Followers

Thursday, May 9, 2013

WACHUMBA KUZOEANA TABIA KABLA YA NDOA..

Hii ni ada na desturi ambayo inaishi na kuchukua nafasi katika baadhi ya familia katika jamii zetu. Binti anapoposwa na kijana na kufungwa kile kinachoitwa “pamvu”, kitu ambacho uislamu haukitambui. Pamvu ni kile kitu ambacho hupelekwa kwa wazazi wa binti ili kufunga mlango wa posa na kuonyesha kuwa tayari binti yao amekwishachumbiwa. Baada ya kufungwa kwa pamvu, kijana wa kiume huwa na fursa ya kufika nyumbani kwao na binti na kupokelewa kwa mapana na marefu. Akapikiwa, akala na kunywa kwa raha na furaha. Akawa na uhuru wa kukaa peke yake na binti faraghani wakazungumza na kucheka kwa furaha.

Zaidi ya yuote hayo, kijana anaweza kumchukua binti na kwenda kutembea nae kokote apendako. Haya yote hufanyika chini ya kivuli ya kile kinachoitwa “kuzoeana kitabia” kabla ya kuishi pamoja kaitka maisha ya ndoa. Desturi hii na yaliyomo ndani ya desturi hii hayakubaliki na hayana nafasi kabisa katika uislamu. Haijuzu kwa mujibu wa sheria mchumba kuzungumza na mchumba wake hata kwa njia ya simu seuze kutokana na matembezi kukaa nae faraghani bila ya kuwepo baina yao maharimu wa mtoto wa kike kama vile Babu, baba au kaka. Kisheria kijana wa kiume anaruhusiwa kumuangalia mtoto wa kike uso na mikono anapotaka kumposa bila ya kumgusa na hili hufanyika mbele ya wazazi wa pande zote mbili. Hekima ya mkutano huu na kuonana huku ni kuwapa vijana hawa fursa ya kumuona yule atakayekuwa mwenza wake katika maisha na pia kuamua kukubali kuoa au kuolewa ama kukataa. Hili tu ndilo linaloruhusiwa na sheria. Baada ya kuonana huku, wachumba hawa hawana ruksa ya kuzugumza au kuonana tena mpaka watakapooana kwa misingi na taratibu zote za kisheria ambapo binti sasa hutambulika kama mke wa mtu na kijana kama mume wa mtu.

Yaliyozuliwa na watu kinyume na utaratibu huu tuliowekewa na sheria ni HARAMU isiyokubalika na yenye adhabu kali mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kutokana na athari yake mbaya kwa jamii. Uzoefu umeonyesha na kuthibitisha kuwa ada hii ya “kuzoeana kitabia” katika hatua ya uchumba imefanya ndoa nyingi zisifungwe. Kijana wa kiume akishapata nafasi ya kukutana na binti na kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa, matokeo yake ni kumtia mimba mtoto wa kike. Baada ya mimba hupatikana mojawapo ya mambo mawili haya:
1. Ama kijana ataukubali mzigo wake ule, akalea mimba na wakaja kufunga ndoa baadaye wakiwa na mtoto wa haramu/njeya ndoa.
2. Au ataukana mzigo ule uwa si wake na hivyo kumuacha mtoto wa kike ahangaike na kuteseka pake yake naye akashika nia kwenda kuendeleza fisadi na uharibifu wake mahala pengine.
Sasa ili ili kuzuia haya yote yasitokee, ndio uislamu ukaamua kuufunga kabisa mlango huu wa fisadi na uharibifu kwa maslahi yetu wenyewe. Tufuatane pamoja katika hadithi ifuatayo ya Bwana Mtume, ili tuone jinsi uislamu ulivyoharamisha mwanamume kumuangalia mwanamke ajnabia (wa kando na kando – yaani si maharim wa mwanamume yule):-
Imepokelewa na Umu Salamah – Allah amuwiye radhi – amesema: Nillikuwa mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu – Rehema na Amani zimshukie - akiwa na Maimunah (mkewe), akaja/akaingia Abdullah Ibn Ummi Maktuum (kipofu). Na hili lilikuwa baada ya kushuka aya za hijabu, akatuambia Mtume; “Jificheni nae,” tukamwambia; Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je, yeye si kipofu ? Hatuoni na wala hatujui ? Mtume akatuambia; “Je! Na nyinyi ni vipofu, hamumuoni ?” Abuu Daawoud na Tirmidhiy.
Haya, ikiwa huyu ni kipofu haoni na bado Bwana Mtume anawaamrisha wakeze waondoke mbele yake, wasimuone kwa kuwa ni mwanamume. Vipi leo, vijana wetu wa kike na wa kiume ambao wote wawilli si vipofu wanaona wakae pamoja wakitazamana na kuzungumza kwa tabasamu pevu na vicheko vya furaha. Ruksa hii na uhalali huu wanaupata wapi na il-hali Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie – anatuonya; “Asikae faragha mmoja wenu pamoja na mwanamke ila (atakapokuwa mwanamke huyo) pamoja na maharimu wake.” Bukhaary na Muslim. Bwana Mtume, anatukataza katika hadithi hii kukaa faraghani (yaani mwanamume na mwanamke peke yao tu) pamoja na mwanamke ambaye si maharimu yetu. Mwanamke asiye maharimuni yule ambaye kisheria hakuna kizuizi wala kipingamizi chochote kwetu kumuoa. Haya ni maelekezo, maagizo na amri ya Bwana Mtume ambayo sisi kama waislamu tunapaswa bali imetulazimu na kutuwajibikia kuifuata na kiutekeleza mara moja bila ya kuzitii na kuzifuata amri na maelekezo ya Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie. Na ni vema ikatiwa akilini kuwa kumtii na kumfuata Bwana mtume ni amri ya mwenyezi mungu mtukufu, tusome na tutekeleze. “………………NA ANACHOKUPENI MTUME (ANACHOKKUAMRISHENI BASI POKEENI), NA ANACHKUKATAZENI JIEPUSHENI NACHO ………………...” (59:7)
Tusome tena kwa mazingatio na kasha tufuate: “SEMA: IKIWA NYINYI MNAMPENDA ALLAH, BASI NIFUATENI; (HAPO) ALLAH ATAKUPENDENI NA KUKUGHUFIRIENI MADHAMBI YENU” (3: 31)
Aya hizi na nyinginezo ndizo zinazotulazimisha kumfuata na kumtii Bwana Mtume katika maelekezo, maamrisho au makatazo yote atakayotupa kwa maslahi na manufaa yetu wenyewe. Kwa bahati nzuri Mwenyezi Mungu mtukufu ametukamilishia dini hii kupitia kwa Mtume wake. Dini hii haikusaza lolote lenye manufaa na faida kwetu katika maisha haya ya dunia na yale yajayo ya akhera ila imetueleza jambo hilo na namna ya kulitekeleza. Kadhalika haikuacha lolote lile lenye madhara na kasoro kwetu ila imetuabainishia na kututahadharisha nalo na kutuonya tusilitende au kulifuata. Sasa ikiwa dini hii imekamilika na kila jambo linalohusu nyanja mbalimbali za maisha yetu ya kila siku limekwisha bainishwa na kuwekewa utaratibu wake wa kulitekeleza au kulienda. Kwenda kinumbe na utaratibu huo, kunamaanisha:
1. Dini hii haikukamilika kama anyavyosema Mwenyezi Mungu mtukufu
2. Kumkadhibisha mwenyezi mungu na Mtume wake, jambo ambalo ni maasi.
3. Sisi tunayo mamlaka na madaraka ya kujitungia sheria kinyume na sheria za Mwenyezi Mungu mtukufu.
4. Tuna uamuzi na khiyari ya kufuata ama kutokufuata sheria/ hukumu za Mwenyezi Mungu mtukufu.
5. Sheria na taratibu zetu tulizojipangia ni bora na zinafaa zaidi kuliko zile za mwenyezi mungu
6. Kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Kwa ujumla kutokumfuata Bwana Mtume ni kumhalifu na kumpinga, jambo ambalo Mwenyezi Mungu mtukufu ametukataza tusome na tuzingatie: “ ................BASI WAJIHADHARI WALE WANAOKAIDI AMRI YAKE USIJE UKWAPATA MSIBA AU UKAWAFIKA ADHABU IUMIZAYO.” (24: 63)
Leo kwa sababu ya ukaidi na kukhalifu kwetu amri ya Bwana Mtume – Rehema na amani zimshukie- na tukaruhusu mila na desturi hii ya kuzoeana tabia iitawale jamii yetu, tayari tumeshafikwa na kupatwa na msiba. Msiba huu si mwingine bali ni wimbi na janga la watoto wa haramu/nje ya ndoa na pengine hata hawa tuwaitao leo watoto wa mitaani ni natija ya kuendekeza na kufuata mila tamaduni n a desturi hizi mbaya. Taathira na athari na ada hizi potofu ziko wazi na bayana kwa kila mmoja wetu. Haya sasa ndugu zanguni waislamu, tuamue ama kumfuata Bwana Mtume tupate salama au kutokumfuata na kuendeleza mila tamaduni na ada zetu wenyewe tufikwe na msiba na adhabu kali iumizayo. Mwisho ni vema tukakumbuka na kukiri kuwa hizi ni hasaha za wiki, kunasihika au kutonasihika huo ni uamuzi wako wewe mwenyewe.

