukiukwaji Wa Haki Msingi Za Waislamu!
Harakati ya Kiislamu ya Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki inakashifu vikali kitendo cha kiuadui cha vikosi vya polisi kuingia ndani ya msikiti wa Musa Majengo Mombasa na kushambulia waumini kwa risasi. Tumehuzunishwa sana na uovu huu uliopelekea mauaji ya baadhi ya Waislamu na majeruhi wengi na wengine kutiwa korokoni. Twamuomba Mwenyezi Mungu awarehemu maiti hao na kuwapa subra familia zote zilikumbwa na msiba huu. Baada ya haya twapenda kusema yafuatwayo:
Hakuna uhalali wowote wa vikosi vya polisi kuzingira msikiti na kuanza kuwamiminia risasi waumini waliokongamana ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu kwa madai eti ni kongamano la kigaidi linalotishia usalama. Swali la kuulizwa ni kwanini wahubiri wa kikristo walipozungumza hadharani kuomba serikali iwape makanisa yote bunduki za AK47 mbona hauwakufanywa lolote au angaa kuitwa magaidi au wenye misimamo mikali? Je matamshi yaliyoangaziwa na vyombo vya habari vikuu nchini mbona hayakuwa ni tishio kwa usalama?
Misemo; 'siasa kali','ugaidi' na 'misimamo mikali' ni kampeni ya kuuchafua Uislamu inayoongozwa na Marekani kote duniani kwa lengo la kuzuia kurudi kwa Uislamu katika kuongoza ulimwengu kama ilivyokuwa hapo awali ulipokuwa ukitekelezwa na dola yake ya Khilafah. Kwa kuwa dalili za kushindwa kwa mfumo wake wa kibepari ziko wazi kote duniani ikiwemo hapa Kenya kiasi cha kusabibisha njaa, maradhi, vita na mengineo. Amerika imejawa na uoga juu ya Uislamu na inatumia miito hii kama njia mojawapo ya kuupaka matope Uislamu. Na kama misemo hii ina maana ya kweli basi Marekani ndiye anastahiki hasa kupewa majina haya na ulimwengu wote utakuwa hauna wasiwasi juu ya hilo.
Kitendo cha kuuvamia msikiti na kuuzingira kwa masaa matatu na kuwadhalilisha Waislamu ni unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za Waislamu nchini Kenya na kimefichua wazi urongo wa miito ya kidemokrasia ya kwamba raia wana uhuru wa kuabudu na uhuru wa kujieleza.
Mwisho ni muhimu Waislamu kutahadhari wasijeingia kwenye mitego ya maadui kila wanapokumbwa na matatizo kama haya. Jukumu letu sio kuanza kutupiana lawama na kuanza kuchukiana. Huu ni wakati wa kuulingania Uislamu pasina na hamasa kwa sura yake kamili ili wasokuwa Waislamu wapate kuona Uislamu kuwa ndio mfumo bora ulio na suluhisho za kikweli pale utakapotabikishwa ndani ya dola yake ya Khilafah.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki.
Simu: +254 720597841 / +254 789 754 608
Pepe: abuhusna84@yahoo.com
Tovuti rasmi ya Hizb ut-Tahrir
www.hizb-ut-tahrir.org
Tovuti ya Afisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
www.hizb-ut-tahrir.info

Kitendo cha Serikali ya Kenya kuwaua Waislaam Msikitini ni kitendo cha Kigaidi"

waislamu wa Masjid Mussa

Kitendo cha kiuhalifu iliyofanywa na Serikali ya kibepari ya Kenya ya kuwaua waislaam waliokuwa msikitii bila hatia imelaaniwa vikali na baadhi ya waanaharakati nawasiasa wa Kislaam na waislaam wanaoishi nchini Kenya na ulimwengu kote.
Kwa upande wa Msemaji wa Polisi nchini Kenya kwa jeuri ameitetea uhalifu uliofanywa na Wanajeshi na Polisi ya kufanya mauaji ndani ya Msikiti mbali na kwenda wanajeshi na Polisi kunajisi msikiti wa Allah.
Gatiria Mboroki ambae ni mwanamke Msemaji wa Polisi nchini Kenya amesema Maaskari walifanya kazi yao iliyokuwa ya kuwaua waislaam aliyowatuhumu kuwa walikuwa na Silaha ndani ya Masjid Mussa.
"Upande wa Polisi walifanya kazi yao vizuri na hakuna kingine isipokuwa hao Maradicall ambao walipelekwa kwa Kortini",alisema Msemaji wa Kike wa Polisi nchini Kenya Gatiria Mboroki.
Alipoulizwa kuhusiana na kitendo kilichofanywa na Maaskari ya kuwaua na Kuingia Msikitini na viatu na ombi la Baraza la Maimu wa kuomba Radhi Polisi kwa kitendo hicho alijibu Msemaji huyo kwa ukali na dharau:-"haya wewe acha kuniuliza maneno ya Viongozi wa Kislaam,Polisi tulienda kufanya kazi yetu kulingana na Sheria ya Kenya ya kuwaua waislaam,mimi nimesema tumefanya kazi yetu kulingana na Sheria,wacha kuleta maneno
ya Dini kwa kazi ya Polisi!", Msemaji wa Polisi Gatiria Mboroki.


Wednesday, December 11, 2013

Kumuoa Mkristo Atakayesilimu Siku YA Ndoa


SWALI:

 Je inakubalika kumuoa Mkiristo atakaesilimu siku ya ndoa?



