Followers

Sunday, October 13, 2013

IDUL-ADH’HA


Hekima ya Swala ya Iddi
Imeshurutishwa swala ya Iddi ili kuzishukuru neema za Mwenyezi Mungu na kushibisha matamanio ya binadamu.
Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى : {فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا فِطْرَةَ اللَّهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّهِ } [الروم:30]
 {{ Basi elekeze uso wako katika Dini iliyo sawa sawa, ndilo umbile Mwenyezi Mungu Alilowaumbia watu (yaani Dini hii ya kislamu inawafikiana barabara na umbo la binadamu) hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Mwenyezi Mungu}}.
 Iddi ni Mkusanyiko wa Mambo Manne;
1-     Kukusanyika kwa watu.
2-     Kukusanyika kwa sehemu.
3-     Kukusanyika kwa wakati.
4-     Kukusanyika kwa ibada maalum.
Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال الله تعالى: {وَلِكُلِّ أُمَّةٍ جَعَلْنَا مَنْسَكًا لِيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ عَلَى مَا رَزَقَهُمْ مِنْ بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ فَإِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ فَلَهُ أَسْلِمُوا وَبَشِّرِ الْمُخْبِتِينَ } [الحج:34]
{{ Na kila umma tumewafanyia mahali pa kuchinja, mihanga ya Ibada ili kulitaja jina la Mwenyezi Mungu juu ya vile alivyowaruzuku katika wanyama hao wenye miguu mine. Basi Mungu wenu ni Mungu mmoja tu; Jinyenyekesheni kwake. Na wape khabari njema wale wanyenyekevu}}.
Imepokewa na Anas kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alipokwenda Madina aliwakuta watu wa Madina wana siku mbili wanacheza, Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akawaambia Mwenyezi Mungu amekubadilishieni siku mbili hizi kwa iddul Adha (kuchinja) na Iddul-fitr (baada ya Ramadhani). Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قوله تعالى: {فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ} [الكوثر:2]. 
{{ Basi Sali kwa ajili ya Mola wako na uchinje kwa ajili ya mola wako}}.
Hukumu ya Kuchinja katika Siku ya Iddi  Pamoja na Sharti Zake na Namna ya Kuchinja.
Amesema Ibnu ‘Umar “Kuchinja ni sunnah”. Amesema Imam Sha’abi: “Haruhusiwi mtu kuacha kuchinja isipokuwa kwa mwenye kuhiji na kusafiri”. Imepokewa na Ibnu Majah kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) ameamrisha kugawanya nyama ya Udhiya mara tatu akisema kuleni, toeni sadaka na muhifadhi.
Kushurutishwa Kupiga Takbira pamoja na Hukumu Zake na Namna yake
Imepokewa na Ibnu Abbas amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)  hakuna siku kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, wala siku zinazopendekezwa kwake amali kama siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhulhija, zidisheni Tasbihi na Takbiri na Tahlil (Lailaha ila Allah).


