1. Kueleza fadhila na ubora wa kujifundisha kusoma Qur’an
2. Kutahadharisha watu wasishughulike sana na Dunia mpaka wakasahau Qur’an
3. Kubainisha adabu za kusoma Qur’an.
Utangulizi
Ewe Muislamu
ulipoumbwa na ukaletwa hapa Duniani uliwekewa katiba na mfumo wa kuishi
na njia ya kupita mwanzo mpaka mwisho, nzuri na mbaya, yote hayo
utayapata kwenye Qur’an ukifundishwa na Bwana Mtume (Swalla Llahu
‘alayhi wasallam).
Kusoma Qur’an na Adabu zake
Baada ya
kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumtakia rehema Bwana Mtume (Swalla Llahu
‘alayhi wasallam) na kutakia radhi Maswahaba na waliokuja baada hao
mpaka qiyama.
Ama baadu:
mazungumzo yetu ni kuhusu kitabu ambacho ndio msingi wa kufaulu kwenu,
chenye kuwatoa kwenye kitua, ndani yake kuna khabari ya waliokuja kabla
yenu na watakaokuja baada yenu na hakimu kati yenu, chenye kupambanua
baina ya haki na batili. Mwenye kukiacha ameumia, mwenye kutaka uongofu
kwa hicho ataongoka, na mwenye kutaka kuongoza na kitabu kingine
amepotea; ni kamba ya Allah ya kuaminika isiyokatika; ni utajo wa
Mwenyezi Mungu ni njia iloyonyoka, mwenye kuifuata hapotei na mwenye
kuifuata hachanganyikiwi. Hawashibi nayo wanavyuoni na maajabu yake
hayapungui. Atakaye ukweli ataupata humo na mwenye kuhukumu nacho
atahukumu kwa usawa. Matakwa ya Allah ni tuisome Qur’an ili atuongoza na
atuingize peponi.
Enyi waumini,
Someni Qur’an na muwasomeshe watoto wenu au wenzenu, muwe mumebebwa na
mazingira yake, frikra zenu na mawazo yawe katika mazingira ya Qur’an,
muwahifadhisha watoto wenu kwa udogoni, kwani mkifanya hivyo, inaifanya
igande vizuri zaidi ndani ya nyoyo zao, kwani kuhifadhi udogoni ni kama
kutia naqshi kwenye jiwe.
Ewe waja wa Mwenyezi Mungu, Muongopeni Mola na muwe na hamu na Kitabu hiki. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال الله عز وجل: {إِنَّ
الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنْفَقُوا
مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَنْ
تَبُورَ ﯺ لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُمْ مِنْ فَضْلِهِ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ ﰄ} [فاطر: 30:29 ]
{{Hakika
wanaosoma hiki Kitabu cha Allah na wakasimamisha swala na wakatoa kwa
mali yao tulizowapa kwa siri na dhahiri, wanatarajia biashara
isiofilisika, na hakika Allah atawalipa awaongeze, kwani yeye
mweyekusamehe saana na ni mwenye kushukuriwa}}. Na mke wa Mtume ‘Aisha
akazidi kutufafanulia akisema: ‘Kusoma kwa Qur’an kunatafautiana, kuna
anayesoma hodari. Hivyo, thawabu zake ni nyingi kiasi cha kutangamana na
Malaika na anayesoma akigongagonga atapata malipo mara mbili.
Vilevile Abi Umama akamwambia amemsikia Mtume
akisema: [Someni Qur’an, itakufaa siku ya Qiyama kuwaombea shufaa. Haya
yote ni fadhila za Qur’an na fadhila za kusoma Qur’an]. Na Mtume wetu
(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alimuusia Abu Said akimwambia :
[Nakuusia umche Mwenyezi Mungu, kwani hilo ndio kichwa cha kila kitu, na
utoke kwenda Jihad kwani hilo ndio daraja kuu la Uislamu na umtaje
Mwenyezi Mungu kwa wingi, na usome Qur’an ukifanya hivyo roho yako
itakuwa mahali pazuri mbinguni na utakuwa na utajo upo ardhini].
Adabu za kusoma Qur’an
- Kusoma kwa ajili ya Allah (Subhaanahu wa Taala)
Waja watalipwa
kulingana na nia zao. Mtume anatutolea khabari kuwa watu watalipwa
vibaya japokuwa tunawaona wakifanya mema, nao ni sampuli tatu:-
a) Mtu anajishughulisha na Qur’an kuisoma vizuri, kuikusanya n.k
b) Mtu aliyeuliwa jihad fi sabilillahi.
c) Mtu tajiri anaye toa sana.
Kumbe wote hawa
watatu, wanafanya riya, Allah atamwambia msomaji Qur’an: Si
nilikufundisha Qur’an? Atajibu: Ndio ewe Mola; baadaye ulifanya nini?
atajibu nilikua nikiisoma usiku na mchana, Mwenyezi Mungu atasema:
‘Umesema urongo, na Malaika watazidi kumkaripia ‘muongo we, na watasema
Ewe Mola: huyu bwana, alikuwa akisoma kwa ajili ya watu, na tukaachia
watu wamlipe kule kule duniani. Mungu atawaamrisha Malaika wamtie motoni
(Mwenyezi Mungu atulinde na hayo)
- Kusoma hali akiwa na utwahara
Hapana shaka kuyasoma maneno ya Allah ukiwa msafi, ndio bora kama vile kupiga mswaki, kutawadha n.k. Kwa sababu Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Hakika midomo yenu, ndiyo njia za kusoma Qur’an, isafisheni kwa miswaki]. Mtume
(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akasema tena: [Ikiwa mja anaswali,
Malaika humjia, na wakamsimamia nyuma yake wakimsikiliza Qur’an na
wanaendelea hivyo mpaka anyamaze]. Na je ikiwa mja kinywa chake chanuka? Malaika watakaa kando.