JIBU:
Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Hakuna tatizo lolote endapo atasilimu kidhati, Imepokewa kutoka kwa Anas amesema: Abu Twalha alipomuoa Ummu Sulaym, mahari yao ilikuwa ni kusilimu, Ummu Sulaym alisilimu mwanzo kabla ya Abu Twalha, alipomchumbia, akasema kwa hakika mimi nimeshasilimu, ikiwa utasilimu utanioa, akasilimu na ikawa kusilimu ndiyo mahari yao" (An-Nasaaiy 6/114).
Lakini Muislamu mwanamume awe makini na mwanamke mwenye kutaka kusilimu siku ya ndoa, isijekuwa ni mwenye kumdanganya akawa anasubiri siku hiyo wakati ameshatayrisha mambo ya harusi kisha amgeukie. Ikiwa hili ndilo sharti aliloliweka huyo mwanamke basi nasiha yetu ni kuwa uwe makini na ujaribu kuchunguza kwanza dhamira yake.

Na Allah Anajua zaidi
 

Mawasiliano Na Mchumba Baada Kuposa Na Kabla Ya Ndoa




SWALI:

INARUHUSIWA KUWASILIANA MARA KWA MARA NA MCHUMBA WAKO? KWA SIMU AMA BARUA AMA E-MAIL?
 




JIBU
Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allahu 'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Qiyaamah.
Ama kuhusu kuwasiliana baina ya mvulana aliyeposa na posa yake kukubaliwa na msichana na walii wake basi hakuna tatizo lolote ikiwa mawasiliano yao ni katika mipaka ya sheria. Hivyo, kumpigia simu hakuna ubaya ikiwa ni katika kuyapanga yale mambo ya ndoa yao na matayarisho yake. Ama ikiwa mawasiliano hayo yatakuwa nje ya misingi hiyo na kupelekea kuzungumza kuhusu mahusiano na mapenzi na mengine yasiyofaa, basi ni vizuri kujiepusha na mawasiliano hayo.
Mara nyingi mawasiliano ya karibu kabla ya ndoa, yameleta uharibifu mkubwa na madhara katika jamii na kusababisha posa nyingi kuharibika na hata vatu kutumbukia katika zinaa.
Mbali na mawasiliano hayo mvulana anaweza kwenda nyumbani kwa mchumba wake bora tu wasikae faragha wao peke yao katika mazungumzo. Inabidi awe pamoja nao maharimu wa msichana. Hii ni kwa sababu Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) amesema: “Hakai faragha mwanamume na mwanamke ila wa tatu wao ni shetani. Na hakika shetani hutembea katika mwili wa mwanaadamu kama itembeavyo damu”. Hii ni kuwa bado nyinyi hamjakuwa mume na mke, na mmoja kati yenu anaweza kuvunja ndoa hiyo baada ya kuwa mmekubaliana hapo awali. Mwanamume anaweza kusema basi hataki tena harusi au mwanamke kujibu kuwa hakuna tena harusi.
Ile desturi ya wachumba kuwa wanakwenda pamoja katika mabustani, sinema au kusafiri kabla ya kuoana si desturi ya Kiislamu. Na athari yake mara nyengine inakuwa mbaya kwani wanaweza kutumbukia katika maasi na kisha mwanamume akasema hataki tena harusi na binti huyo. Baada ya hapo wanaume wanakuwa wakimtweza binti kama yule na inakuwa ni vigumu kwake kutakiwa na mume mwengine.
Na Allah Anajua zaidi

Uzazi Wa Kupanga Unafaa?



SWALI:
Jee Sheikh kuna njia yoyote ya uzazi wa mpangilio ya kiislam na kama ipo ni njia gani?    Je, Sheikh kutumia condom kwa mke na mume ni vibaya?

JIBU:           
Sifa zote njema Anastahiki Allah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'Alayhi Wa Aalihi Wasallam)  na   Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'Anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Hakika ni kuwa njia za mpango wa uzazi zipo katika ulimwengu huu nyingine zikiwa zinakubalika na Uislamu na nyengine hazifai kutumika. Njia ambayo haifai kutumika ni ile ya kufunga kizazi milele (permanent) isipokuwa kwa haja kubwa ambayo inakubalika kisheria kama shida ya mama katika kuzaa na mfano wake.
Njia ambayo inayokubalika ni ile ya kutumia azl (coitus interuptus -kumwaga nje maji ya uzazi). Jaabir ibn ‘Abdillahi (Radhiya Allaahu 'Anhu) amesema: “Tulikuwa tukifanya azl ilhali Qur’ani ilikuwa ikiteremshwa, habari hii ilimfikia Mtume (Swalla Allahu 'Alayhi Wa Aalihi Wasallam) naye hakutukataza” (Al-Bukhaariy na Muslim).
Wanachuoni wameafikiana kuwa njia yoyote ya upangaji uzazi inakubalika isipokuwa ile ya kufunga kabisa kizazi. Na mtu anatakiwa atumie njia ambayo ni salama kwa mwenye kutumia kwa sababu zake za kibinafsi, lakini haifai kuwa ni sheria na kanuni ya dola.
Wanachuoni wametumia Qiyaas ya kwamba kwa kuwa azl ilikuwa inatumika kuzuia mbegu kufika kwenye uzao wa mama njia hizi nyengine za upangaji uzazi zinaruhusiwa kwa muda kwa kuafikiana baina ya mume na mke. Hivyo, kutumia condom inaruhusiwa. Kuhusu njia nyengine inabidi wanandoa wapate ushauri kwa daktari Muislamu mtaalamu, mcha Mungu ili ampatie njia muafaka na maumbile yake.
Tanbihi: Ieleweke kuwa njia nyingi za kutumia madawa na sindano zina madhara makubwa sana kwa binadamu, hivyo tuwe na tahadhari ya hali ya juu katika utumiaji wa vitu hivyo.
Kwa maelezo zaidi ingia katika kiungo kifuatacho :
Na Allah Anajua zaidi