Kutembelea Jamii na kutumia Wakati kwa Michezo na Furaha
Amesema ‘Aisha kuwa wahabesha ( watu wa Ethiopia) wanachezea siku ya Iddi,  akaniita Mtume wa Mwenyezi Mungu na nikawa nawaangalia kupitia mabega ya Mtume, akaja Abubakar. Mtume akamwambia Abubakar amuwache kwani kila jamii wana Iddi yao. Ni makosa wanawake kudhihrisha mapambo yao na kujirembesha. Kunazidi kujirembesha kwa wanawake katika siku ya Iddi na hivyo ni kinyume ya sheria.
Katazo la kupigana na kuoneshana Silaha katika Siku ya Iddi
Imepokewa na Abu Huraira Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akisema atakayebeba silaha si katika sisi ( kwa Waislamu). Amesema Hasan Al-Basri: kumekatazwa kubeba silaha katika siku ya Idd isipokuwa kwa atakayetishiwa na adui.
Kukutana Siku ya Iddi na Ijumaa
Imepokewa na Abu Huraira Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema “Imekutana kwenu nyinyi Idd mbili atakayetaka hatoswali ijumaa, lakini mimi nitaswali Idd na Ijumaa (haimanishi kupomoka swala ya adhuhiri).
Kuombea Dua za Kheri Siku ya Iddi
Amesema Adham kijakazi wa Umar ibn Abdul Aziz “Tulikuwa tukimwambia ‘Umar Ibn ‘Abdul ‘Aziz siku za Idd mbili: Mwenyezi Mungu Atukubalie sisi amali zetu na alikuwa akitujibu”
Mwisho
Ndugu Waislamu, siku ya Iddi ni siku muhimu katika maisha ya Muislamu kwa kufanya mambo ya kheri na kujikurubisha kwa Allah (Subhaanahu wa Taala). Siku hii si siku ya kufanya machafu na kumkasirisha Allah (Subhaanahu wa Taala). Kufanya hivyo ni kinyume na mafundisho ya Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) na Masahaba wake. Ni jukumu la kila Mzazi kuwafundisha familia yake hukumu ya siku hii muhimu katika Dini ya kislamu, ili jamii ya kiislamu iweze kujiepusha na mambo ya upuzi katika siku hii.
Tumuombe Mwenyezi Mungu Atupe baraka na kutusamehe madhambi yetu na kutupa mazuri hapa duniani na kesho akhera.


Saturday, October 12, 2013

MAPENZI YA MWENYEZI MUNGU (SW) NA MTUME WAKE (SAW)


.


.
Na ameweka bayana Mtume kama ilivyo katika sahihi Muslim kwamba wazushi watasogea katika birika la Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) na watafukuzwa kwa sababu ya uzushi wao unamaliza Dini sahihi ya Mwenyezi Mungu.


