Followers

Thursday, July 25, 2013

Kulia wakati wa kusoma Qur’an


  1. Kulia wakati wa kusoma Qur’an
Mola Anasema kulingana na maana ya Aya Akiwasifu waumini ya kuwa; wanaposomewa Qur’an wanapomoka kusujudu huku wanalia na hio  linawanazidisha kumcha Mwenyezi Mungu.  Maswahaba wengi walikua wakilia kwa sababu ya ucha Mungu na kumfuata Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam).  Mmoja wao ni Ibnu Mas’uud aliyesema: ‘ Siku moja Mtume aliniambia nimsomee,  nikamjibu kwani Qur’an, inakuteremkia wewe iweje mimi nikusomee?. Mtume akasema: [Napenda nimsikie mtu akisoma. Nikasoma suratul Nisaa mpaka nikafika Aya fulani, nikaona macho ya Mtume yakitoka machozi].
Mmoja katika maswahaba amesema: ‘Nilimjia Mtume naye akiwa anaswali na ana kitambaa akijifutia nacho machozi. Na habari mashuhuri kwa Abu Bakr anaposoma Qur’an katika kuwasalisha alikua akilia.  ‘Umar ibnu Khattwab alipokuwa akisoma Aya, alisikia sauti za kilio na yeye akalia akadondokwa na machozi. Mke wa Mtume ‘Aisha amewahi kupita sehemu mbalimbali watu wasoma na ukali. ‘Abdullah Ibnu ‘Abbas alikuwa akisoma Qur’an na akirudia rudia na wasikilizaji wakilia.
Kilio wakati wa kusoma Qur’an ni dalili ya kumcha Mwenyezi Mungu ikiwa ni kilio cha kweli, kwani kilio kiko namna nyingi:- kilio cha rahma na sikitiko,  kilio cha kumuogopa Allah, kilio cha mapenzi na shangu, kilio cha furaha na kilio cha huzuni. Kilio kinachotakikana ni cha kumuogopa Mwenyezi Mungu na sio cha kinafiki na riya cha kujifanya unamuogopa Allah. Na kilio cha kumuogopa Mungu, yule msikilizaji naye huhisi kumuogopa Mwenyezi Mungu.  Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Hakika sauti nzuri ya Qur’an ni ukisikia wamuona mwenzio anamuogopa Mwenyezi Mungu].
Ama kujiliza na kujikamua kulia ni sampuli mbili:-
(1) Namna imesifiwa nzuri
(2) Namna imesifiwa vibaya.
(1) Kusifiwa vizuri, kama alivyojiliza ‘Umar alipomuona Mtume na Abubakar wanalia, alipowauliza sababu,  wakachelewa kumjibu, na ‘Umar akakianza chake. Watu wema waliotangulia wanasema: lieni kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu au lizaneni.
(2) Ama kilio kinacholaumiwa ni mtu kujifanya mwema mbele ya watu kwa kulia hiki ni kilio cha unafiki. Kwa yote hayo ni Muumini alie anaposoma Qur’an, khabari zikitokana na mama ‘Aisha, amemsikia mmoja kati ya masahaba watukufu akisema yeye kama ni kulia basi ni moja katika aina tatu:-
(1) Akisoma Qur’an na akisikia inasomwa.
(2) Akisikia khutba ya Mtume.
(3) Akiona jeneza.
3   Kuizingatia Qur’aan
Ukisoma Qur’an na ukizingatia, ndio jambo muhimu zaidi ambalo linazaa matunda Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Anasema:
قال الله تعالى: {كِتَابٌ أَنْزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِيَدَّبَّرُوا آَيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ} [ص: 29]
{{Tumeteremsha kitabu kilicho barikiwa, basi kisomeni na mkizingatie enyi mulio na akili}}. Basi tukisome na tukifikirie na tukifahamu vilivyo. Na ikiwa hatuzingatii Mwenyezi Mungu Atatuuliza ilikuaje wasikizingatie ama nyoyo zao zimefungwa, nyuma ya Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) baada ya Fatiha akaanza Baqarah akarukuu baada ya kumaliza Aya mbili akaanza rakaa nyengine baada ya fatiha akasoma suratul Al-‘Imran na yote hayo, akipita tasbihi, anasabihi, na kadhalika mpaka tukamaliza swala na maswahaba wengi hivi ndivyo wakifahamu na kuizingatia, mmoja ni AbdulRaman anasema, wenzetu wakisoma Qur’aan kwa Mtume baadae wakaendea wenzao, basi wale wenzao wakichukuwa Aya kumi kumi wakienda nazo, baada ya kufahamu na kuzingatia wakija wakijiongezea nyingine
  1. Kusujudu kwa sababu ya kusoma Qur’an