Hukmu Ya Kusoma Vitabu Vya Mapenzi Na Tendo La Ndoa


SWALI:
JE KUSOMA VITABU VINAVYOZUNGUMZIA MASUALA YA MAPENZI NI SAHIHI? NA KAMA SI SAHIHI JE VYA KIDINI VINAVYOELEZEA MASUALA YA TENDO LA NDOA?


JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allahu 'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Qiyaamah.
Ama kusoma vitabu vinavyozungumzia masuala ya mapenzi havina tatizo ikiwa vitakuwa vinakwenda sambamba na mafundisho ya Uislamu. Hivyo, vikiwa na picha zenye kuonyesha mume na mke wakiwa uchi katika kufafanua au kueleza vitakuwa havifai kabisa. Au katika maelezo yake ikiwa vitakwenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu pia vitakuwa havifai.
Ama vitabu vilivyoandikwa na wanachuoni kwa kufuatana na maagizo ya Qur-aan na Sunnah hivyo ndivyo vinavyohitajiwa kusomwa ili tupate muongozo sahihi wa wana ndoa kufanya tendo la ndoa kwa njia zilizo sahihi. Ni muhimu kwa sababu    aghlabu wana ndoa wa Kiislamu huwa hawapati mafunzo hayo kiuwazi na wengi wanaona aibu kuuliza, kisha wanaishia kujinyima haki zao katika tendo la ndoa na huenda wakaingiwa na shauku ya kutafuta njia nyingine za kupata mafunzo hayo ambazo sio halali kama kutazama sinema za ngono n.k. Lakini watakapopata vitabu vyetu vya Kiislamu watapata mafunzo sahihi na khaswa yanayotokana na mafunzo ya dini yetu. 
Tutambue kuwa dini yetu haifichi haki, na hakuna aibu kuelezea mambo ya ndani ya ndoa yaliyo haki ili mafunzo hayo yawekwe wazi kwa Waislamu watambue yanayowapasa kutenda kihalali hata waweze kujitosheleza na starehe za kitendo cha ndoa, waweze kuimarisha ndoa zao na kujiepusha na vishawishi vya haramu. 
Kwa hakika vitabu hivi viko vingi katika lugha ya Kiarabu na kwa Kiswahili vimeanzwa kuandikwa kama kwa mfano Furaha ya Ndoa na Siri ya Unyumba na pia Zawadi kwa Wanandoa ambacho tayari kiko katika hii tovuti yenu kwenye kitengo cha vitabu, ingia hapa ukisome: ZAWADI KWA WANANDOA. Na chengine ambacho kimetafsiriwa ni Malezi ya Kijinsiya lakini bado kuchapishwa.
Na Allah Anajua zaidi
 

Hadithi Ya 01: Kila Kitendo Kwa Nia Yake




الحديث الأول
" إنما الأعمال بالنيات "
  عن أَمِيرِ المُؤمِنِينَ أَبي حَفْصٍ عُمَرَ بنِ الخطَّابِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ : سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ:   ((إِنَّما الأَعْمَالُ بالنِّيَّاتِ وإنَّما لكُلِّ امْرِىءٍ ما نَوَى، فَمَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ فَهِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ، ومَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ لِدُنْيا يُصِيبُها أو امْرأةٍ يَنْكِحُها فَهِجْرَتُهُ إلى ما هَاجَرَ إليه)).  
رَوَاهُ إِمَامَا الْمُحَدِّثِينَ أَبُو عَبْدِ اللهِ مُحَمَّدُ بنُ إِسْمَاعِيل بن إِبْرَاهِيم بن الْمُغِيرَة بن بَرْدِزبَه الْبُخَارِيُّ     وَأَبُو الْحُسَيْنِ مُسْلِمٌ بنُ الْحَجَّاج بن مُسْلِم الْقُشَيْرِيُّ النَّيْسَابُورِيُّ   رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا فِي "صَحِيحَيْهِمَا" اللذينِ هُمَا أَصَحُّ الْكُتُبِ الْمُصَنَّفَةِ.


HADITHI YA 1
KILA KITENDO KWA NIA YAKE
Kutoka kwa Amiri wa Waumuni, Abu Hafs 'Umar Ibn Al Khattaab رضى الله عنه ambaye alisema : Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyeezi  Mungu صلى الله
 عليه وسلم akisema:
Vitendo vinategemea (vinalipwa kwa) nia na kila mtu atapata kwa mujibu wa kile alichokusudia.  Kwa hivyo yule aliyehama  kwa ajili ya Allaah na Mtume wake, uhamaji wake ni kwa ajili ya Allaah na Mtume wake, na  yule ambae uhamaji wake ulikuwa ni kwa ajili ya manufaa ya kidunia au kwa ajili ya kumuoa mwanamke (Fulani)  uhamaji wake ulikuwa kwa kile kilichomuhamisha.
Imesimuliwa na Maimam wawili mabingwa wa hadithi Abu Abdalla Muhammad  Ibn Ismail Ibn Ibrahim Ibn Mughiyra Ibn Bardizbah Al Bukhari na Abu Al Husayn Muslim Ibn Al-Hajjaj Ibn Muslim Al Qushayri An-Naysaburi, katika sahihi zao mbili ambavyo ni vitabu vya kutegemewa.