1.  Kufuata matamanio ya nafsi zao na kuacha Sunna Sahihi za Bwana Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Amesema mwanachuoni Muqaatil Ibn Hayan: ‘Watu wa matamanio ni maangamivu kwa umati Muhammad hali ya kuwa wanamtaja Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) na jamaa zake wakitaka kuwavutia kwa utajo huu mzuri, watu wasiojua chochote katika Dini na kuwatia katika maangamivu, na hao wamefanana zaidi na wanaotia sumu katika asali’.
2.  Kufuata baba zetu bila ya uongofu. Mola (Subhaanahu wa Taala)  Amesema  pale Nabii Ibrahim alipowaambia watu wake:
قال تعالى : {قَالُوا نَعْبُدُ أَصْنَامًا فَنَظَلُّ لَهَا عَاكِفِينَ ﮡ قَالَ هَلْ يَسْمَعُونَكُمْ إِذْ تَدْعُونَ ﮧ {قَالَ هَلْ يَسْمَعُونَكُمْ إِذْ تَدْعُونَ ﮬ قَالُوا بَلْ وَجَدْنَا آَبَاءَنَا كَذَلِكَ يَفْعَلُونَ ﯔ)   [الشعراء:74:71]
  {{ Je mnaabudu nini?  Wakasema tunaabudu masanamu na hatuachi kulazimiana nayo, akasema : Je wanawasikia mnapowaomba au wanawanufaisha au wanawadhuru,  wakasema: Tumewapata baba zetu wakifanya hivyo}}.
3.  Kufuata maneno ya wanavyuoni yanayokwenda kinyume na mafunzo mazuri na sahihi ya Uislamu.
Madhara ya Uzushi
Enyi waja wa Mwenyezi Mungu uzushi una madhara mengi ambayo yatakiwa tuyajue. Na katika madhara hayo ni:-
1)  Uzushi huangamiza dini sahihi huku ukichukua nafasi ya Sunna. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)  amesema: [Hawatazua watu uzushi isipokuwa ataondoa Mwenyezi Mungu kwao Sunna mfano wake].
2)   Ufisadi wa uzushi ni kujiepusha mtu na Sunna na akawa mtu hataki kuzifanya sunna akawa na bidii kutekeleza uzushi, na kumbe anapoteza nguvu zake na pia wakati wa huku akiaona kuwa Dini ni pungufu akitaka kuikamilisha dini na uzushi wake.
3)  Uzushi unarejesha watu katika jahiliya kwa kuwafanya watengane wawe mbali mbali,  kila kikundi kinafurahia msimamo wake. Mola (Subhaanahu wa Taala) amesema:
قال الله تعالى : {كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَﰅ} [الروم: 32 ]
 {{ Kila kikundi kinafurahia msimamo wake}}.  Kwani Sunna inafanya watu kuwa kitu kimoja. Mola Asema:
قال تعالى : {وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا} [آل عمران: 103 ]
 {{ Shikamaneni na Dini ya Mwenyezi Mungu wala msifarakane}}.
4)  Uzushi unasababisha kuikataa haki anapolinganiwa mzushi katika Sunna hakubali na natija yake huendelea kushikamana na uzushi wake.
5)  Uzushi unaharibu Dini sahihi ya Mwenyezi Mungu,  kwani uzushi ndio silaha kubwa ya kuharibu Dini ya Mwenyezi Mungu. Kwani wengi katika wazushi hutaka maslahi ya kidunia katika ulinganizi wao.
Mwisho
Ndugu Waislamu ! Maswahaba walikuwa wakiwatahadharisha watu na uzushi katika Dini. Ilimfikia Ibn Mas’uud kuwa ‘Amru ibn ‘Utba ambaye ni katika wafuasi wake amejenga Msikiti mjini Kuufa akaamrisha Ibn Mas’uud uvunjwe Msikiti ule, kisha akasikia sasa wanajikusanya nje ya Msikiti huo wakileta nyiradi na adhkaar na takbira maalum kinyume na mafunzo mazuri ya bwana Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Alifunga safari Ibn Mas’uud akawajia wao hali ya kuwa amejifunika uso wake ili wasimjue, kisha akakaa nao wakaanza kuleta adhkaar zao, kisha akafungua uso wake,  kisha akawauliza mumekuwa wajuzi wa dini zaidi kuliko maswahaba wa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam), Kisha akawaonya watu hao na uzushi, na hapo hapo watu waliomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu kwa uzushi wao waliokuwa wakiufanya. Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume ! Muogopeni Allah (Subhaanahu wa Taala),  na mujue ya kwamba yaliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) yanamtosha Muislamu katika maisha yake wala asijishughulishe na chochote cha uzushi. Na wausia mshikamane na Sunna kisawasawa.

Mwisho kabisa tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie ni miongoni mwa mwenye kushikamana na Sunna na kijiepusha na uzushi na atuongoze katika Dini Yake ya sawa.

