Followers

Thursday, August 29, 2013

Waasi wakatili wanaopigania Katanga

Gedeon Kyungu Mutanga huwaambia vijana kuwa wanapigania maisha mazuri 

Baada ya muasi mkubwa na anayesifika sana kutoroka jela Katanga, mkoa huo wenye madini chungu nzima uliokuwa thabiti umekuwa ukivurugwa kwa mwaka mmoja uliopita na kundi linalotaka eneo hilo kujitawala.
Mkoani Katanga, ni kawaida kuwasikia watu wakilalamika kuwa hawajanufaika sana kutokana na madini yaliyo kwenye mkoa huo, mfano Shaba nyekundu na Cobalti kwa hivyo sio jambo la kushangaza kuwa vijana wengi waliitikia wito wa eneo hilo kujitenga.
Chini ya wiki moja baada ya uhuru wa Congo mwezi Juni mwaka 1960, ulitangaza kuwa unajitenga na hivyo kuzua mgogoro uliochochewa na uhasama uliotokana na vita baridi.
Kiongozi wa wale waliotaka kujitenga Moise Tshombe ambaye pia alikuwa mfanyabiashara , aliungwa mkono na Ubelgiji, Marekani na Uingereza zote zenye maslahi ya uchimbaji madini.

Baada ya miezi minne, waziri mkuu wakati huo Patrice Lumumba alipinduliwa na baadaye akauawa huku Tshombe akirejeshwa kwenye jeshi kutokana na shinikizo kutoka kwa Umoja wa Mataifa na Katanga kufanywa kuwa sehemu ya DRC mwaka 1963.

Siasa za vita baridi huenda sio hoja kwa mkoa huo wenye kuzungumza Kiswahili, na ambao ni wenye ukubwa sawa na Ufaransa.
Zamani mbinu iliyokuwa inatumiwa sio ya sasa. Wapiganaji wa vuguvugu la Mai Mai hawatumii mbinu zitakazowafurahisha wenyeji wa mkoa huo.
''Walimfungia mamangu kwenye mti na kumdunga kwa mshale,'' alisema Antoinette mwenye umri wa miaka 18 akikumbuka mashambulizi yaliyofanywa katika kijiji chake cha Montofita ambapo baadhi ya nyumba ziliteketezwa na mamake kutekwa nyara.

"walikata matiti yake na niliona kila kitu kwa macho yangu. Kisha kila mwanamume akanibaka. Majirani zangu walizikwa wakiwa hai,'' alisema Antoinette.

Kijiji cha Pueto ni makao kwa maelfu ya wakimbizi waliotoroka Katanga

Antoinette amepata hifadhi katika kijiji cha Pweto katika eneo la mpakani na Zambia ambako zaidi ya watu laki sitini pia wamepata hifadhi.
Shirika la kuwahudumia wakimbizi UNCR, linakadiria kuwa zaidi ya 1,700 walioachwa bila makao ni wanawake na wengi walibakwa kabla ya kutoroka.
Takriban watu laki nne waliachwa bila makao na sasa wamepata hifadhi katika kambi za wakimbizi.
"labda ikiwa wenyeji wa Katanga wangewaunga mkono waasi hao wa Katanga, lakini waasi hawakutupa nafasi, walianza kutuua na kuchoma nyumba zetu. Sio kama watu wanaopigania ukombozi,'' asema Priscille,mkimbizi anayeishi katika kijiji cha Pweto.
Kuna makundi mengi ya wapiganaji wa Mai Mai, neno hilo likitumiwa na makundi yaliyojihami mkoani humo.

Usajili vijijini

Kata Katanga, neno la kiswahili linalomaanisha Katanga ijitawale, lilibuniwa baada ya Gedeon Kyungu Mutanga kutoroka jela mwezi Septemba mwaka 2011.
Kabla ya kufungwa jela mwaka 2006, alikuwa kiongozi wa kundi la waasi ambalo lilisaidia jeshi la Congo kupigana na waasi kutoka Rwanda miaka ya tisini.
Baada ya kumalizika kwa mgogoro huo,alidaiwa kuendelea kupokea msaada wa mtu aliyekuwa jeshini.
Hata hivyo baada ya kutoroka alisemekana bado alikuwa anapokea msaada wa kifedha kutoka kwa mtu aliyekuwa anaishi ughaibuni.

Mwanamume mmoja aliyetoroka kundi hilo la waasi akiwa na wake wawili pamoja na watoto wanane, aliambia BBC ambavyo kundi hilo huwasajili wapiganaji kwani huwashawishi vijana kujiunga na waasi hao wakipigania maslahi yao na kuwa hawakuwahi kumuona kwa macho yao kwani alikuwa akijificha chumbani wakati akiongea nao.