Maana Ya Hadiyth Dhwa'iyf



Maulamaa wanasema kuwa: Hadiyth dhaifu ni ile isiyokuwa na sifa zinazokubalika. Na wengine wakasema kuwa Hadiyth dhaifu ni ile isiyostahiki kuitwa Sahihi wala Hasan (njema).
Zipo aina nyingi ya Hadiyth dhaifu zikiwemo:


Mursal:
Nazo ni zile zilizonyanyuliwa moja kwa moja kutoka kwa Taabi'iy mpaka kwa Mtume  صلى الله عليه وآله وسلم.  

Taabi'iy ni Muislamu aliyeishi wakati wa Maswahaba رضي الله عنهم   akawaona lakini hajamuona Mtume صلى الله عليه وآله وسلم.
Kwa mfano Tabi'iy aseme:
“Mtume wa Mwenyezi Mungu  صلى الله عليه وآله وسلم amesema…”
Wakati yeye hajawahi kuonana na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم.

Maulamaa wamekhitalifiana juu ya kuzitumia Hadiyth za aina hii katika makundi manne:
1.     Imaam Abu Haniyfah na Imaam Maalik na baadhi ya wanavyuoni wanasema kuwa Hadiyth hizi zinafaa kutumika.

2.     Imaam An-Nawawiy akieleza juu ya Jamhuur kubwa ya Maulamaa na pia akimnukuu Imaam Ash-Shaafi'iy anasema kuwa Hadiyth za aina hii zinaweza kutumika kama ni hoja lakini si hoja ya moja kwa moja (ya kutegemewa).

3.     Imaam Muslim anasema: “Hadiyth Mursal kwetu sisi na kwa wengi kati ya wanavyuoni si hoja hata kidogo.”

4.     Wengine wakasema kuwa inaweza kuwa hoja pale tu ikiwa imepokelewa kutoka kwa Tabi'iy mkubwa, kisha Hadiyth hiyo iwe imefanyiwa kazi na Swahaba yeyote au na wanavyuoni wengi.


Munqatwi'i:
Hizi ni zile Hadiyth zilizokatika Isnadi zake, yote sawa kukatika huko kuwe mwanzo au mwisho wa majina ya wapokezi


Al-Mudallas:
Nazo ni zile Hadiyth ambazo muelezaji aeleze kuwa amehadithiwa na mtu aliyeishi katika zama moja kisha ikathibiti kuwa hawajapata kuonana. Au ahadithie kama kwamba amehadithiwa na mtu huyo wakati ukweli ni kuwa hakuhadithiwa na mtu huyo, kwa mfano aseme:
“Amenihadithia fulani.” Au: “Nilimsikia fulani.” Wakati ingekuwa sahihi kama angesema:
“Amesema fulani.” Au: “Kutoka kwa fulani.”

Maulamaa wanasema kuwa Mudallis (muelezaji wa Hadiyth hizi) hazikubaliwi riwaya zake hata kama aliwahi mara moja tu katika maisha yake kusema uongo katika Hadiyth.

Wengine akiwemo Imaam Ash-Shaafi'iy wakasema kuwa: “Ni zile Hadiyth alizodallis tu hazikubaliki, lakini zile alizozielezea kwa njia sahihi zinakubalika.”


Mudhwtwarib:
Nazo ni zile Hadiyth nyingi zinazogongana. Hadiyth aina hii zimedhoofishwa kwa sababu ya kugongana kwake na kutokuwa thaabit.


Munkar:
Nazo ni zile zilizohadithiwa na ‘Dhaifu’ (mtu asiyeaminika) kisha zikakhitilafiana na Hadiyth zilizohadithiwa na Thiqah (mtu mwenye kuaminika).


Al-Mudhwa'af:
Nazo ni zile Hadiyth zilizodhoofishwa na baadhi ya Maulamaa kutokana na udhaifu wa wapokezi wake, wakati baadhi nyingine ya Maulamaa wakasema kuwa ni sahihi.


Al-Matruuk:
Nazo ni zile zilizohadithiwa na mtu anayetuhumiwa kwa uongo katika Hadiyth au hata katika mazungumzo yake. Au anayetuhumiwa kuwa ni Faasiq wa maneno au vitendo. Matruuk pia ni yule mwenye kusahau sana au mwenye kukosea sana.


Wakati Gani Hadiyth Dhaifu Inakuwa Na Nguvu?
Hadiyth dhaifu inapata nguvu pale tu ikiwa rawi wake (mwenye kuhadithia) anatuhumiwa kuwa ameanza kusahau sahau. Ni Sharti awe Thiqah hatuhumiwi kwa Uongo wala kwa Ufaasiq wala kwa kusahau sana. Kisha Hadiyth alozungumza juu yake ziwe zimepokelewa kwa njia nyingi sana, na hapo inapanda darja na kuwa ‘Hadiyth Hasan.’

Na hii ni kwa sababu imepokelewa kwa njia zinazokubalika tena kwa njia ya rawi asiyetuhumiwa kwa uongo au kwa sababu ovu za kumdhoofisha.