KUWAKUMBUSHA WATU DALILI ZA MWENYEZIMUNGU KATIKA VIUMBE


Ama baada ya kumtukuza na kumshukuru Allah na pia kumtakia rehma na amani Mtume wetu. Mwenyezi Mungu Ametuamrisha tuamini kwamba yeye yuko. Na Aya zinazozungumzia suala hili ni nyingi sana pia ameumba viumbe vinavyoonesha kwamba yeye yupo.Kwani kupatikana kwa viumbe ni kuonesha kuna aliyeumba.
Enyi ndugu katika imani ! Hakika katika kila kitu alivyoviumba Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) ni dalili ya kuonesha kwamba yeye ni mmoja, na ndiye anayestahiki kuabudiwa kwa haki kabisa na haifai kushirikishwa na yoyote wala chochote.
Napenda nizitaje baadhi ya Aya ambazo zimetuamrisha kuzingatia katika ulimwengu.
قال تعالى : {أَوَلَمْ يَنْظُرُوا فِي مَلَكُوتِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا خَلَقَ اللَّهُ مِنْ شَيْءٍ وَأَنْ عَسَى أَنْ يَكُونَ قَدِ اقْتَرَبَ أَجَلُهُمْ فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ}     [الأعراف : 185].
Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala): {{ Je hawaangalii ufalme katika mbingu na ardhi na alivyoumba Mwenyezi Mungu katika vitu, na huenda ikiwa umekaribia muda wao wa kuondoka duniani kumalizika. Basi ni maneno gani baada ya Qur’an watayamini}} [Al-Araaf : 185].
وقال : {أَفَلَمْ يَنْظُرُوا إِلَى السَّمَاءِ فَوْقَهُمْ كَيْفَ بَنَيْنَاهَا وَزَيَّنَّاهَا وَمَا لَهَا مِنْ فُرُوجٍ *الْأَرْضَ مَدَدْنَاهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنْبَتْنَا فِيهَا مِنْ كُلِّ زَوْجٍ بَهِيجٍ *تَبْصِرَةً وَذِكْرَى لِكُلِّ عَبْدٍ مُنِيبٍ } [ق : 6 – 8].
 Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala): {{ Je hawaangalii mbingu juu yao vipi tuliijenga na kuipamba na kuifanya kuwa haina nyufa. Na ardhi vipi tuliitandaza na kuiweka vigingi (isitikisike) na tukaotesha katika ardhi hiyo kila mimea mizuri hali ya kuwa ni kifumbua macho kwa kila mtu muelekevu}} [Qaaf : 6 - 8].
وقال : {أَفَلَا يَنْظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ * وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ * وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ * وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ } [الغاشية 17 – 20].
 Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala): {{Je hamwangalii Ngamia vipi ameumbwa, na mbingu vipi zimeinuliwa, na milima vipi imekitwa na ardhi vipi imetandikwa}] [Al-Qaashiyah: 17- 20].  Hizi ni alama ambazo Mola anataka tuzingatie kuumbwa kwake.
Napenda sasa kutaja baadhi ya viumbe vingine vya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala).  Navyo ni vinavyopatikana katika ardhi kama vile;  Maji, Madini, Majabali, Mimea aina tofauti tofauti, kwani Mwenyezi Mungu ameidhalilisha ardhi hii kwa manufaa ya wanadamu na wanyama, wanadamu wanailima kwenye ardhi na kupanda mimea ili kujipatia chakula chao, wanatoa maji katika ardhi kwa matumizi yao na pia kuwanywesha wanyama wao. Mwenyezi Mungu amesema
قال تعالى {وَفِي الْأَرْضِ آَيَاتٌ لِلْمُوقِنِينَ} [الذاريات:20].
Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala): {{ Na katika ardhi kuna alama nyingi kwa wenye yakini}}. Tukiangalia mbinguni kuna nyota nyingi, jua, mwezi na sayari nyinginezo. Vilevile mbinguni kuna viumbe vya Mwenyezi Mungu ambao ni Malaika wanaotekeleza kazi alizowapa Mola aliyetukuka.
Na katika alama nyingine za kumjua Mwenyezi Mungu ni usiku na mchana. Mchana ni wakutafuta maisha na riziki na usiku ni kupumzika.
قال تعالى {وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاسًا *وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشًا } [النبأ:11:10]   .
Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala): {{ Na tumeufanya usiku ni nguo na tukaufanya mchana ni wa kutafuta maisha}}. Na katika alama hizi mbili za usiku na mchana amewafanyia watu mchana kwenda  katika ardhi ya Allah na kutafuta fadhila zake na katika kutafuta fadhila hizo atazidi kubainikiwa mwanaadamu na kuzifahamu alama nyingine za Mwenyezi Mungu. Na katika usiku ni wakati wa kujipumzisha baada ya uchovu wa mchana katika hali ya kutafuta riziki na kutafuta maisha.