Msomaji akipitia sehemu ya sijda, ni muhimu asujudu. Na wamekhitalifiana wanavyuoni kuhusu jambo hili, Abu Hanifa amesema ni wajibu kusujudu, ama kauli yenye nguvu ni kauli ya ‘Umar Ibnu Khatwab, kwamba kusujudu ni sunna na hivyo ndio kauli ya wanavyuoni wengi. Msomaji awe katika hali ya adabu, inafaa asome akiwa amekaa, amesimama, au akitembea na kadhalika. Kama Allah (Subhaanahu wa Taala) anavyosema:  
قال تعالى: {الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَى جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ } [آل عمران: 191].
{{ Waja wema wanamtaja Mwenyezi Mungu ikiwa wamesimama au wamekaa au wamelala}}. Lakini vizuri zaidi ni mtu akae kisawasasa kikao cha heshima, kama Mtume alivyokua akikaa na akielekea kibla, akisoma baada ya swalatul Fajri mpaka jua kuchomoza, na asikae sana, isipite siku tatu pasina kusoma Qur’an,
Kutahadharisha Kusahau Qur’an
Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, watu wameshughulika na dunia wakasahau kusoma Qur’an, na watoto wameshughulika na masomo ya kilimwengu mpaka hawana wakati wa kutosha na walimu hawashughulikiwi ikapelekea wasifanye kazi yao vizuri. Yote hayo, yamefanya Qur’an kuwa  kitu kigeni, dhaifu na hata wasomao Dini wanapata shahada nzuri nzuri, hawasomi Qur’aan kisawasawa imepelekea kuipa mgongo Qur’an. Tumekua wajinga na hata  katika mambo ya kidini tunaongozwa na wajinga hii ndio hasara, hatuipi kipaombele Qur’an. Hali hii itafanya Qur’an itushitaki kesho akhera ikisema:  “ Ewe Mola hawa waja wako duniani walinitupa na wakanidharau, walikuwa hawanisomi, hawanifikirii na hawanizingatii, Wala hawanitumii katika maamrisho wala makatazo, bali wao wakishughulikia machezo, nyimbo na maneno ya upuzi.
Hatuna budi tupate Walimu Wazuri
Enyi waja wa Mwenyezi Mungu hatuna budi mpaka tupate walimu wazuri, wa kutusomeshea watoto, sio kila mtu au mtoto apate msahafu ajisomee mwenyewe mpaka Mwalimu amsikilize kwani maandishi peke yake hayatoshi, tupate utatuzi wa kuwaweka walimu wa kisawa na utatuzi wa matatizo ya wanafunzi, na mipangilio ya masomo yao, bali ziko madrasa nyingi kubwa kwa ndogo, vichochoroni na upenuni, kumbi na vyumba, vyote havina matokeo mazuri, tunachekwa na dini nyinginezo, walimu na wanafunzi na majengo, yapo katika hali ya kudharauliwa, sababu hatuna mwelekeo, lakini lau tungekuwa na wasimamizi wa mijini, mashambani tungepata matokeo mema.
Tuhifadhi Kitabu Kitukufu
Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, Tujifundishe na tukihifadhi kitabu chake, tukisomeni kwa kumuogopa Allah. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)  amesema:  [Mwenye kusoma herufi moja ana thawabu kumi, na utahesabiwa harufu moja moja]. Amesema ibnu-ll-Qayyim: ‘ Hebu zingatia, Allah ni mfalme wa wafalme, Atubembeleza tujipatie thawabu nyingi, Atutie moyo tupate thawabu hizo kwa urahisi, na ametunasihi saana, hii neema ya uhai isitupotee, vile vile ametuahidi raha kubwa kwa kumtii, na Ametuonya adhabu kali kwa kumuasi, na waja wema, inawapeleka kwenye wema ni kumtaja Allah kwa wingi kuwa ni Nuru, ni dawa, ni uongofu ni upambanuzi na ni hoja.
Mwisho
Mwenyezi Mungu alituumba kwa lengo la kiibada, kisha akatutumia Mtume akatufundisha vile atakavyo Yeye Mola, lakini Mungu huyo hatumuoni wala hatumsikii sauti, na tunaona dalili zake, alama zake na miujiza yake, kama mbingu na ardhi usiku na mchana na maneno yake matukufu. Mwenye kuyasoma atapata thawabu nyingi kwa kila herufi moja thawabu kumi na faida tofauti tofauti utazipata utakapoisoma Qur’an.
Nyoyo zetu na akili zetu zimejaa mashughuli ya kilimwengu hata hatuna nafasi ya kusoma Qur’an. Kwa hivyo ni kuangalia akhera yetu tupate taqwa, na tufuate utaratibu wa kuisoma. Tuisome tuijuwe maana huenda Qur-an ikarudi kwenye vifua vyetu na mienendo yetu.
Ewe Mwenyezi Mungu, Tujaalie waja wema,  tuisome Qur’an kama maswahaba, tuisome na kuifahamu, tuisome kwa nidhamu, adabu na kuiheshimu.