Kuzifanyia Kazi Hadiyth Dhaifu:
Maulamaa wamekhitalifiana katika hukumu za kuzifanyia kazi Hadiyth za aina hii katika makundi matatu:

1.     Wapo wanaosema kuwa Hadiyth hizi hazifai kuzifanyia kazi kabisa, yote sawa iwe katika kuamrisha mambo ya Fadhila au katika Hukmu. Na hii ni kauli ya Yahya bin Ma'iyn na Abu Bakr bin Al-'Arabiy na pia Al-Bukhaariy na Muslim.

2.     Wengine wakasema kuwa Hadiyth hizi zinaweza kufanyiwa kazi.

3.     Na wengine wakasema kuwa Hadiyth hizi zinaweza kufanyiwa kazi katika mambo ya Fadhila na katika kuwaidh watu tu. Na kwamba zisitumike katika kutoa hukmu au katika ibada, tena ziwe zimekamilisha baadhi ya masharti kama vile asituhumiwe mmojawapo wa wapokezi wake kwa uongo au ufasiki n.k. Na pia udhaifu wa Hadiyth usiwe mkubwa sana, na pia mtu anapoelezea Hadiyth ya aina hii awajulishe watu kuwa ina udhaifu ndani yake. 

Anasema Dr. Muhammad Al-‘Ajjaaj Al Khatwiyb katika kitabu chake ‘Al-Mukhtaswar Al-Wajiyz fiy 'Uluum al-Hadiyth:
“Mimi naunga mkono rai ya mwanzo inayosema kuwa Hadiyth dhaifu zisifanyiwe kazi kabisa. Zipo Hadiyth za kutosha zilizo sahihi katika mambo ya fadhail na mawaidha kiasi ambapo haina haja ya kuingiza Hadiyth zenye shaka zinazoweza kuwa ni maneno ya uongo aliyozuliwa Mtume wa Mwenyezi Mungu صلى الله عليه وآله وسلم.”         
Pia Fadhail na Tabia njema ni katika mambo muhimu sana katika dini kwa hivyo haina haja kuzitumia Hadiyth dhaifu kwa ajili yake.”

Rai ya Dr. Muhammad Al-‘Ajjaaj ni bora zaidi kwa sababu mtu atawezaje kuiamini Hadiyth iliyosimuliwa na Mudallis, mtu mwenye kubadilisha majina ya Mashaykh au ya miji akijua kuwa anawadanganya wasikilizaji wake, au muongo ‘Kadhaab’ anayependa kuwadanganya watu katika mambo ya kidunia ambaye hatoshindwa kuwadanganya katika mambo ya dini.
Na vipi mtu ataweza kuifanyia kazi Hadiyth Mudhtwarib inayogongana na Hadiyth Swahiyh au Hadiyth Matruuk iliyodhoofishwa kwa ajili ya tabia ovu za msimulizi kwa ajili ya uongo na ufasiki n.k.

Na Allah Anajua zaidi

Friday, December 6, 2013

Dunia Imejaa Ghururi

Dunia Imejaa Ghururi



Naaswir Haamid
Hakika dunia imejaa ghururi, basi yasikudanganyeni maisha ya dunia wala asikudanganyeni yule mdanganyi mkubwa (Ibilisi) katika (mambo ya) Mwenyezi Mungu. Dunia itupeni mbali kama vile Mwenyezi Mungu Alivyotutaka na itafuteni akhera yenu, kwani Mwenyezi Mungu Ameipigia mfano dunia[1].
"Na wapigie mfano wa maisha ya dunia ni kama maji tunayoyateremsha kutoka mawinguni; kisha huchanganyika nayo mimea ya ardhi kisha ikawa majani makavu yaliyokatikakatika ambayo upepo huyarusha huku na huko. Na Mwenyezi Mungu Ana uweza juu ya kila kitu.
"Mali na watoto ni pambo la maisha ya dunia. Na vitendo vizuri vibakiavyo ndivyo bora mbele ya Mola wako kwa malipo na tumaini bora (kuliko hayo mali na watoto)". Al Kahf - 45 – 46
Nakuusieni waja wa Allaah kumuogopa Allaah, kwani Taqwa ni jambo bora la kunasihiana baina ya waja wa Allaah, na ndiyo amali Anayoridhika nayo Mwenyezi Mungu kutoka kwa waja wake.
Mumeamrishwa kumcha Mungu na kwa ajili ya wema mumeumbwa, kwa hivyo ogopeni yale Allaah Aliyokutahadharisheni nayo, kwa sababu Amekutahadharisheni na adhabu kali kabisa.
Muogopeni Mwenyezi Mungu kuogopa kwa kweli na tendeni matendo yenu bila ya kujionesha kwa watu wala kutaka sifa au umaarufu, kwani mwenye kufanya amali yoyote ile kwa ajili ya kujipendekeza kwa mwengine asiyekuwa Allaah, basi Mwenyezi Mungu Humsukumiza nazo amali zake kwa huyo aliyemfanyia amali hiyo.
Ogopeni adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu Hajakuumbeni kwa upuuzi, na wala Hakuacha chochote kiende ovyo. Keshataja athari zenu na Keshajua siri zenu na kuzihesabu amali zenu na kuziandika ajali zenu. Kwa hivyo dunia isikubabaisheni kwani inawaghururisha watu wake, na ameghurika yule atakayebabaishwa nayo.
Na jueni ya kuwa Akhera ndiyo makazi ya milele.[2]

Kwa Nini Wanaume Wamepewa Cheo/Fadhila/Mamlaka Zaidi Kuliko Wanawake? Wanawake

Kwa Nini Wanaume Wamepewa Cheo/Fadhila/Mamlaka Zaidi Kuliko Wanawake?
 Wanawake
SWALI:

Assalamu alayum warahmatu llahi taala wabarakatu. Naomba kuuliza maSWALI: ambayo yananiumiza kichwa changu na kila ninaemuuliza naona sijafaidika bado na majibu ninayoyapata. Kwa nini mwanamme ana cheo kikubwa kuliko mwanamke katika uislam wakati mwanamke ana kazi kubwa kuliko mwanamme? Mwanamke anazaa, anashughulikia nyumba na watoto, anamshughulikia mume kama mtoto mchanga, mwanamke ni mtu mwenye kazi masaa ishirini na nne hapumziki, mwanamme kazi anayoifanya ni kutafuta kijio. Lakini tunaambiwa kwamba kama kuna kusujudu baada ya M Mungu tungeambiwa tusujudie waume zetu, na mirathi wao wamepewa mingi kuliko wanawake, lazima ukitoka uage wao si lazima, wao wamepewa uwezo wa kuoa mke mwengine, wamepewa uwezo wa kutoa talaka, na mambo mengi ambayo mwanamke hakupewa, swali langu liko hapo.



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mwanamme kupewa cheo zaidi kuliko mwanamke.

Hakika hili ni suala ambalo linaonekana hivyo na watu hasa kwa ajili ya kasumba ambazo zinatiwa na wasiokuwa Waislamu wasiouelewa Uislamu na haki inayompatia kila mmoja.

Awali ya yote inatakiwa tufahamu kuwa aliyempatia haki kila mmoja wetu ni Allaah Mtukufu ambaye Anamjua kila mmoja wetu na kila analostahiki. Hakika ukichambua haki zilizoko kwa kila mmoja wetu utakuta kuwa mwanamke amepatiwa haki zaidi na Uislamu kuliko mwanamme. Tutajaribu katika jibu letu kuangazia yote yaliyoulizwa na ndugu yetu.

Kabla ya kuendelea na kuangazia haki na wajibu wa mwanamke na fadhila zake, tuangalie mwanamke alivyokuwa akifanywa kabla ya kukamilishwa Uislamu kwa kuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa mfano:

1. Katika Bara Arabu mwanamke alikuwa hana hadhi, akiuliwa pindi anapozaliwa (an-Nahl [16]: 58 – 59), kurithiwa na hata watoto wake wa kambo pindi alipokuwa mumewe, kunyimwa urithi kabisa na mengineo mengi.

2. Mwanamke katika ustaarabu wa Kigiriki alikuwa ni chombo cha kuondolea matamanio ya kiwiliwili cha mwanamme; hivyo alikuwa akiuzwa kama machungwa sokoni. Socrates alisema: “Mwanamke ni chanzo cha machafuko yote duniani, yeye ni kama mti wa dafali ambao sura ya nje ni ya kuvutia mno lakini iwapo ndege ataula basi ni wazi atakufa”

.
3. Ama mwanamke katika Ukristo hana thamani kabisa. Kulingana na Biblia, mwanamke hana utukufu kwa sababu ameumbwa kwa ajili ya mwanamme (1 Wakorintho 11: 7 – 10). Vile vile yeye ni najisi (Ayubu 14: 1 – 4), ndiye asili ya dhambi (Mwanzo 3: 12) na kadhalika.


4. Mwanamke katika Ubaniyani alikuwa akichomwa hadi kufa na mumewe iwapo mume atakufa kabla yake na kutokuwa na uhuru kabisa wa aina yoyote.


5. Mwanamke wa Kirumi alikuwa ni pambo kwa mwanamme na kwa kuwafurahisha wafalme alikuwa anaimbishwa akiwa uchi. Na tabia hii ya kishenzi imebakia hadi leo.


6. Mwanamke wa Kichina alikuwa hana haki yoyote katika jamii, na mumewe alikuwa ana haki ya kuuza mwili wa mkewe kwa wanaume wengine. Naye alirithiwa kama mali na jamaa za mumewe pindi anapoaga dunia.


7. Ama mwanamke wa kisasa katika tamaduni mbali mbali amekuwa ni chombo cha kuridhisha wanaume kwa njia moja au nyingine. Hakuna bidhaa yoyote inayouzwa bila kuonyesha mwanamke kwenye matangazo.

Tukija katika Uislamu Allaah Aliyetukuka Amempatia kila mmoja kati ya mwanamme na mwanamke majukumu, haki na wajibu wake kulingana na maumbile yake. Hata hivyo, mwanamme amepatiwa daraja ya juu kuliko mwanamke. Anasema Aliyetukuka:
“Wanaume ni walinzi wa wanawake; kwa sababu Allaah Amewafadhilisha baadhi yao kuliko wengine, na kwa sababu ya mali zao wanazozitoa” (an-Nisaa’ [4]: 34).


Ama majukumu yao yanakuwa ni wenye kusaidiana ili kuleta mabadilko mazuri katika jamii. Utapata kwa suala lingine mwanamke yuko juu ya mwanamme na kwa jambo jingine ni mwanamme mwenye jukumu kubwa zaidi.

Uislamu umetangaza kabisa kuwa asili ya mwanamke na mwanamme ni moja:
“Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi (asili) moja. Na Akamuumba mkewe kutoka katika nafsi ile ile. Na Akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi” (an-Nisaa’ [4]: 1).
Na Mtume (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:
“Hakika wanawake ni ndugu wa wanaume” (Abu Daawuud na at-Tirmidhiy).