HAYA NDIO MAFUNZO YA NDOA YALIO SAHIH

MAFUNZO YA NDOA KUTOKA KWA  FATMA BINT RASULU-LLAH.

Ilikuwa katika mwaka wa 2AH. Imam Ali (ra) alipomkabili Mtume SAAW kwa lengo la kumchumbia Bibi Fatma ( ra) na kumueleza :
‘Ewe Mtume wa Allah, umenilea mimi k...ama mwanao mwenyewe. Ulinijaza na zawadi zako, ukarimu wako na wema wako. Nimepewa nawe kila kitu katika maisha yangu. Sasa naomba wema mmoja zaidi kutoka kwako’.
Mtume SAAW alifahamu kwa kina lengo la Imam Ali ra. na akawa hana budi ila kumueleza mwanawe Bi Fatma: Kwamba Ali anaomba uchumba wake, na kumtaka jibu lake. Hata hivyo Fatma Zahra ra. akabakia kimya bila ya jibu lolote, na Mtume SAAW akatafsiri kimya chake ni kukubaliana na posa hiyo. Akarudi Mtume SAAW kumjuulisha Ali ra. kwamba ombi lake limekubaliwa. Na akamtaka aanze kufanya matayarisho ya harusi.
Miezi miwili baada ya ushindi wa Waislamu katika vita vya Badr, Imam Ali RA. na Bi Fatma
Zahra Binti wa Mtume SAAW walifunga ndoa. Maandalizi ya harusi yakafanywa, na Mtume SAAW akamkabidhi shughuli yote ya harusi kwa upande wa wanawake kusimamiwa na ‘nyanya’ yake Ummu Ayman.
Mwanzoni mwa mwezi wa Dhul-hijjah katika mwaka wa 2AH Mtume aliwaalika masahaba wa Muhajirina na Answar kuhudhuria katika shughuli ya harusi. Mtume SAAW mwenyewe akatowa hotuba ya ndoa, akawaozesha na akawatangaza rasmi Ali ra. na Bibi Fatma ra. kwamba tayari wameshakuwa mke na mume. Wageni waalikwa waliandaliwa na Mtume SAAW karamu ya nyama ya kondoo, mikate na kinywaji cha mchanganyiko wa tende na maziwa (juice). Waislamu wakala, wakanywa, wakafurahi na wakampongeza Mtume SAAW na maharusi katika tukio hili tukufu lililojaa baraka tele. Na Mtume SAAW akaomba baraka za Allah ziwe juu yao wote.
Siku chache baadae, ndani ya mwezi wa Dhul-hijjah, Bibi Fatma Zahra akaiga nyumba yao aliyokuwa akiishi na kupelekwa nyumbani kwa mumewe. Bibi Fatma akasaidiwa na Baba yake kupanda juu ya ngamia maalum kuelekea nyumbani kwake.
Katika siku hiyo, mji wote wa Madina ulijaaa furaha, nderemo, vifijo, hoi hoi na kuririma kwa ‘takbeer’. Salman al Farsi alishikilia hatamu za ngamia wa Bibi Harusi (ambae alikuwa ngamia jike wa Mtume SAAW) akaongoza msafara huku akisoma aya tukufu za quran, Mtume SAAW nae alitembea upande mmoja wa msafara, na upande wa pili alikuwepo Ami yake Hamza RA. (Bwana wa Mashahid).
Masahaba jumla na vijana wapanda farasi wa Bani Hashim walipanda farasi kama wasindikizaji wa bibi harusi. Panga zao zikiririma na kumeremeta na kunyanyuliwa juu kwa furaha isiyo na kifani. Nyuma yao wanawake wa Muhajirina na Answar wakiimba qasida nzuri nzuri katika maandamano yaliyozunguuka Msikiti wa Mtume (Masjid Nabawi) na yakafikia kilele chake chini ya nyumba ya maharusi. Baada ya kushuka bi harusi juu ya ngamia wake, Mtume SAAW akauchukua mkono wa bi Fatma ra. na akauweka juu ya mkono wa mumewe, akasimama juu ya kizingiti cha nyumba yao na kuwaombea dua:
‘Ewe Allah ninawaweka Ali na Fatma, waja wako wanyenyekevu, kwenye ulinzi Wako. Uwe Wewe ndio Mlinzi wao. Wabariki hawa. Kuwa radhi nao, na uwape neema Zako zisizo na mipaka, huruma, na fadhila Zako bora juu yao. Uifanye ndoa yao kuwa yenye matunda, na uwafanye wote imara katika upendo Wako, na ibada zako.’
Pamoja na mafunzo mengi yaliyomo katika tukio hili kubwa. Hata hivyo, funzo moja kubwa na muhimu linadhihirika wazi wazi. Namna Mtume SAAW alivyoondosha fikra chafu ya uaswabia na ubaguzi kivitendo kwa kuwashirikisha mstari wa mbele kikamilifu masahaba wasiokuwa waarabu katika tukio hili. Hilo hudhihirika katika hali mbili. Kwanza, alimpa jukumu nyanya yake Ummu Ayman kusimamia shughuli ya harusi kwa upande wa wanawake. Huyu ni mwanamke mwenye asili ya kihabeshi (Ethiopia) awali aliyekuwa mtumwa wa baba yake Mtume SAAW, na baadae Mtume akampa uhuru wake. Ikumbukwe kwamba Ummu Ayman kwa kauli ya Mtume SAAW ni mwanamke wa peponi, na ndie mwanamke aliyekuja kuolewa na Zaid bin Harith ra. na kumzaa shujaa katika mashujaa wakubwa wa kiislamu. Jemadari Usamah bin Zaid ra. Sahaba ambae pia Mtume SAAW alimpa jukumu la ujemadari wa jeshi la kiislamu bila ya kuzingatia kabila wala nasabu yake, na akawaacha wenye makabila makubwa ya kiqureish na waarabu jumla katika kubeba jukumu hili.
Katika hali ya pili, Mtume SAAW alimchagua Salman Al Farsi kuongoza msafara wa bi harusi bila ya kumzingatia kwamba yeye si muarabu. Bali alimpa hadhi hiyo kwa moyo mkunjufu bila ya kuonyesha hisia yoyote ya kibaguzi. Salman ra. awali kabla ya kusilimu aliwahi kuuzwa kuwa mtumwa wa yahudi katika viunga vya Madina, na akakombolewa baada ya kusilimu kwake. Uislamu ukampandisha daraja ya juu hadi siku moja ‘Muhajirina’ na ‘Answar’ walipozozana juu ya haiba yake, wengine wakisema Salman ni ‘Answar’ na baadhi wakisema ni katika ‘Muhajirina’. Mtume akaondosha mzozo wao huo kwa kusema: ‘Salman ni katika Ahul-bayt yangu’.
Leo umma wa kiislamu baada ya kuanguka Khilafah na kufitinishwa na makafiri umesibiwa kwa kiasi kikubwa na uchafu, uovu na maradhi ya dhambi kubwa ya uaswabia na ubaguzi, kuanzia wa kimaeneo, kikabila, rangi, nchi nk. Dhambi ambayo Mtume SAAW aliikemea wazi kwa ukali kwamba ni ‘uvundo’ na tujiepushe nao. Na badala yake Uislamu unatuamrisha kwamba kipimo pekee cha kumzingatia mtu ni Uislamu na ucha Mungu wake.Tukumbuke kauli yake Mtume SAAW aliposema:

‘Kwa hakika watu wote tangu zama za Adam mpaka leo wako sawa kama meno ya kitana, na hakuna ubora juu ya Muarabu kwa asiyekuwa Muarabu, wala ubora wa Mwekundu kwa Mweusi, ila kwa ucha Mungu.’(Mustadarak- ul-Wasa’il)

KISA CHA BILAAL

KISAA CHA BILAL....MUADHINI WA MWANZO KATIKA UISLAMU.
Bilaal Bin Rabaah (Radhiya Allaahu 'Anhu)

‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa kila linapotajwa jina la Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) akisema;

"Bwana wetu aliyemkomboa Bwana wetu". Akimkusudia Bilaal bin Rabaah (Radhiya Allaahu ‘anhu). Wanasema wanavyuoni kuwa; Unapomsikia ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akimwita mtu 'Bwana wetu', basi tambua ya kuwa huyo ni mtu adhimu.

Imeandikwa katika Siyar al-A’alaam an-Nubalaa kuwa Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye asili yake ni Mhabeshi (mu-Ethiopia), alikuwa mweusi sana, mwembamba, mrefu na mwenye nywele ndefu.

Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa mtumwa wa kabila la Bani Jumhi, na maisha yake yalikuwa kama mtumwa yeyote wa kawaida pale Makkah, hakuwa na uwezo wala uhuru wowote isipokuwa kuwatumikia mabwana zake watu wa kabila la Al-Jumhi. Baadaye alimilikiwa na Umayyah bin Khalaf peke yake ambaye pia anatokana na kabila hilo la Al-Jumhiy, na mama yake Bilaal na jina lake lilikuwa Hamaamah, naye pia alikuwa mtumwa wa kabila hilo la Al-Jumhi.
Mara baada ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) kuanza kuwalingania watu katika dini ya Kiislam kwa jahari, Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akawa anasikia habari za dini hii mpya na habari za Mtume huyu mpya (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), na habari hizo zilikuwa zikimfurahisha sana kila anapozisikia hasa kutoka kwa Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliyekuwa kila anapopata fursa akimwendea Bilaal na watu wengine pia na kuwahadithia juu ya dini hii.
Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasilimu mikononi mwa Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliyekuwa akifanya kazi kubwa sana tokea siku ya mwanzo katika kuwalingania watu katika dini hii tukufu.
Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa akiwalingania watu waliokuwa huru na akafanikiwa kuwasilimisha watu watukufu wakiwemo watano katika wale kumi waliobashiriwa Pepo nao ni ‘Uthmaan bin ‘Affaan, Az-Zubayr bin ‘Awaam, ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf, Sa’ad bin Abi Waqaas na Twalha bin ‘UbayduLlaah (Radhiya Allaahu ‘anhu) na wengi wengineo, na alikuwa pia akiwalingania watu wasiokuwa huru kama vile Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliyekuwa rafiki yake Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) tokea hata kabla ya Uislam, na wengineo pia.
Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) alifuatana na Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) mpaka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) na kuzitamka shahada mbili mbele yake, na kwa ajili hiyo akawa miongoni mwa watu wa mwanzo kuingia katika dini hii tukufu.

Ahadun Ahad

Uislam ulipoanza kuenea katika mji wa Makkah, na baadhi ya Ma-Quraysh kutambua kuwa watumwa wao walikuwa wakiingia katika dini hii mpya kwa siri tena kwa wingi, wakaanza kuwatesa kwa kuwaonjesha kila aina ya adhabu.
Miongoni mwa Waislam wa mwanzo waliokuwa watumwa na wakapata adhabu kubwa kutoka kwa washirikina wa Makkah, ni Sumayyah, mama yake ‘Ammaar aliyekuwa mke wa Yaasir (Radhiya Llaahu ‘anhum) waliokuwa na asili ya Ki-Yemen.
Walikuwa wakiadhibishwa sana, na kila Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) anapopita nje ya nyumba yao alikuwa akiwaambia;

"Kuweni na subira enyi watu wa nyumba ya Yaasir, kwani hakika waadi wenu ni Pepo".

Sumayyah (Radhiya Allaahu ‘anhu) alifariki akiwa anateswa na akapata bahati ya kuwa Shahid wa mwanzo katika dini ya Kiislam.
Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) naye alipata sehemu kubwa ya adhabu, kwani bwana wake Umayyah bin Khalaf aliyekuwa mtu khabithi sana, alikuwa akimtoa nje wakati wa jua kali linalounguza mwili na kumvua nguo zake kisha anamlaza juu ya mchanga wa jangwani unaounguza na kumwekea jiwe kubwa sana juu ya kifua chake huku akimwambia;

"Utabaki hivyo hivyo mpaka ufe isipokuwa kama utamkanusha Muhammad na kumtukana kisha urudi tena kuiabudu miungu yako Lata na Uzza".

Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa akimjibu kwa kusema;

"Ahadun Ahad".(Mmoja tu, mmoja tu)

Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliwahi kuulizwa;

"Kwa nini ulikuwa ukiendelea kusema hivyo "Ahadun Ahad".(Mmoja tu, mmoja tu), na hali unajua kuwa maneno hayo yanawaghadhibisha na kwa ajili hiyo wao wataendelea kukuadhibu?"

Akajibu;

"WaLlaahi kama ningekuwa nalijuwa neno jingine linaloweza kuwakasirisha zaidi kuliko hilo, basi ningelilitamka".
Hakika neno; "Ahadun ahad", lilikuwa likimkera sana Umayyah na kila anapolisikia alikuwa ghadhabu zinampanda na akawa anampiga Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) kama mwendawazimu.

Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akawa anaendelea kuadhibishwa na yeye alikuwa akiendelea kustahamili huku akiendelea kulitamka neno lake hilo 'Ahadun ahad', mpaka Umayyah mwenyewe akashindwa, kwani kila siku baada ya kumtesa wakati wa mchana, alikuwa akimfunga kamba shingoni na kuwakabidhi watoto wadogo na wendawazimu waliokuwa wakimburura Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kuzunguka naye mjini Makkah, huku wakimzomea na kumpiga, na yeye alikuwa akiendelea kusema'

"Ahadun ahad" (Mmoja peke yake mmoja peke yake).

Na Amchae Mungu

Siku moja Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipokuwa akipita akamuona Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika hali ile, akamwambia Umayyah;
"Humuogopi Mungu wewe, unamtesa namna hii maskini huyu, mpaka lini utaendelea hivi?'

Umayyah akamwambia;

"Wewe ndiye uliyemharibu huyu, kwa hivyo sasa muokoe wewe kama unaweza".
Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamnunua kwa wakia tano na akamuacha huru kwa ajili ya kutaka Radhi za Mwenyezi Mungu, na kabla ya hapo Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa keshawanunua watumwa sita na kuwaacha huru, na Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa wa saba.
Bilaal akaepukana na adhabu, na Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) bila shaka akapata ujira mkubwa kutoka kwa Mola wake (Subhanahu wa Ta’ala).

Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliendelea na kazi hiyo ya kuwanunua watumwa na kuwaacha huru, na Maulamaa wa tafsiri wamekubaliana kuwa Mwenyezi Mungu Alimsifia Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika Aya ya 17 katika Suratul Layl pale Aliposema;

“Na amchaye (Mwenyezi Mungu) ataepushwa nao (Moto).
Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.

Na hali ya kuwa hakuna yeyote aliyemfanyia ihsani ili awe anamlipa.

Isipokuwa (anafanya haya) kwa kutaka radhi ya Mola wake Mtukufu.
Basi atapata la kumridhisha.”

Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) akaondoka hapo pamoja na Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kwenda mpaka kwa Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), na alipokuwa akiondoka naye, Umayyah akamwambia;
"Ondoka naye hapa, Naapa kwa Laata na Uzza, kuwa ungekataa kumnunua kwa wakia tano, basi hata kwa wakia moja tu ningekuuzia".

Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamjibu;

"WALLAHI, LAU KAMA UNGETAKA NIMNUNUE KWA WAKIA MIA, BASI NINGEKUPA".

Muadhini Wa Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wa Sallam) Wa Mwanzo

Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alifurahi kupita kiasi alipomuona Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akiwa huru, na akawabashiria Waislam juu yake na akamfanya baadaye kuwa ni Muadhini wake wa mwanzo katika Uislam, kwani Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa na sauti nzuri sana na Mwenyezi Mungu Akaijaalia sauti hiyo iwe yenye kuleta taathira ndani ya nyoyo za kila mwenye kuisikia.
Mji wa Madiynah ulikuwa ukitulia pale anapoadhini Bilaal, na watu walikuwa wakikimbilia Msikitini mara baada ya kuisikia sauti yake (Radhiya Allaahu ‘anhu), na Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) pia alikuwa akimpenda sana Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) na akistarehe sana kila anapoisikia sauti yake, na hasa anapoadhini, na alikuwa akiwatanguliza Bilaal na watu masikini miongoni mwa Waislam kabla ya matajiri na alikuwa akikaa nao muda mrefu zaidi na alikuwa akiwakirimu.
Siku ile Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alipoingia na majeshi yake kuuteka mji wa Makkah, na baada ya kusafishwa msikiti wa Makkah kutokana na masanamu yaliyokuwa yamejaa humo, aliingia Msikitini na kuufunga mlango nyuma yake akiwa yeye na Bilaal na ‘Usaamah (Radhiya Allaahu ‘anhu) peke yao ndani ya Msikiti na katika riwaya nyingine aliingia pia na ‘Uthmaan bin Twalha (Radhiya Allaahu ‘anhu), na kuwaacha watu wa kabila lake na watu wa nyumba yake pamoja na Maswahaba wakubwa wakubwa kama vile Abu Bakr, ‘Umar, ‘Uthmaan na ‘Aliy (Radhiya Llaahu ‘anhum) nje ya Msikiti.

Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akamtaka Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) apande juu ya Al-Ka’abah na kuadhini, na Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akafanya kama alivyoamrishwa, na jambo hili liliwakasirisha sana baadhi ya Ma-Quraysh, akasema Itab bin Usayd;
"Nashukukru baba yangu hajaishi mpaka akaweza kuyaona haya! Hivyo Muhammad hajapata mwengine wa kutuadhinia isipokuwa kunguru huyu mweusi?"
Bilaal na ‘Usaamah (Radhiya Allaahu ‘anhu) wote walikuwa watumwa kabla ya Uislam.
Na katika hadithi, siku moja Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alimuuliza Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu);
"Nielezee juu ya ‘amali njema kabisa unayoitenda, kwani nimesikia sauti ya viatu vyako vikiwa mbele yangu Peponi?"

Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu;

"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu sijafanya ‘amali yoyote niliyoiona kuwa ni bora kwangu isipokuwa kawaida yangu mimi kila nikitawadha huswali kadiri ninavyojaaliwa kuswali”.
Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akamwambia;

“Hilo ndilo lililokufikisha”.
Al-Bukhaariy

Baadhi Ya Sifa Zake

Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) hakuwa akimiliki sauti nzuri tu, bali alikuwa pia shujaa na alishiriki katika vita vyote walivyopigana Waislam, vile alivyoshiriki Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ndani yake na pia vile asivyoshiriki, na alikuwa mpiganaji mzuri sana. Alishiriki katika vita vya Badr na kupigana kwa ushujaa mkubwa, na yeye ndiye aliyemuua Umayyah bin Khalaf baada ya kutekwa na Waislam katika vita hivyo.
Ingawaje daraja yake ilikuwa mbele ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) na mbele ya Maswahaba wake (Radhiya Allaahu ‘anhu), lakini Bilaal hakuwa mtu mwenye kujiona wala kujivuna wala mwenye kutakabari, bali alikuwa mnyenyekevu kwa Waislam wenzake, huku akiichunga nafsi yake, jambo lililomfanya aheshimiwe zaidi na Maswahaba wenzake (Radhiya Allaahu ‘anhu).