- Kusoma kisawasawa
Mola wetu
anatuamrisha kuisoma Qur’an na Mtume wetu anatushinikiza hivyo, na
maswahaba wakisoma Aya Aya, mmoja wao ni Anas bin Malik Anatuambia Mtume
akiwafundisha hata kuvuta Bismillahi na kadhalika. ‘Abdallah bin Masuud
amesema, “Kusoma haraka haraka ni mbaya bali ni usome pole pole, ipate
kugonga ndani ya moyo, na usimame katika Aya za maajabu, igonge moyo”.
Albara amesema: ‘Nimemsikia Mtume akisoma Wattini Wazzaytuni kwenye
Swala ya Ishaa. Sijawahi kusikia sauti nzuri kama hiyo’. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Tengenezeni sauti zenu mnaposoma Qur’an]. Na hizo hadithi ni swahihi. Ni vizuri asome kwa sauti ya kuimbia ya kughani, imepokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Si katika sisi yule mtu atasoma Qur’aan na haghani]. Na
kughani kwenyewe ni mume kwa sauti ya kiume na mke ajikaze, sio sauti
kuwavutia wengine, na asome asimame kwenye mwisho wa kila Aya kama
anavyotueleza mke wa Mtume Ummu Salama.
- K usoma kwa kwa sauti ya chini
Mtume (Swalla
Llahu ‘alayhi wasallam) alitufundisha, tusisome kwa sauti ya juu, mpaka
tukawaudhi wengine. Kwa mfano, wengine wanaswali na majirani wamelala,
soma kwa kiasi. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) anatuambia katika
maana ya hadithi: “Nyote mtaitwa na mola wenu, msiudhiane wala
msipandishiane sauti nyingi na kama mtu anasinzia aache kusoma alale,
asije akasoma makosa makosa asijijue, na asiache sura zile fadhila zaidi
kama suratul-Ikhlas, ambayo ni theluthi ya Qur’an. Na katika riwaya
kadhaa Mtume amekuwa akisema: [Suratul-Ikhlas,
ni theluthul ya Qur’an. na alikuwa akisoma Suratul Sajdah na Suratul
Insaan katika Sala ya Alfajiri, na Tabaraka na Surat Al-Falaq na An-Nisa
kabla ya kulala. Na vile vile akisoma Surat Al-Falaq na An-Nisa na
Ayatul-Kursiyu baada ya kila swala].
- Kukatazwa kusoma Qur’an katika rukuu na Sijida
Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) mwenyewe ametukataza hilo kwenye hadithi swahihi akisema: [Enyi
watu, hakukubakia kwenye bishara za mitume isipokua ndoto za watu
wema, nami nimekatazwa kusoma Qur’an kwenye rukuu na sijida. Mtukuzeni
Allah na mjitah idi kwa dua]. Na sababu yake ametaja Sheikhul-Islam, kukaa rukuu na sijida ni pahali pa kujidhalilisha Muislam kwa Mola wake.
No comments:
Post a Comment
10 Ways of Protection from Shaytan:
Imam Ibn ul Qayyim
Seeking refuge with Allah from Shaytan. Allah the Most High said, “And if there comes to you from Satan an evil suggestion, then seek refuge in Allah. Indeed, He is the Hearing, the Knowing.” [41:36]
Recitation of the two soorahs al-Falaq and an-Nas, as they have wondrous effect in seeking refuge with Allah from evil, weakening Shaytan and protection from him. This is why the Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said: “No person seeks refuge with anything like the Mu`awwidhatayn (soorahs al-Falaq and an-Nas)”. [an-Nasaa’i, 5337]
Recitation of Ayat al-Kursi (2:255).
Recitation of soorah al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “The house in which al-Baqarah is recited is not approached by Shaytan.” [Muslim]
The final part of al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “Whoever recites the two last verses of al-Baqarah at night they will suffice him.” [Muslim]
Recitation of the beginning of soorah Mu’min (Ghafir), until His saying, “wa ilayhi-l-maseer” (to Him is the destination). (i.e. “Ha. Meem. The revelation of the Book is from Allah, the Exalted in Might, the Knowing, the forgiver of sin, acceptor of repentance, severe in punishment, owner of abundance. There is no deity except Him; to Him is the destination.” [40:1-2])
Saying “la ilaha ill Allah wahdahu la sharika lah, lahul mulku wa lahul hamdu wa huwa `ala kulli shay’in qadir” (there is nothing worthy of worship except Allah, He has no partner, His is the Dominion and Praise, and He is able to do all things) a hundred times.
The most beneficial form of protection from Shaytan: abundance of remembrance of Allah, the Exalted.