Ama katika Uislamu hakuna kosa la asili ambalo analaumiwa mwanamke bali wote wanalaumiwa kwa kushawishiwa na Shaytwaan:
“Lakini Shaytwaan aliwatelezesha wote wawili na akawatoa katika hali waliyokuwa nayo” (al-Baqarah [2]: 36).
Na pia:
“Wakasema: Mola wetu! Tumedhulumu nafsi zetu, na kama Hutatusamehe, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye hasara” (al-A‘raaf [7]: 23).
Hivyo, wote walikosa na wakasamehewa, kwa hiyo kutokuwa na makosa baada ya hapo.

Mwanamme na mwanamke wapo sawa katika malipo lau mmoja wao atatenda mema. Anasema Aliyetukuka:
“Na mwenye kutenda mema akiwa mwanamme au mwanamke naye ni Muumini, basi hao wataingia Peponi wakiruzukiwa bila hesabu” (al-Ghaafir [40]: 40).
Na pia,
“Hakika Mimi sipotezi juhudi ya mfanya juhudi miongoni mwenu akiwa mwanamme au mwanamke” (aal-‘Imraan [3]: 195).
Pia waweza kutazama kuhusu haya katika Suratun Nahl: 97 na pia Suratul Ahzaab: 35.

Na mwenye kufanya uhalifu ima wa kuiba au kuzini, akiwa mwanamke au mwanamme atapata adhabu hiyo hiyo. Tazama adhabu ya wizi katika Suratul al-Maa’idah: 38 na uzinzi katika Suratun Nuur: 2.

Pia Uislamu umempatia kila mmoja wao usawa wa kiuchumi na kumiliki mali, kufanya biashara baina ya jinsia hizo mbili. Allaah Aliyetukuka Anasema:
“Na wala msitamani vile ambavyo Allaah Amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wanayo sehemu (haki kamili) ya walivyo vichuma na wanawake pia wanayo sehemu (haki kamili) ya vile walivyo vichuma” (an-Nasaa’ [4]: 32).
Na kwa ajili hii tunaona vipi wanawake katika enzi tofauti waliweza kuusaidia Uislamu na Waislamu kwa pesa zao, mfano mmoja ni Mama wa Waumini Khadijah (Radhiya Allaahu ‘anha).

Mwanamke naye ana haki sawa katika kurithi kile ambacho kimeachwa na jamaa wa karibu. Kwa hilo, Allaah Aliyetukuka Anasema: “Wanaume wana sehemu katika mali wanayoacha wazazi na jamaa wakaribu. Na wanawake pia wana sehemu katika yale waliyoacha wazazi na jamaa wa karibu” (an-Nisaa’ [4]: 7).
Hata hivyo, Uislamu umempatia mwanamme sehemu mbili kwa moja anayopata mwanamke. Huenda hilo likaonekana ni dhuluma kwa mwanamke, lakini tukiona hekima kwa mgao huo tunaweza kugundua kuwa pengine mwanamme amepata sehemu ndogo zaidi kwa mgao huo. Kwa muhtasari mwanamme amepatiwa sehemu kubwa zaidi katika urithi kuliko mwanamke katika shari’ah ya Kiislamu. Na hiyo ni kwa sababu zifuatazo:

1. Mwanamme amelazimishwa kutoa mahitaji kwa mkewe, wanawe, jamaa zake wa karibu, tofauti na mwanamke ambaye hakukalifishwa kishari’ah kutoa mahitaji yoyote. Kwa hiyo, mali anayopata mwanamme inatumika kwa watu wengi ilhali ya mkewe itakuwa ni yake anaweza kuweka akiba, wala hatolazimika kutoa senti moja katika mali aliyorithi kwa ajili ya watu wengine.


2. Mwanamme anawajibika kutoa mahari kumpa mwanamke wakati akioa ilhali mwanamke yeye hatoi mahari bali ndiye anayepatiwa mahari tena anayotaka yeye.

3. Wajibu wa kuwaelimisha watoto, kuwatibu wenye kumtegemea na kuwatunza ni wa mume. Kwa hivyo, urithi wake wote utatumika kwa mambo kama hayo, ilhali urithi wa mwanamke ni wake naye hana wajibu kama huo.

Labda tuchukue mfano wa mzazi aliyekufa akaacha mvulana na msichana na akiwa amebakisha 30,000. Kwa mgao wa Kiislamu ikiwa hakuna mrithi mwengine, mvulana atapata 20,000 na msichana 10,000. Na endapo wote wawili wamefikisha umri wa kuoa na kuolewa, na kila mmoja atalipa au kulipwa elfu kumi (10,000). Kwa minajili hiyo, mvulana atatoa 10,000 na kubakisha 10,000, ilhali msichana akipata 10,000 atakuwa na pesa taslimu 20,000. Hizi pesa za msichana ni zake na anaweza kuzitumia kwa njia yoyote atakayo ilhali mvulana pesa alizobaki nazo itabidi azitumie kumtazama mkewe na watoto atakaporuzukiwa. Msichana hata akizaa jukumu la kumtazama yeye pamoja na mtoto/ watoto ni la mumewe. Na lau ikitokea sinto fahamu (su-u tafaahum) baina ya mume na mkewe, na kutokea talaka msichana huyo atarudi kwa kaka yake na ni jukumu la kaka kumtazama katika hali zote zile.