Kuposa Kwake

Katika kitabu cha Siyar al-A’alaam an-Nubalaa cha Imaam Adh-Dhahabiy na katika Al-Bidaayah wan-Nihaayah cha Ibn Kathiyr imeandikwa kuwa; Siku ile alipokwenda yeye na ndugu yake kuposa katika nyumba moja ya watu wa kabila la Ki-Yemen, aliwaambia;
"Mimi ni Bilaal na huyu ni ndugu yangu Abshan, sisi ni watu wa Uhabeshi, tulikuwa tumepotoka na Mwenyezi Mungu Akatuongoza, na tulikuwa watumwa na Mwenyezi Mungu Akatukomboa. Kama mtakubali kutuozesha watoto wenu, 'AlhamduliLlaah' tunamshukuru Mwenyezi Mungu, na kama mtatukatalia basi 'Allaahu Akbar' Mungu ni Mkubwa".
Bilaal na ndugu yake waliowa katika nyumba hiyo.

Siku Aliyofariki Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wa Sallam)

Maisha yake yote Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa pamoja na Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), tena karibu naye. Kila siku akimuadhinia huku Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akifurahishwa na sauti yake na yeye kwa upande wake alibahatika kuweza kuyatia nuru macho yake kila siku kwa kumuona kipenzi cha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) asubuhi na jioni, mchana na usiku, mpaka siku ile Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alipoisalimisha roho yake kwa Mola wake.
Siku ile, Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliingia chumbani kwa Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) kwa ajili ya kumtizama kipenzi chake kwa mara ya mwisho, na Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa amefunikwa na kulazwa juu ya tandiko lake, na Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akawa anamtizama huku machozi yakimlenga. Aliposhindwa kuimiliki nafsi yake akaanza kulia kwa kwikwi.na baada ya muda akatulia, kisha akasogea mbele yake na kumswalia. Baada ya kumswalia akatoka chumbani huku machozi yakiwa yanaendela kumiminika.
Usiku uliofuata Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) hakuweza kupata usingizi hata kidogo kutokana na huzuni iliyomjaa moyoni mwake, na hasa kila anapokumbuka kuwa hatoweza kumuona tena Swahibu yake kama alivyokuwa akimuona kila siku mbele ya macho yake. Akawa katika hali hiyo usiku kucha mpaka ulipokaribia wakati wa Swalah ya Alfajiri alipotoka na kuelekea Msikitini kama kawaida yake kwa ajili ya kuadhini, na ulipoingia wakati wa adhana akaanza kuadhini;

"Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, Allaahu Akbar Allaahu Akbar. Ash-hadu an laa ilaaha illa Llaah, Ash-hadu an laa ilaaha illa Llaah…" Alipotaka kutamka;
"Ash-hadu anna Muhammadan Rasuulu Llaah", Akashindwa, - pumzi zilimkaba, sauti ikashindwa kutoka, na aliposhindwa kuimiliki nafsi yake, machozi yakaanza kummiminika, na watu waliposikia kukatika kwa adhana na kilio cha Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) wote waliokuwepo Msikitini nao pia wakaanza kulia. Na baada ya kuweza kuimiliki nafsi yake, Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akaikamilisha adhana kwa sauti ndogo na hakuweza kuinyanyua sauti yake.

Baada ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) kuzikwa, Bilaal akaondoka na kujitenga mbali kidogo na watu huku akilia kwa huzuni. Ulipoingia wakati wa Swalah, watu wakawa wanamsubiri Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) awastareheshe kwa kuwaadhinia kwa sauti yake nzuri. Lakini Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) hakuadhini. Watu wakamkumbusha kwa kumwambia;

"Wakati wa adhana ushaingia ewe Bilaal".

Akasema huku machozi yakimlenga;

"Sitoadhini tena baada ya leo, bora aadhini mwengine badala yangu."

Sitoadhini Tena Baada Ya Kufa Kwa Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wa Sallam)

Wakati wa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipokuwa Khalifa wa Waislam, alimtaka Bilaal aadhini akamwambia;
"Adhini".
Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikataa, akamwambia;

"Ikiwa ulinikomboa kwa ajili ya nafsi yako basi nikamate, ama ikiwa kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, basi niache na Mungu wangu."
Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamwambia;
"Nilikukomboa kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu Peke Yake".

Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamjibu kwa huzuni;

"Basi mimi sitoadhini tena baada ya kufa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam)".

Baada ya kufariki Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akataka kwenda kupigana Jihaad, lakini Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimkatalia, akamwambia;
"Nakuomba kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ewe Bilaal, kwa hisani yako, umri wangu ushakuwa mkubwa na siha yangu ishadhoofika na ajali yangu ishakaribia, tafadhali baki hapa pamoja na mimi".

Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akakubali kuwa pamoja naye mpaka Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipofariki dunia.
Bilaal (Radhiya Allaahu ‘Anhu) Anakwenda Kupigana Jihaad
Alipotawala ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu), naye pia alimtaka Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) aadhini, naye akamkatalia pia ombi lake hilo, kisha ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamuuliza;

"Yupi unaona nimpe kazi ya kuadhini?"
Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema;

"Sa’ad, kwani yeye aliwahi kuadhini wakati wa Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam)".

Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamwendea ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kumuomba amruhusu kwenda kupigana Jihaad.
‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamwambia;
"Ewe Bilaal, hutaki kubaki pamoja nami kama ulivyokuwa pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) kisha pamoja na Abu Bakr?"
Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema;

"Natamani kwenda kupigana Jihaad ewe Amiri wa Waislam, na naona kuwa Jihaad ni miongoni mwa ‘amali bora kupita zote".‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamwambia;

"Fanya kama unavyotaka ewe Bilaal."

Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasafiri kuelekea nchi ya Shaam na kujiunga na jeshi lililokuwa likiongozwa na Abu ‘Ubaydah ‘Aamir bin Jarraah (Radhiya Allaahu ‘anhu).

Bilaal (Radhiya Allaahu ‘Anhu) Anaadhini Tena

Alipoitembelea nchi ya Shaam wakati wa Ukhalifa wake, ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) alionana tena na Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu), na Waislam wakamuomba ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) awaombee kwa Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) ili awaadhinie angalau mara moja tu ili wapate kuisikia sauti yake ‘adhimu aliyokuwa akiinyanyua kila siku mara tano wakati wa uhai wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam).
Ulipoingia wakati wa Swalah, ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamuomba Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) aadhini na Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akalikubali ombi lake, akapanda juu ya mlmbari na kuanza kuadhini. Nyoyo za watu zilikuwa zikipiga kwa nguvu huku wakiisikiliza sauti ya Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliyekuwa akiadhini kwa mara ya mwanzo tokea alipofariki Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam).
Imeandikwa katika kitabu cha Siyar A’alaam an-Nubalaa kuwa;

"Watu hawakupata kulia kama siku hiyo kwa ajili ya kukumbuka uhai wa Mtume wao (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam)".

Kifo Chake (Radhiya Allaahu ‘Anhu)

Haya kwa ufupi ni maisha ya Swahaba huyu mtukufu (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliyejitolea nafsi yake kwa ajili ya kuipigania dini ya Mwenyezi Mungu.
Alifariki katika mji wa Damascus mwaka wa ishirini baada ya Hijrah ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akiwa ana umri uliopindukia miaka sitini kwa maradhi ya tauni yaliyowaua watu wengi sana katika nchi ya Shaam.
Inasemekana kuwa roho yake ilipokuwa ikimtoka, mkewe alikuwa akimwambia;
"Huzuni iliyoje, huzuni iliyoje."