Tukigusia zaidi alama za Allah ni wanyama wengi wakubwa kwa wadogo na katika wadogo kuna wadogo zaidi, kuna wengine ametufanyia kuwatumia katika kazi zetu za kila siku, kama kubeba mizigo na kutupeleka sehemu nyingine  Na dalili ya alama za Mwenyezi Mungu ni kuumbwa kwetu kwani kuna mazingatio makubwa sana.
قال تعالى {وَفِي أَنْفُسِكُمْ أَفَلَا تُبْصِرُونَ} [الذاريات:21].
Mola (Subhaanahu wa Taala) Amesema:{ Na je katika nafsi zenu basi hamuoni}.   Aya hii inatueleza kuwa katika maumbile yetu wanadamu kuna mazingatio makubwa kumjua Mwenyezi Mungu. Lengo kuu la kumtambua ni kuzingatia katika viumbe vyako ni kumjua yeye ili kumthamini, kwani tukimthamini tutamuabudu haki ya kumuabudu na hilo ndio lengo kuu la kuumbwa majini na binadamu.
قال تعالى : {وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ}    [الذاريات: 56].
 Mola (Subhaanahu wa Taala) Amesema: {{Na sikuumba na majini na binaadamu isipokuwa waniabudu}}. Napenda kusema kwamba Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) ndiye aliyeumba ulimwengu wote na viumbe vyote bila usaidizi wa mtu yoyote na yeye ndiye anayeupeleka ulimwengu huu. Kwa hivyo,  Yeye ndiye anayestahiki ibada kwa sababu hakuna yoyote aliyemsaidia katika uumbaji. Ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa kuumba na anaupeleka ulimwengu aliomba anavyotaka na wala haulizwi kwa analofanya bali viumbe ndio watakaoulizwa katika vitendo vyao.
Ndugu katika imani! Jueni ya kwamba viumbe vyote ambavyo vinapatikana ulimwenguni havijileti vyenyewe bali Mwenyezi Mungu aliyetukuka ndiye aliyeviumba viumbe hivyo.
قال تعالى : {أَمْ خُلِقُوا مِنْ غَيْرِ شَيْءٍ أَمْ هُمُ الْخَالِقُونَ * أَمْ خَلَقُوا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بَل لَا يُوقِنُونَ }   [الطور: 36:35].
 Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amesema kwenye Kitabu Chake: {{ Au  mumeumbwa kwa kisichokuwa kitu au nyinyi ndio waumbaji.  Au nyinyi ndio  mlioumba mbingu na ardhi bali wao hawana yakini}}.  Kulingana na Aya hizi  zinaonesha kwamba ulimwengu haukujiumba wenyewe na haukuwa kiumbe ambacho hakikumbwa wenyewe na kitu bali lazima tena kuna aliyeumba ulimwengu huu na akasimama kwa jambo lake (huo ulimwengu) naye si mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) hakuna Muumba asiyekuwa Yeye wala Mola asiyekuwa Yeye.
Enyi waumini! Lau mtaambiwa kuna jumba kubwa la ghorofa lililokamilika,  halina kasoro yoyote, ya kwamba limejijenga lenyewe mtaamini? Bila shaka hili ni jambo lisilowezekana kabisa. Na lau inasemekana kuwa jumba kubwa la ghorofa limepatikana ghafla mtaamini? sina shaka kwamba mtasema haiwezekani. Kwa hivyo,  huu ulimwengu ulio mpana uliokwenda juu na chini. Haiwezekani kabisa kujileta wenyewe na haiwezekani kabisa kujitokeza ghafla bali ni lazima kuna aliyeuleta ulimwengu  huu ambaye ni Mjuzi Muweza naye ni Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala).
Tujue ya kwamba hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)  katika kutudhalilishia ardhi na vilivyomo humo. Kwa hivyo, ni lazima kwa kila Muislamu kushukuru neema kubwa za Mwenyezi Mungu Alizotuneemesha Allah Mola wa viumbe vyote. Akipenda Mwenyezi Mungu tutabainisha suala la kuzishukuru neema za Mwenyezi Mungu katika khutba ya pili.
Enyi waumini! mcheni Allah (Subhaanahu wa Taala) na kumshukuru kwa uongofu aliotupa na aliyotufundisha yale ambayo tulikuwa hatujui katika mambo yaliyo na maslahi katika Dini yetu na kutujuza mambo yasiyofikiwa na akili zetu na ambayo haifungamani na  na maslahi yetu hali ya kuwahurumia nyinyi na hamkupewa ilimu isipokuwa kidogo.
Mwenyezi Mungu Aliyetuelimisha vipi alianza kuumba huu ulimwenguni,  na ilimu hii huwezi kuipata mpaka kupitia Mtume rehma na amani zimfikie. Na yoyote atakayetaja chochote kuhusu jinsi ya kuumbwa mbingu na ardhi,  hakika ni  wajibu tulinganishe na mafunzo walio kuja nayo Mitume ikiafikiana na vile walivyotufundisha Mitume,  basi itakubaliwa,  na ikienda kinyume na maelezo ya Mitume haikubaliwi na ikiwa Mitume hawakubainisha basi sisi itabidi tulinyamazie suala hilo wala  haifai kabisa kutia ufundi wetu mpaka itubainikie kuwa ni haki au ni batili.