Pia Uislamu umeweka nidhamu kuwa wazazi wanatakiwa wawalee watoto wote bila ya kuwabagua kati yao kulingana na jinsia zao. Allaah Aliyetukuka Anatuambia:
“Enyi Mlioamini! Jiokoeni nafsi na jamaa zenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe” (at-Tahriym [66]: 6).
Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye watoto wa kike watatu au dada watatu au watoto wa kike wawili au dada wawili akawalea vyema na akamcha Allaah kwa ajili yao basi atapata Pepo” (at-Tirmidhiy).
Na hivyo, hapa tunapata msisitizo wa umuhimu wa kuwalea watoto wa kike kwa wema na njia nzuri.

Uislamu umempatia haki mwanamke kwa kumuelimisha sawa na mwanamme na umesisitiza sana kupewa elimu wanawake tangu awali ya risala yake kupitia kwa Mtume wa mwisho (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Allaah Aliyetukuka Ametujulisha kwamba wenye kumuogopa yeye kikweli ni watu wenye elimu bila kubagua jinsia,
“Na kwa hakika wanaomuogopa Allaah katika viumbe Vyake ni wenye elimu” (al-Faatwir [35]: 28).

Pia jinsia zote mbili zina jukumu la kuamrisha mema na kukataza maovu. Hiyo ni kama Alivyosema Aliyetukuka:
“Na Waumini wanaume na Waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao. Huamrisha yaliyo mema na kuyakataza maovu” (at-Tawbah [9]: 71).

Inatakiwa tufahamu kuwa kila mmoja – kati ya mwanamme na mwanamke ni mchungaji na ana jukumu kila mmoja katika Nyanja yake katika maisha. Mume na mke wanatakiwa wasaidiane katika kutengeneza jamii kwa njia iliyo nzuri zaidi.

Yapo majukumu mengine ambayo yanampasa mwanamme peke yake, miongoni mwayo ni kuitazama nyumba yake na pia kuipigania Dini ya Allaah Aliyetukuka. Mwanamke hapaswi kuitazama nyumba ila tu anapotaka kumsaidia mumewe na hiyo itakuwa ni ihsani kwa upande wake. Ama Jihadi wanawake, hawana uwajibu wa kutekeleza hilo. Na kwa ajili ya kutazama nyumba zao, wakati mmoja wanawake walimtuma msemaji wao, Asmaa’ bint Yaziyd as-Sakan (Radhiya Allaahu ‘anha) alikuwa kwa Mtume (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa yupo pamoja na Maswahaba zake, ambaye alisema: “Ewe Mtume wa Allaah! Umetumwa kwa wanawake na wanaume, nasi tumekuamini. Hata hivyo, wanaume wanapata fadhila zote kwani wao wanahudhuria Swalah pamoja nawe, wanapata kujifunza kwako na wanapigana katika njia ya Allaah ilhali sisi twawatazama watoto wao wakiwa hapo. Je, nasi tutapata nini?” Akasema: “Kukaa kwenu nyumbani mnashirikiana nao katika thawabu”.

Uislamu umetambua kazi kubwa ya mwanamke, hasa katika kubeba mimba, kuzaa na kumlea mtoto na kwa ajili hiyo, Allaah Aliyetukuka Anasema:
“Na Tumemuusia mwanaadamu wazazi wake – mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumnyonyesha na kumuachisha kunyonyesha katika miaka miwili – ya kwamba Unishukuru Mimi na wazazi wako” (Luqmaan [31]: 14).

Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa: “Ni nani aliye na haki wa usuhuba wangu?” Akasema: “Mama”. Kisha nani? Akasema: Mama. Kisha nani? Akasema: Mama. Kisha nani? Akasema: Baba” (al-Bukhaariy na Muslim).

Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametoa dhamana kwa mwanamke ambaye ataswali Swalah zake tano, kufunga mwezi wa Ramadhaan na kumtii mumewe kuwa ataingia Peponi kwa mlango wowote atakao.

Ama kuhusu talaka ameachiwa mume kwa sababu yeye ni mvumilivu zaidi na anaweza kuzuia hasira zake kwa wakati ambao alikuwa afanye jambo ambalo litaleta hasara katika jamii. Mara nyingi mwanamke hisia zake zinakwenda na yale mabadiliko ambayo anakabiliana nayo katika maisha yake na mwilini mwake mabadiliko ambayo mwanamme hana kwa kiasi cha mwanamke. Mwanamke ni mwepesi wa kuchukua hatua za haraka kisha kujuta baadaye mbali kabisa na mwanamme. Bila shaka, mwanamke pia amepatiwa aina mbili za talaka – Khul’ (kujitoa na kujivua katika ndoa) na pia kupitia kwa Qaadhi ikiwa mume ana makosa.

Ukitazama katika haya tuliyoyaeleza utakuta kuwa mwanamke amepatiwa fadhila kubwa na Uislamu kwa yale majukumu wafanyao na kazi zao nzuri.

Tunatumai majibu haya yataondosha shaka shaka ulizokuwa nazo na ambazo zinachangiwa sana na makafiri na wale Waislamu haswa wanawake wanaodai kupigania haki za wanawake wanaotumiwa na makafiri.

Na Allaah Anajua zaidi

احمد محب الدين الأخبار جديد/احب الله ورسوله

حبّ الرسول صلّى الله عليه وسلّم

قال عليه والصلاة والسلام <<من أحبّ سنّتي فقد أحبّني ومن أحبني كان معي في الجنة>>وقال تعالى<<قل إن كنتم تحبّون الله فاتبعوني يحبب كم الله و يغفر ذنوبكم>>

Popular Posts