Lakini Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa akiyafumbua macho yake akasema;
"Bali furaha iliyoje, kesho nitaonana na wapenzi, Muhammad na Maswahaba.
"

"Bali furaha iliyoje, kesho nitaonana na wapenzi, Muhammad na Maswahaba."

WABUNGE WACHOCHEZI NDO CHANZO CHA UVUNJIFU WA AMANI.

www.fahadahm.blogspot.com
BAADA ya kubaini kuwa wao ndio chanzo cha uvunjifu wa amani kutokana na kauli zao bungeni, wabunge wameona haja ya kuangalia upya sheria, ikiwamo ya kinga ambayo inawapa uwezo wa kutoa kauli hizo.

“ Pande zote za wabunge zimekuwa zikitoa lugha za chuki ndani ya Bunge kwa kisingizio cha kinga, hili halifai, halifai, halifai, sisi tunaanzisha wimbo humu ndani na watu wanaitika. Tuzuie kauli za chuki ndani na nje ya Bunge,” amesema Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Anna Abdallah.

Akitangaza jana azimio kuhusu tukio la kulipuliwa bomu Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Arusha Jumapili, Anna alisema wabunge wengi wamekuwa wakitoa lugha za chuki kwa kisingizio cha demokrasia na kuwakumbusha kuwa hakuna demokrasia isiyo na mipaka.

“Hakuna haki utakayoipata kwa kuvunja haki ya mwingine, huwa najiuliza ni kwa nini kikundi kinaanzishwa kuipinga BAKWATA (Baraza Kuu la WaislamuTanzania) na kinasajiliwa?” alihoji.

Kuhusu shambulizi hilo, aliitaka Serikali kuchukua hatua dhidi ya viashiria vyote vya uvunjifu wa amani. Kwa azimio hilo, Bunge liliitaka Serikali kuhakikisha uchunguzi wa kina unafanywa na kuwatia nguvuni wahusika wote wa tukio hilo na kisha kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria, ili kuwapa wananchi matumaini ya kujumuika na kuabudu kwa uhuru bila hofu ya usalama wao.

Alisema katika miaka ya karibuni, zimekuwapo dalili za uvunjifu wa amani na utulivu ambapo baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakijeruhiwa, kuuawa na baadhi ya nyumba za ibada kuchomwa moto.

“Hali hii imekuwa ikiwatia hofu wananchi wa imani na hali zote na kuhoji kiini cha matukio haya, tukio la mlipuko wa bomu limeongeza hofu miongoni mwa Watanzania na kuendelea kutikisa misingi ya amani, utulivu na mshikamano miongoni mwao,” alisema Anna.

Alisema pamoja na kazi nzuri ya Serikali kukamata baadhi ya watuhumiwa, Bunge liliitaka Serikali na vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha wanatumia uwezo uliopo kuchunguza kwa kina na kuchukua hatua stahiki haraka.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira alisema hakuna mtu aliyehusika na mlipuko huo atakayepona na wote watashughulikiwa bila kujali hadhi zao.

Alitaka Watanzania kwa sauti moja kushinda vitendo vya kigaidi na kutolea mfano Marekani ambao baada ya matukio ya ugaidi waliungana bila kujali tofauti za kidini na kisiasa.

“Hakuna dini inayoogopa Mungu itakayounga mkono tukio lile na kama ipo basi wanaabudu kingine na si Mungu, na kuna chama au dini itafurahia hili labda kama hawatumikii wananchi,” alisema.

Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe (Chadema) alisema ongezeko la matukio hayo ni dalili kuwa nchi ina nyufa zinazotumiwa na maadui katika kuvuruga na kugawa Watanzania.

Alisema wakati umefika wa kuangalia sheria za nchi ili kuzuia lugha za chuki. Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, pamoja na kulaani tukio hilo, alisema kauli za viongozi wa dini na siasa zinakuwa kichocheo cha chuki katika jamii.

Akitolea mfano, Simbachawene alisema: “Tuangalie, hapa tunaweza kugombana, lakini tukitoka tunakumbatiana na kula pamoja, vivyo hivyo viongozi wa dini ambao wanaweza kupanga mambo yao pamoja, lakini kuna watu tunaowapelekea ujumbe ndio wanaoathirika na kujikuta wakitumika.”

Aidha, Simbachawene alitoa mwito kwa Watanzania kuwa ni vizuri kuangalia sheria za uhuru wa kuabudu na kutangaza dini na uhuru wa kufanya mihadhara. Mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Habib Mnyaa (CUF), alisema muda mrefu wananchi wamekuwa wakifurahia kwa amani na utulivu na hivi sasa chokochoko zinazojitokeza zinaweza kuipeleka pabaya nchi ikiwa wananchi hawatakuwa makini katika kudhibiti hali hiyo.

“Nahadharisha kuwa kama kuna baadhi ya watu kupitia mgongo wa siasa wanataka kutumia Waislamu pekee wanajidanganya na kama kuna watu kupitia siasa wanaweza kutumia makanisa kutawala nchi, hii haiwezekani,” alisema Mnyaa.

Aliomba vyombo vya ulinzi na usalama kuwa makini na kuacha kudhani kuwa huenda majanga hayo yanatokana na kauli za kwenye miadhara kwa kuwa kuna uwezekano zikachochewa na mataifa ya nje.

Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), aliitaka Serikali kutokuwa na kigugumizi katika kuchukua hatua kwenye majanga makubwa kama hayo na kuwa ipo haja kwa Serikali kusimamia Katiba na vyombo vya Dola kutekeleza wajibu wao bila kuegemea upande wowote.

Mbatia alionya wanasisasa wanaotumia muda mwingi kuanzisha chokochoko kwa viongozi wa dini na kuwa ni wajibu wa viongozi wa siasa wa pande zote, kutopenda kupata madaraka kwa kutumia damu ya Watanzania.

Mbunge wa Viti Maalumu, Fakharia Khamis Shomar (CCM), alitaka Watanzania kuungana katika kupambana na tatizo hili na kutaka wahusika kuchukua hatua za kisheria stahiki ambazo zitaridhisha kila mtu.

Mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema (TLP), alitaka vyombo husika vinavyotoa vibali vya uanzishwaji wa makanisa na vikundi vya dini kufuatilia kinachofanywa na watu hao.

“Siamini kwa Wakristo wanaohubiri wana sifa za kufanya hivyo, na pia tupige marufuku mihadhara yenye mwelekeo wa kashfa na matusi na yeyote atakayehusika apigwe marufuku na anyang’anywe leseni, natoa siku saba jambo hili lishughulikiwe.”

Mbunge Viti Maalumu, Getrude Rwakatare (CCM), alisema mashambulio hayo yamekuwa yakijitokeza kutokana na Serikali kuchukua hatua dhaifu na kuitaka ichukue hatua kwa ukamilifu na kupendekeza kupitia upya sheria hizo ili kunusuru nchi.

Wakati huo huo, Spika Anne Makinda aliongoza jopo wa wabunge 23 jana kwenda Arusha kuwapa pole wafiwa na majeruhi. Sambamba na hilo, wabunge walikubaliana kutoa posho yao ya siku moja ikiwa ni mchango wao kwa waathirika wa tukio hilo.