Katanga ina utajiri mkubwa sana , lakini wanachi wanahisi kuwa hawafaidi vyovyote.
Madini ya Cobalt yako kwa wingi zaidi katika mkoa huu kuliko sehemu yoyote nyingine duniani na mkoa huu ni wa pili kwa ukubwa katika uzalishaji wa Shaba nyekundu.
Wakati maelfu ya watu wakitembea siku hizi kwenye barabara zenye vumbi, kutoroka waasi hao, barabara zengine hutumiwa kusafirisha madini yenye thamani ya mamilioni ya dola nje ya nchi.
Ni familia chahe sana ambazo zimepewa mahema na umoja wa mataifa wengi hulazimika kujijengea

Malori mengi yenye madini ya Cobalt na Shaba nyekundu, huonekana yakiwa yamepanga foleni kuingia Zambia
Kulingana na sheria ya DRC serikali inapaswa kuupatia mkoa huo asilimia 40 ya kodi zinazotozwa makampuni ya uchimbaji kwa mkoa wa Katanga lakini mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa pesa hizo hazijafaidi chochote.
Lucien,ni mwalimu wa shule kutoka Kabisa ingawa sasa anaishi kijiji cha Pweto, anasema kuwa mamia ya vijana wamejiunga na wapiganaji wanaopigania uhuru wa Katanga kutoka kwa kijiji anakoishi.
"Nililengwa kwa sababu nina elimu , mimi huwambia watu ukweli wa mambo na kwa hivyo builiwashawqishi vijana kutojiunga na waasi hao, '' aliambia BBC
''Niliwaambia kuwa mwishowe wangetaabika tu.''
Kulingana na maafisa wakuu katika kijiji cha Pweto, mamia ya wapiganaji wa Mai Mai wameondoka jeshini tangu mwanzoni mwa mwaka huu, wakiwa wamechoka na kuishiwa na matumaini.
"Hatutawahi kupata uhuru. Leo tuko maskini zaidi kuliko miaka ya nyuma, wengi wetu wamefariki,'' alisema mpiganaji mmoja aliyekuwa katika vuguvugu hilo.
Mnamo mwezi Machi karibu wapiganaji 200 wa Kata Katanga wakiwa wamejihami na kubeba bendera za kutaka ukombozi wa Katanga waliingia Lubumbashi.
Walipeperusha bendera yao kabla ya kujisalimisha kwa UN baada ya makabiliano makali ambapo wapiganaji 23 waliuawa. Tangu hapo wapiganaji hao wametishia kwa mara nyingine kuvamia mji huo.
Je unaweza kuwalaumu waasi kwa kuchukua silaha wakidai maslahi yako ambayo ni haki yao huku wakitaka uhuru wao? Baadhi wanasema wanaona uhuru wa Katanga ukiwa kitu kizuri lakini inategemea wataupata kwa njia gani.
Waziri mkuu wa DRC Matata Ponyo, anasema kuwa hapa hakuna uasi akiongeza kuwa watu wana haki ya kudai haki zao kwa njia ya kidemokrasia na kuwa serikali itajitahidi kukabiliana na makundi kama hayo.

No comments:

Post a Comment

10 Ways of Protection from Shaytan:

Imam Ibn ul Qayyim

Seeking refuge with Allah from Shaytan. Allah the Most High said, “And if there comes to you from Satan an evil suggestion, then seek refuge in Allah. Indeed, He is the Hearing, the Knowing.” [41:36]

Recitation of the two soorahs al-Falaq and an-Nas, as they have wondrous effect in seeking refuge with Allah from evil, weakening Shaytan and protection from him. This is why the Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said: “No person seeks refuge with anything like the Mu`awwidhatayn (soorahs al-Falaq and an-Nas)”. [an-Nasaa’i, 5337]

Recitation of Ayat al-Kursi (2:255).

Recitation of soorah al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “The house in which al-Baqarah is recited is not approached by Shaytan.” [Muslim]

The final part of al-Baqarah. The Messenger, sallallahu `alayhi wa sallam, said, “Whoever recites the two last verses of al-Baqarah at night they will suffice him.” [Muslim]

Recitation of the beginning of soorah Mu’min (Ghafir), until His saying, “wa ilayhi-l-maseer” (to Him is the destination). (i.e. “Ha. Meem. The revelation of the Book is from Allah, the Exalted in Might, the Knowing, the forgiver of sin, acceptor of repentance, severe in punishment, owner of abundance. There is no deity except Him; to Him is the destination.” [40:1-2])

Saying “la ilaha ill Allah wahdahu la sharika lah, lahul mulku wa lahul hamdu wa huwa `ala kulli shay’in qadir” (there is nothing worthy of worship except Allah, He has no partner, His is the Dominion and Praise, and He is able to do all things) a hundred times.

The most beneficial form of protection from Shaytan: abundance of remembrance of Allah, the Exalted.

احمد محب الدين الأخبار جديد/احب الله ورسوله

حبّ الرسول صلّى الله عليه وسلّم

قال عليه والصلاة والسلام <<من أحبّ سنّتي فقد أحبّني ومن أحبني كان معي في الجنة>>وقال تعالى<<قل إن كنتم تحبّون الله فاتبعوني يحبب كم الله و يغفر ذنوبكم>>

Popular Posts