Tunamshukuru Mola aliyetukuka. Rehma na amani zimfikie Mtume wetu Muhammad. Ama baada ya  kupeleka shukrani  kwa Mwenyezi Mungu na kumtakia rehma na amani Mtume Muhammad. Tumegusia katika khutba ya kwanza yanayohusiana na dalili za kumjua Allah katika viumbe vyake, vile vile kubainisha ukubwa wa Mwenyezi Mungu na kustahiki kwake kuabudiwa peke yake, huku tukiangazia kudhalilishwa viumbe mbali mbali kwa maslahi ya wanadamu. Vilevile kulinganiwa watu kutumia viumbe hivi katika kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kumuabudu yeye peke yake. Katika khutba hii ya pili napenda kubainisha shukrani za wanadamu kwa Mwenyezi Mungu kwa neema tofauti tofauti.
Enyi ndugu katika uislamu! Shukrani ni kumsifu aliyekupa neema. Na shukrani kwa mtu inakusanya nguzo tatu muhimu, kiasi kwamba haiitwi shukrani kwa Mwenyezi Mungu mpaka zikamilike, nazo ni:
(1) Mtu kuitambua neema katika moyo wake.
 (2) Kuizungumza neema ile kwa ulimi wake.
 (3) Kuitumia neema ile katika kumtii Mwenyezi Mungu. Kwa ufupi kabisa tunaweza kusema kuwa shukurani inafungamana na moyo, ulimi na viungo vya mwanadamu vilivyobakia. Kazi ya moyo ni kuitambua neema ile ya kwamba inatoka kwa Mwenyezi Mungu  (Subhaanahu wa Taala) na kumpenda Mwenyezi Mungu. 
Na kazi ya ulimi ni kuitaja neema ile na kumsifu Mwenyezi Mungu kwa neema hiyo na viungo vilivyosalia kazi yake ni kuvitumia katika kufanya maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Tusisahau ya kwamba kuna faida anayoipata mwenye kumshukuru Mola na faida hiyo ni radhi zake Allah (Subhaanahu wa Taala).
قال تعالى {وَاللَّهُ أَخْرَجَكُمْ مِنْ بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ لَا تَعْلَمُونَ شَيْئًا وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ}    [النحل:78]
 Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala):  {{ Mwenyezi Mungu Amewatoa katika matumbo ya mama zenu hali ya kuwa hamjui chochote akawajaalia masikio, macho na moyo ili mumshukuru yeye}}.
Mtume wetu Muhammad ni mfano mzuri katika kumshukuru Mola (Subhaanahu wa Taala) kwa neema nyingi alizomneemesha yeye na viumbe vyote. Alikuwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)  akiswali mpaka ikivimba miguu yake akaulizwa: Wewe pia wafanya hivi na umeshasamehewa dhambi zako zilizotangulia na zitakazaokuja?. Akasema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam):  Je, basi siwi mja mwenye kushukuru]. Na imethibiti kwamba Mu’adh bin Jabal alifundishwa na Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie kukutaja na kukushukuru wewe na kufanya vizuri ibada yako].
Tunajua vyema kila wakati tukumbuke kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa  kutudhalilishia neema nyingi na fadhila zake ili tupate kumuabudu yeye peke yake hana mshirika. Bado anasisitiza katika suala hili la kushukuru neema za Allah kwa kutaja neema za Allah kwa wingi.  Anasema Hasan Al Baswariy: ‘ Tajeni neema hizi kwa kwa wingi kwani kufanya hivyo ndio kuzishukuru’.  Kwa hakika Mola Amemuamrisha Mtume wake na pia sisi kuzizungumza na kuzitaja neema tulizopewa aliposema (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى : {وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ}    [الضحى : 11]
{{ Na ama neema za Mola wako zizungumze}} [Adhuhaa: 11]
Mwisho wa khutba hii, nawausia na kujiusia nafsi yangu kutumia neema za Mwenyezi Mungu vilivyo,  kwani utumiaji wa neema vilivyo ni katika kushukuru neema hiyo. Kutumia macho inavyotakiwa ni kuishukuru neema hiyo kwani wako watu hawana neema hiyo ya macho,kutumia ulimi vizuri ni kushukuru neema hiyo ya ulimi. Neema ya mikono na miguu kuzishukuru neema hizi ni kuzitumia katika mambo ya kheri. Maneno haya tuliyoyataja yanatufundisha ya kwamba kila neema ina  namna yake ya kuishukuru.Tukimalizia neema ya chakula.
يقول الله تعالى : {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّهِ إِنْ كُنْتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ}    [البقرة : 172]
Mola (Subhaanahu wa Taala) Amesema: {{ Enyi mulioamini kuleni katika vizuri mulivyoruzukiwa na mumshukuru Allah ambaye mnamuabudu na kumtii}} [Al-Baqara : 172]. Pia Mwenyezi Mungu  (Subhaanahu wa Taala) Anasema:
وقال : {فَكُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّهُ حَلَالًا طَيِّبًا وَاشْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّهِ إِنْ كُنْتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ}
 [النحل : 114]
{{ Kuleni katika alivyowaruzuku Allah vilivyo halali vizuri na mushukuru neema za Mwenyezi Mungu ikiwa kweli mnamuabudu}}  [Al-Nahal : 144].