SERIKALI IMETOA TAMKO YA KUPIGA MARUFUKU MIHADHARA YA KIDIIN

MIHADHARA YA KIDIIN KUPIGWA MARUFUKUwww.fahadahm.blogspot.com
HATIMAYE Serikali imeanza kubaini sehemu ya kiini cha vurugu na vitendo viovu vinavyofanywa kwa kisingizio cha udini nchini na kutangaza hadharani kuwa mihadhara ya kidini inachangia.

Mihadhara kama mihadhara ambayo inalenga kueneza Neno la Mungu haina matatizo, lakini inapotumiwa kuhubiri mabaya ya dini nyingine, hapo ndipo inapopoteza umuhimu.

Lakini kwa kuwa sasa Serikali imeuona mchango wa mihadhara hiyo katika vurugu za kidini, ni dhahiri kwamba hatua zinapaswa kuchukuliwa, ikiwa ni pamoja na kutoa uamuzi mgumu ili kunusuru amani ya nchi.

Awali, waumini wa dini za kiislamu na kikristo, walidhani kuwa kuanzishwa kwa mihadhara hiyo kulilenga kuhubiri dini na kuwapa mafunzo mema waumini kama ifanyikavyo ndani ya majengo ya ibada.

Imani hiyo ndiyo ilifanya hata Serikali kudhani kweli hayo ndiyo yanayofanyika, lakini kumbe baadhi ya wahubiri ambao ni viongozi wa dini, walianza kutetereka na kutumia vibaya majukwaa ya mahubiri hayo.

Waliibuka waumini wa dini hizo mbili kubwa nchini, wakaanza kuchambua Biblia na Korani kinyume na makusudio, lengo likiwa ni kuonesha kuwa vitabu hivyo vitukufu si lolote bali vinadanganya waumini.

Polepole mahubiri hayo yaliachiwa kukithiri na kujenga chuki katika nyoyo na vichwa vya waumini na hatimaye dini moja kuonekana haifai na nyingine inafaa.

Bila shaka upotofu na upotoshaji huo ndio uliofanya sasa waibuke wanadini wanaovutana kuhusu nani achinje na nani asichinje, wakisahau kuwa huko nyuma jambo hilo lilifanyika bila ubishani wala ugomvi!

Mihadhara potofu ya kuponda dini nyingine, ndiyo iliyowafikisha Watanzania walipo hivi sasa ambapo mtu wa dini moja anamwangalia wa nyingine kwa jicho la chuki na husuda.

Mihadhara hii ambayo imekuwa ikifanyika katika maeneo ya wazi na kutumia vipaza sauti vyenye sauti kubwa mchana na usiku, imekuwa ikivuta hisia za wengi na wengine kushawishika kufanya hata mabaya yanayohubiriwa.

Chuki ya kidini hushika zaidi katika akili za binadamu na kuzama katika nyoyo zao na hivyo kuwa vigumu sana kumgeuza kirahisi aliyeamini na ndiyo sababu wengine huwa tayari kujitoa mhanga ‘kufia dini’.

Ikumbukwe, kwamba viongozi wa dini huaminika zaidi ya hata viongozi wa familia, kaya, siasa na hata serikali; wanalolisema wao linaaminika kwa sababu ndiyo njia ya kuuona ufalme wa Mbinguni.

Kutokana na ukweli huo, ndiyo sababu tumesikia vita vya wenyewe kwa wenyewe visivyomalizika katika nchi ambako chuki za kidini zimetamalaki.

Watanzania tunaelekea huko, tukioneana haya sasa na kuacha hali hii ijichimbie miongoni mwa jamii, matokeo yake yatakuwa mabaya na hakutakuwa na wa kulaumiwa ila sisi wenyewe.

Tufike mahali sasa tuone kuwa kuendelea na hali hiyo ni hatari kwa mustakabali wa nchi, kwani tutafikia mahali ambako tutapigana kidini vita ambavyo mwisho wake hakika ni mgumu.

Serikali sasa isimame kidete na kutoa kauli nzito, kwamba kuanzia sasa mihadhara ya kidini imepigwa marufuku na kama ni mafunzo ya dini na mahubiri yafanyike ndani ya makanisa na misikiti na majengo mengine ya ibada

يقولون إن مستشرقاً ذهب إلى السعودية فعاد مستغرباً

بدرية البشر
الأربعاء ٨ مايو ٢٠١٣

يقولون إن مستشرقاً ذهب إلى السعودية فعاد مستغرباً، أي متعجباً. قد تبدو هذه الحقيقة أكثر الحقائق التي تنطبق علينا هذه الأيام في تعاطينا مع المنصات الرقمية، وأشهرها «تويتر»، فنحن انكشفنا و«كل شي بان»، كما يقول عبدالمنعم مدبولي في مسرحية «ريا وسكينة».

«تويتر» أصبح اليوم أكثر التجارب التي يشترك فيها عدد كبير من السعوديين، ووفقاً لتقرير وكالة الوسائط الاجتماعية «ذا سوشال كلينيك»،- نقلته صحف عدة - فإن المملكة بها أكثر من ثلاثة ملايين مستخدم نشط لـ «تويتر» يُصدرون 50 مليون تغريدة في الشهر، كما سجل مستخدمو «تويتر» في المملكة نمواً قدره 3000 في المئة، بين عامي 2011 و2012، أي أعلى بكثير من المتوسط العالمي، لهذا لا تستغرب أن يعود كل مستشرق مستغرباً.

وفي «تويتر» تجد طرائف كثيرة، أشهرها ذلك الطالب الذي كتب تغريدة طلب فيها من متابعيه أن يجدوا له عذراً يكذب به على والده حتى لا يذهب إلى المدرسة غداً، فجاءه جواب يقول: «كن صريحاً مع أبيك، وقل له الحقيقة». وقد كان المرسل والده. والزوجة التي تقول لزوجها الذي ينضح رومانسية في «تويتر» أن يترك عنه هذا ويحضر معه خبزاً وحليباً للطفل في طريق عودته. لكن ليس كل ما يحدث في «تويتر» طريفاً، فهناك تغريدات ذهبت بأصحابها إلى السجن، وهناك تغريدات ذهبت بأصحابها إلى المحاكم. لكن الشيء الأكيد أن «تويتر» كشف ما هو «مغطى ومكشوف»، أهمه أزمة التربية والحرية لدينا، وأن التعدد الوحيد المقبول لدينا هو في الزوجات فقط، فأصبح «تويتر» مرتعاً للنعرات وللتطرف ولحرية الشتائم طالما لا أحد قادراً على تعقبك ومعاقبتك.

ويقال إن بعض القنوات الإعلامية الغربية وجدت في «تويتر» أهمية بكشف وقياس حرارة الرأي العام السعودي. لكن هل يمكن الاعتماد على هذا الموقع ليكون مرجعاً حقيقياً، لا أزال أشكك، لكن ما أنا متأكدة منه أن الوقوع في حبال «تويتر» قد أصبح تجربة فريدة لبعض السعوديين، فهناك من يقول إن «تويتر» غيّر حياته، ولا ندري بأي اتجاه، كيف لا!؟ وقد أصبح صديقاً لمن لا صديق له، وعدواً لمن لا عدو له، وجمهوراً لمن لا جمهور له، بل بات اليوم مثل قصة «بركة الجنون» التي تقول إن جميع من في القرية شربوا من ماء بركة أصابتهم بالجنون عدا شخصاً واحداً، فاكتشف أنه يشقى بعقله، فشرب معهم.