No comments:

Post a Comment

10 Ways of Protection from Shaytan:

Imam Ibn ul Qayyim

Seeking refuge with Allah from Shaytan. Allah the Most High said, “And if there comes to you from Satan an evil suggestion, then seek refuge in Allah. Indeed, He is the Hearing, the Knowing.” [41:36]

Recitation of the two soorahs al-Falaq and an-Nas, as they have wondrous effect in seeking refuge with Allah from evil, weakening Shaytan and protection from him. This is why the Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said: “No person seeks refuge with anything like the Mu`awwidhatayn (soorahs al-Falaq and an-Nas)”. [an-Nasaa’i, 5337]

Recitation of Ayat al-Kursi (2:255).

Recitation of soorah al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “The house in which al-Baqarah is recited is not approached by Shaytan.” [Muslim]

The final part of al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “Whoever recites the two last verses of al-Baqarah at night they will suffice him.” [Muslim]

Recitation of the beginning of soorah Mu’min (Ghafir), until His saying, “wa ilayhi-l-maseer” (to Him is the destination). (i.e. “Ha. Meem. The revelation of the Book is from Allah, the Exalted in Might, the Knowing, the forgiver of sin, acceptor of repentance, severe in punishment, owner of abundance. There is no deity except Him; to Him is the destination.” [40:1-2])

Saying “la ilaha ill Allah wahdahu la sharika lah, lahul mulku wa lahul hamdu wa huwa `ala kulli shay’in qadir” (there is nothing worthy of worship except Allah, He has no partner, His is the Dominion and Praise, and He is able to do all things) a hundred times.

The most beneficial form of protection from Shaytan: abundance of remembrance of Allah, the Exalted.

احمد محب الدين الأخبار جديد/احب الله ورسوله

حبّ الرسول صلّى الله عليه وسلّم

قال عليه والصلاة والسلام <<من أحبّ سنّتي فقد أحبّني ومن أحبني كان معي في الجنة>>وقال تعالى<<قل إن كنتم تحبّون الله فاتبعوني يحبب كم الله و يغفر ذنوبكم>>

Popular Posts