Mwisho
Tunamshukuru Mola Aliyetuwezesha kuyazungumza yanayohusiana na baadhi ya alama za kumjua Mungu kupitia viumbe vyake. Pia nimegusia kuhusu ukubwa wa Mungu na kwamba yeye Ndiye anayestahiki kuabudiwa.  Vilevile ni kuweza kuchambua suala la watu kumshukuru Mungu aliyetudhalilishia viumbe vyake,  na nimewakumbusha katika kutumia neema za Mungu alizotupa kwa kumuabudu yeye.
Mwisho kabisa tunamuomba Mwenyezi Mungu Atujaaliye miongoni mwa wenye kuzishukuru neema zake, na kupata radhi zake, na atujaaliye ni wenye kumcha na kumuabudu yeye mpaka mwisho wa uhai wetu na tuingie katika pepo yake. Na rehma na amani zimfikie Mtume Muhammad.


Thursday, August 29, 2013

بشار الأسد: سنقاوم العدوان الغربي


قال الرئيس السوري بشار الأسد إن بلاده ستدافع عن نفسها ضد العدوان الغربي، بينما تسعى الولايات المتحدة وبريطانيا لشحذ التأييد الدولي لخططهما لضرب سوريا.
في هذه الأثناء، انتهى اجتماع ممثلي الدول الخمس دائمة العضوية في مجلس الأمن التشاوري الذي عقد لبحث موضوع اصدار قرار جديد حول الوضع في سوريا.