إن احتفظت بعقلك وظللت تتابع الجيل الجديد ونصف الجديد اليوم وهو يدفن رأسه في جواله ويدق بأصابعه سريعاً على أزراره فستصاب حتماً بالإحباط، وتستغرب لما يفضل هذه الجالس معك صحبة غيرك، وإن ذهب إليه سيجد آخر أبعد يحدثه وهكذا.

مشكلة «تويتر» أنه يعطيك عكس ما تحس به، أي يخدعك، فهو يوهمك أنك تزداد تواصلاً مع الناس في حين هو يزيدك عزلة، ويصور لك أنك تعيش حياة أجمل فيما هو يخرب حياتك الواقعية، وحين تظن أنك تتسلى فقط ستجد أنك وقعت في ما يشبه الإدمان بل الإدمان نفسه، حمرة في العيون، فقدان القدرة على السيطرة بترشيد التعاطي أو التوقف. ومن ثم خسارة شركائك في الحياة الذين ملوا من نصحك.

الغريب أن هذه النتائج الكبيرة لا تدل سوى على أين يقع أكثر الأسواق استهلاكاً بين الشباب، فلا أحد تثيره شهية الاستطلاع المعرفي السوسيولوجي، لا أحد يهتم بأن يعرف بماذا يفكر شبابه وبماذا يطمح، ما هي أزماته، وغريب أيضاً أن تكون لدينا كل هذه الكثافة والرغبة في الثرثرة المتمثلة في التمركز في منابر التعبير التي بسببها تحولت منصات الترفية إلى أغراض لغير ما جاءت من أجله، ولا أحد يهتم بدرسها، لا مراكز الأبحاث في الجامعات ولا شركات الرصد العلمي، فقط مراكز أجنبية تدل التجار إلى أفضل مكان يعلنون فيه سلعهم ويقتنصون زبائنهم
.

Monday, May 6, 2013

PICHA KUMI KUTOKA ENEO LA OLASITI JIJIN ARUSHA KULIPOTOKEA MLIPUKO WA BOMU MAPEMA ASUBUHI YA LEO ONA HAPA.

MAAGIZO ALIYOYATOA RAIS KIKWETE KUHUSU SHAMBULIO LA KIGAIDI LILILOFANYIKA HUKO ARUSHA -muhibu diin

PANGO LA VIJANA WA AS HAABUL KAHF(WATU WA PANGONI)

www.fahadahm.blogspot.com
cave of as habul kahf/pango la as habul kahfi ndani yake
Cave of Ashabe-Kahf (interior)

The main view above shows a section of the interior. The crafted stone blocks are tombs; one of them has a viewing hole through which bones can be seen (inset). The bones of the dog have also been displayed.

    The Prophet (s.a.w.) was challenged by the Quraysh of Makkah who did not believe in his message to answer three questions passed onto them by the Jews. One of the questions was, “Who were the youth who disappeared, and how many were they?” The Jews knew that the Prophet (s.a.w.) would only be able to tell the story if he was indeed a prophet.

    The Prophet (s.a.w.) had no clue and said that he would answer them tomorrow, hoping for the answer to be revealed to him through Jibraeel (a.s.) but forgetting to say ’Inshallah’ (if Allah wills). No revelation came to the Prophet (s.a.w.) for 15 days, leading the Quraysh to greatly abuse and revile him.

    The answer, however, was eventually revealed to the Prophet (s.a.w.) in a Surah named after the cave (Al-Kahf) of the sleepers. The Quran revealed the exact story that the Jews knew of, and it answered the questions similarly to the information they had. The Quran confirmed that they slept for 309 years, which the Jews knew of. The Quran however did not give an exact answer as to how many they were. Allah (swt) revealed:“(Some) will say: They were three, their dog the fourth, and (some) say: Five, their dog the sixth, guessing at random: and (some) say: Seven, and their dog the eighth. Say (O Muhammad): My Lord is best aware of their number. None knowth them save a few. So contend not concerning them except with an outward contending, and ask not any of them to pronounce concerning them.” [18:22]

    The Jews themselves did not know exactly how many there were (whether 3,5 or 7) and were astonished when the Quran gave all the possible numbers they had suspected for the number of sleepersPANGO LA WATU WAPANGONI

www.fahadahm.blogspot.com
inje ya pango

i love the holy qur'an

www.fahadahm.blogspot.com
qur'an is our life we believe that
ndani yake muna shifaa(ponyo ,dawa ya kila ugonjwa,kila tatizo)

Batle badri place

www.fahadahm.blogspot.com
mahala walipo pigana masahaba vita vya badri
mahala yalipo tokea mapambano ya vita vya badri
www.fahadahm.blogspot.com
kaburi la nabii ibrahim/tomb of ibrahim(a,s)
kaburi la nabii ibrahim (a,s)This is the tomb of Ebrahim (a.s.) which is built directly above his actual grave which is below ground. On the left side is the window from the Jewish synagogue which is built right next to the mosque. This place is a source of great friction between Muslims and Jews and is heavily guarded.

    Ebrahim (a.s.) is mentioned by name 69 times in the Holy Quran. He is known as ‘Khalil-ullah’, the friend of Allah. Ebrahim (a.s.) is considered the Patriarch of the three great monotheistic faiths, Judaism, Christianity and Islam.

    Almighty Allah has declared in the Holy Quran in Surah al-Imran: “O People of the Scripture (Jews and Christians)! Why do you dispute about Abraham, while the Torah and the Gospel were not revealed till after him? Have you then no sense? Verily, you are those who have disputed about that of which you have no knowledge. Why do then dispute concerning that which you have no knowledge? It is Allah Who knows, and you know not. Abraham was neither a Jew nor a Christian, but he was a true Muslim Hanifan (Islamic Monotheism), to worship none but Allah Alone and he was not of the polytheists (he joined none in worship with Allah). Verily, among mankind who have the best claim to Abraham are those who followed him, and this Prophet (Muhammad) and those who have believed (Muslims). And Allah is the Wali (Protector and Helper) of the believers.” [3:65-68]

    Ebrahim (a.s.), along with his eldest son Ismail (a.s.) rebuilt the Ka’bah in Makkah, carrying the stones with their own hands.

    Yahya bin Said bin al−Musayyub said, “Ebrahim, may Allah bless him and grant him peace, was the first to give hospitality to the guest and the first person to be circumcised and the first person to trim the moustache and the first person to see grey hair. He said, ‘O Lord! What is this?’ Allah the Blessed, the Exalted, said, ‘It is dignity, Ebrahim.’ He said, ‘lord, increase me in dignity!’ “

    Ebrahim (a.s.) died at the age of 175.
by :Ahmad muhibu diin
Email:halfanallyahmad@yahoo.com
Gmail:ahmadabdulhamid79@mail.com
call:+255717166644

احمد محب الدين الأخبار جديد/احب الله ورسوله

حبّ الرسول صلّى الله عليه وسلّم

قال عليه والصلاة والسلام <<من أحبّ سنّتي فقد أحبّني ومن أحبني كان معي في الجنة>>وقال تعالى<<قل إن كنتم تحبّون الله فاتبعوني يحبب كم الله و يغفر ذنوبكم>>

Popular Posts