وأفاد مراسل بي بي سي في واشنطن لقمان أحمد إنه لم يصدر أي بيان عن ممثلي الدول التي شاركت في الاجتماع

.
وتقول الولايات المتحدة وبريطانيا إن نظام الرئيس الأسد قتل مئات السوريين في هجمات شنها مؤخرا بالاسلحة الكيمياوية، ولكن دمشق تنفي هذه الادعاءات وتحمل المعارضة المسلحة مسؤولية الهجمات.
ويعكف فريق تابع للأمم المتحدة بالتحقيق في الهجوم.
ومن المقرر أن يفرغ فريق المفتشين الدولي من عمله يوم الجمعة، ويرفع تقريره إلى الامين العام للمنظمة الدولية بان كي مون السبت.
ولا يتضمن التفويض الذي يتمتع به الفريق تحميل أي من طرفي النزاع في سوريا مسؤولية الهجوم الذي وقع قرب العاصمة دمشق في الحادي والعشرين من الشهر الجاري وخلف 355 قتيلا على الأقل.

"رد موحد"

وكانت بريطانيا قد حثت أمس الاربعاء مجلس الأمن التابع للأمم المتحدة على اصدار قرار يسمح للدول الغربية باستخدام القوة المسلحة ضد سوريا، ولكن الطلب البريطاني لم يحظ بالدعم الضروري.
وعرقلت روسيا والصين في السابق صدور قرارات تخص الشأن السوري في مجلس الأمن، ويقول محللون إنه من المرجح ان يكرر البلدان ذلك في المستقبل.
وكانت المستشارة الالمانية انغيلا ميركل قد اجرت اتصالا هاتفيا بالرئيس الروسي فلاديمير بوتين في وقت سابق اليوم حثت خلالها روسيا على التعاون مع مجلس الأمن للتوصل إلى "رد فعل سريع وموحد" ازاء الوضع في سوريا.
ولكن مكتب رئيس الحكومة البريطانية قال في بيان إن بريطانيا ما زالت تتمكن من اتخاذ "اجراءات استثنائية بما فيها التدخل العسكري" لدواع انسانية حتى في حال اخفاق مجلس الامن في التوصل الى اجماع.
وسيصوت نواب مجلس العموم البريطاني في وقت لاحق اليوم على مشروع قرار يطالب بالتدخل العسكري في سوريا، وينص على ان "الموضوع يجب ان يتابع من خلال الامم المتحدة الى اقصى مدى ممكن."
ومن المتوقع ان يطلع مسؤولو الادارة الامريكية كبار زعماء الكونغرس سرا في وقت لاحق على الادلة المتوفرة التي تثبت تورط نظام الاسد باستخدام الاسلحة الكيمياوية.
ولكن الرئيس السوري أخبر وفدا من النواب اليمنيين يقوم بزيارة لدمشق ان سوريا ستدافع عن نفسها ضد أي عدوان قد تعرض له، حسبما اوردت وكالة سانا الرسمية للانباء.
وقال الرئيس السوري إن التهديدات الغربية بضرب بلاده لن تزيده الا عزما على مقاومة المعتدين، حسبما نقل عنه الاعلام الرسمي.
ونقلت الوكالة عن الرئيس الأسد قوله "إن سوريا بشعبها الصامد وجيشها الباسل ماضية ومصممة على القضاء على الإرهاب الذي سخرته وتدعمه إسرائيل والدول الغربية خدمة لمصالحها المتمثلة بتقسيم المنطقة وتفتيت واخضاع شعوبها."
وقالت تقارير من دمشق في غضون ذلك إن كبار القادة العسكريين اخذوا بالابتعاد عن المقار والمباني التي يعتقد انها ستكون هدفا للغارات الغربية.
كما غادر الكثيرون من سكان العاصمة خوفا من هجوم مرتقب

احمد محب الدين الأخبار جديد/احب الله ورسوله

حبّ الرسول صلّى الله عليه وسلّم

قال عليه والصلاة والسلام <<من أحبّ سنّتي فقد أحبّني ومن أحبني كان معي في الجنة>>وقال تعالى<<قل إن كنتم تحبّون الله فاتبعوني يحبب كم الله و يغفر ذنوبكم>>

Popular Posts